Kwanini Rais Samia anatupiwa lawama?

Samia Suluhu Hassan aliapishwa baada ya kushinda kwa asilimia 98 ya kura katika uchaguzi wa Oktoba 29.

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 5

Tanzania bado imegubikwa na matokeo ya ghasia mbaya zaidi za baada ya uchaguzi, mgogoro ambao umetikisa sifa yake ya muda mrefu kama mwanga wa amani na utulivu barani Afrika.

Pia imepokea karipio adimu kutoka kwa mashirika ya kikanda na bara.

Idadi ya vifo haijulikani wazi lakini familia zinaendelea kutafuta au kuzika jamaa waliouawa kufuatia kura ya hivi karibuni, ambayo Rais Samia Suluhu Hassan alishinda kwa 98%.

Samia ni kiongozi mpole ambaye hulka yake ya utulivu na upole, mwanzoni ilichochea matumaini alipochukua madaraka mwaka wa 2021 baada ya kifo cha ghafla cha mtangulizi wake, John Magufuli.

Lakini hilo sasa limebadilika.

"Samia ameiingiza Tanzania katika kipindi kigumu cha maandamano, machafuko, na hali ya kutoeleweka," alisema Profesa Peter Kagwanja, mchambuzi wa sera kutoka Kenya, alipoongea na BBC.

Maandamano hayo, yaliyofanywa na vijana, yanarandana na harakati za kizazi cha Gen Z duniani kote zinazopinga uongozi uliozoeleka na serikali zisizowajali raia.

Wachambuzi wanasema ingawa machafuko hayo hayakuwahi kutokea kwa Tanzania, yalitanguliwa na hali ya kisiasa yenye msukosuko, iliyooneshwa na mageuzi yaliyokwama, miaka ya hasira kali ya vijana, mivutano ya madaraka ndani ya chama tawala na mateso endelevu ya viongozi wa upinzani.

Unaweza kusoma

"Maandamano hayo yalikuwa ni kilele cha miaka ya hasira na malalamiko ambayo yamezuiliwa na Watanzania," Godfrey Mwampembwa, mchoraji vibonzo wa kisiasa aliyezaliwa Tanzania, maarufu kama Gado, alisema.

Vibonzo vya kejeli vya Godfrey vinavyomuonesha Rais Samia kama mtu wa kimabavu na asiyevumilia ushindani wa kisiasa, vimesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Mazishi yamekuwa yakifanyika kwa baadhi ya waliofariki katika ghasia za baada ya uchaguzi

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwandishi wa habari mkongwe wa Tanzania, Jenerali Ulimwengu, alielezea katika makala jinsi uchaguzi wa hivi karibuni ulivyokuwa kilele cha hasira za ambazo zimekuwa zikijengeka taratibu miongoni mwa jamii kwa miongo kadhaa, bila kutambuliwa na uongozi usiojua kinachoendelea, ambao umezama kabisa katika starehe na manufaa ya madaraka.

Hisia kama hizo zilitolewa na Godwin, ambaye alishutumu chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa "kuficha kichwa chake kwenye mchanga" na "kutosikia sauti" ya wito unaoongezeka wa Watanzania wa mabadiliko.

"Kwa miaka mingi CCM imewanyima raia haki ya kupiga kura na kupuuza taasisi za serikali zinazoiweka madarakani," alisema msanii huyo, ambaye ana makao yake katika nchi jirani ya Kenya lakini amekuwa akifuatilia kwa karibu matukio katika nchi yake ya asili.

Charles Onyango-Obbo, mchambuzi wa kisiasa kuhusu masuala ya Afrika Mashariki, anakubali kwamba CCM "ilikuwa imechanganya utulivu kwa muda mrefu na ukomavu, lakini ilikuwa ni umri na kiburi tu kilichojificha nyuma ya historia tukufu".

Charles Onyango-Obbo, Mchambuzi wa masuala ya kisiasa ya Afrika Mashariki anaunga mkono hoja kwamba CCM ''ilichukulia utulivu wa Watanzania kuwa ukomavu, lakini ilikuwa ghadhabu iliojificha nyuma ya hekima iliyotokana na historia.

"Ilichanganya ukimya wa watu na amani, bila kutambua kuwa ilikuwa utulivu wa uchovu," aliandika.

Tofauti na wengine katika kanda, CCM, ambayo ilitokea kutoka Tanganyika African National Union, ni chama cha ukombozi baada ya ukoloni ambacho kimeendelea kudhibiti si tu madaraka bali pia akili na mitazamo ya taifa.

Lakini ni asili ya uchaguzi huu wa karibuni imefichua sura mpya ya kushangaza ya Tanzania, nchi ambayo kwa muda mrefu imeonekana kuwa na watu wasio na utamaduni wa kufanya maandamano, hasa ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya.

Katika miezi iliyotangulia siku ya uchaguzi, serikali ya CCM ilifanya kazi ya kuondoa ushindani wowote unaoaminika, kulingana na wachambuzi.

Kwenye miezi iliyotangulia kabla ya uchaguzi, serikali ya CCM ilifanya kazi ya kuondoa ushindani wowote unaoaminika, kulingana na wachambuzi.

Viongozi wawili wakuu wa upinzani walizuiwa kugombea, Tundu Lissu yuko kizuizini kwa mashtaka ya uhaini, ambayo anakanusha, huku ugombea wa Luhaga Mpina ukikataliwa kwa misingi ya sababu za kiufundi.

Kulingana na mtaalamu wa masuala ya utawala, Profesa Kagwanja, kitendo hicho pekee kilikwenda kinyume na kile ambacho Tanzania na Rais wake mwanzilishi Julius Nyerere walisimamia.

"Hamuwafungi wapinzani wenu, mnatafuta kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu dhidi ya upinzani," alisema Profesa Kagwanja.

Akijulikana kama Mama Samia, rais huyo mwenye umri wa miaka 65 sasa anakabiliwa na tuhuma zinazoongezeka za kuongoza serikali kandamizi inayohusika na kukandamiza maandamano ya kihistoria kwa nguvu.

Mtazamo wake wa uongozi ulipendwa mwanzoni ndani na nje ya nchi kwani aliruhusu vyama vya upinzani kuandaa mikutano na kukosoa serikali bila hofu.

Alikuwa ameahidi kuifungua tena Tanzania kwa ulimwengu kupitia mafundisho yake ya "4R", upatanisho, ustahimilivu, ujenzi upya na mageuzi.

Kwa kuwa alizaliwa na kukulia Zanzibar, kisiwa chenye uhuru wa nusu kinachojulikana kwa unyenyekevu na ukarimu, haikuwa jambo la kushangaza kwamba Samia alitia moyo hisia ya utulivu alipochukua madaraka mwaka wa 2021.

Waandamanaji vijana waliingia mitaani kulaani kile walichokiita ukosefu wa haki katika uchaguzi

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Lakini wachambuzi wanasema kuwa wakati Samia alipoanza kutazama uwezekano wa muhula wa pili, alianza kuona shinikizo la ndani la chama ndani ya CCM na kuibuka tena kwa upinzani kama tishio kwa malengo yake.

Kwa miaka mitatu iliyopita, alikuwa amebadilisha baraza la mawaziri mara nyingi na kuwabadilisha wakuu wa kijeshi na ujasusi, katika hatua zinazoonekana kama kuwaondoa wafuasi wa mtangulizi wake.

"Ndani ya CCM, alitumia mbinu kama ya Magufuli ya kudhibiti chama, Kuongeza madaraka kwake binafsi, na kuzungukwa na kundi dogo la wafuasi waaminifu waliokuwa msingi mkuu wa madaraka," alisema Profesa Kagwanja.

Ujanja wa kisiasa wa Samia, ambao ulimpa jina la utani "Simba jike" miongoni mwa wafuasi wake, ulizaa matunda kwani CCM ilimteua kama mgombea wake wa urais mnamo Januari.

Miezi kadhaa kabla ya uchaguzi, wimbi la utekaji nyara, kukamatwa na mauaji ya kikatili ya wanachama wa upinzani yaliikumba nchi, na kuharibu matumaini ya mageuzi na maridhiano.

Nafasi ya kisiasa ilikuwa imepungua sana katika kuelekea uchaguzi wa hivi karibuni, ambao ulifunikwa na kukatika kwa mtandao na amri ya kutotoka nje.

Mamia huenda wamekufa katika machafuko ya baada ya uchaguzi kulingana na upinzani. Mamlaka bado haijatoa idadi rasmi ya vifo.

Ghasia hizo zilikuwa za kushangaza kwa taifa ambalo lilikuwa limejenga taswira ya utulivu, makubaliano, na utulivu kwa karibu miongo sita.

"Hadithi ya ubaguzi wa Tanzania imeharibika," alisema Bw. Onyango-Obbo.

Katika hotuba ya kuapishwa, Samia alisema uchaguzi ulikuwa wa haki na uwazi lakini alikiri watu walikufa wakati wa maandamano. Aliwalaumu wahusika raia wa kigeni kwa maandamano hayo mabaya.

Katika ukosoaji wa nadra, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika ya kikanda walisema ushindi wa uchaguzi wa Samia haukukidhi viwango vinavyokubalika vya kidemokrasia, wakitaja udanganyifu wa kura, ukandamizaji na dosari za kimfumo.

Upinzani mkuu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilipuuza matokeo hayo kama "ya udanganyifu".

"Changamoto ya Samia haikuwa kushinda uchaguzi, badala yake, ilikuwa ni kushinda mioyo na akili za Watanzania na Waafrika Mashariki ndipo alipochaguliwa katika shindano la haki. Kwa masikitiko, Samia alichagua kutawazwa. Alifunga njia zote za shindano la haki," alisema Profesa Kagwanja.

Anapoanza kutumikia muhula wake wa pili ofisini, wachambuzi wanasema Samia anakabiliwa na uchunguzi wa kimataifa unaoongezeka ambao unaweza kudhoofisha uhalali wake wa kuongoza nchi hiyo ya Afrika Mashariki.