Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 03.02.22: Pochettino, Silva, Militao, Zaniolo, Dybala, Keane, Saliba

Mauricio Pochettino

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mkufunzi wa PSG Mauricio Pochettino anayenyatiwa na Manchester United

Mkufunzi wa PSG raia wa Argentina Pochettino, 49 anasemekana kuchoshwa na ukosoaji ambao amevumilia katika mji mkuu wa Ufaransa na hana nia ya kusalia na klabu hiyo zaidi ya msimu huu. (Footmercato - kwa Kifaransa)

Manchester United wanazidi kujiamini kuwa wanaweza kumteua kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino kama meneja wao wa kudumu katika majira ya joto. (Mirror)

Manchester City wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 tayari kuwa na mkataba unaoendelea hadi 2025. (Times, usajili unahitajika).

Diego Militao

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa kati wa Real Madrid Mbrazil Eder Militao, 24, anasakwa na mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel msimu wa joto kama mbadala wa Mjerumani Antonio Rudiger, 28, na Mdenmark Andreas Christensen, 25, ambao wote wanaweza kuondoka wakiwa huru mwishoni mwa msimu. (AS - kwa Kihispania)

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema klabu hiyo itafanya kila iwezalo kumsajili tena mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30 Alexandre Lacazette kutoka Arsenal msimu wa joto. (Sun)

Tottenham na Juventus zote zinavutiwa na winga wa Roma mwenye umri wa miaka 22 Nicolo Zaniolo. (Calciomercato - kwa Kitaliano)

Nicolo Zaniolo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tottenham na Juventus zinavutiwa na winga wa Roma Nicolo Zaniolo (Kulia)

Mabingwa wa Italia Inter Milan na wapinzani wao wa jiji la AC Milan wako tayari kumenyana na Real Madrid katika usajili wa beki wa kati wa Arsenal wa chini ya miaka-21 William Saliba, 20, ambaye yuko Marseille kwa mkopo. (Calciomercato - kwa Kitaliano)

Real Madrid wanafikiria kutumia kipengele cha kumnunua tena katika kandarasi ya Sergio Reguilon ili kumsajili tena beki huyo wa miaka 25 kutoka Tottenham katika msimu wa joto. (ABC - kwa Kihispania)

Liverpool, Chelsea, Arsenal, Manchester City, Tottenham na Manchester United zote zimepewa nafasi ya kujadili uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala msimu huu wa joto baada ya mazungumzo ya Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 28 kuhusu kandarasi mpya kuvunjika. (90min)

Paolo Dybala

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala

Barcelona wanasemekana wamebainisha Manchester United na Juventus kama vilabu vinavyotaka kumsajili winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ambaye atakuwa mchezaji huru msimu wa joto. (Sport - in Spanish)

Klabu ya Wayne Rooney inayokabiliwa na changamoto za kifedha Derby County wamekubali ofa ya £600,000 ya Aston Villa la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Ireland Kaskazini wa miaka 16 Omari Kellyman. (Sun)

Klabu ya Lille nchini Ufaransa imekataa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa zamani Jack Wilshire ambaye anasalia kuwa mchezaji huru baada ya kutolewa na Bournemouth mwezi Mei mwaka jana. (L'Equipe, via Metro)

Jack Wilshere

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa zamani wa Bournemouth Jack Wilshire

Mlinzi wa Blackburn Rovers Darragh Lenihan, 27, anatakiwa klabu ya Ligi ya Marekani New York Red Bulls na inasemekana wanajiandaa kuwasilisha "ofa nono" kumnunua kiungo huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland. (Football Insider)