Mwanamfalme Andrew apoteza vyeo vyake vya kijeshi na ufadhili

Mwanamfalme Andrew

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamfalme Andrew

Mwanamfalme Andrew amepoteza vyeo vyake vya kijeshi na ufadhili na hatoitwa tena jina linalopatiwa wafalme la HRH.

Majina ya kijeshi ya Duke wa York na ufadhili wa kifalme umerudishwa kwa Malkia,Kasri la Buckingham limetangaza.

Mwanamfalme Andrew pia ataacha kutumia jina la ukuu linalopatiwa wafalme la HRH , ufalme huo umeongezea .

Majukumu yake sasa yatasambazwa miongoni mwa wanachama wa familia ya kifalme.

Haya yanajiri huku akiwa anakabiliwa na kesi kuhusu madai ya kumnyanyasa kingono mwanamke mmoja alipokuwa na umri wa miaka 17, jambo ambalo amekuwa akikanusha mara kwa mara.

Jaji mmoja siku ya Jumatano aliamuru kwamba kesi iliyoletwa na Virginia Giuffre inaweza kuendelea, baada ya Andrew kujaribu kuiondoa.

Kasri la Buckingham lilisema katika taarifa: "Kwa idhini na makubaliano ya Malkia, ushirika wa kijeshi wa Duke wa York na ufadhili wa kifalme umerudishwa kwa Malkia.

"Duke wa York hatowakilisha ufalme kwa kazi yoyote ya umma na atajitetea katika kesi hii kama raia wa kawaida."

Ataacha kutumia jina la 'Ufalme Wake' katika nafasi yoyote rasmi, waliongeza.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi alisema haikuwa na maoni yoyote kuhusu vyeo vya kijeshi vya Ndrew kurudishwa kwa Malkia, na kwamba ni suala la Kasri hilo

tunazidi kukupasha...