Virginia Giuffre: Tunayoyajua kuhusu mwanamke anayemshutumu Mwanamfalme Prince Andrew kumnyanyasa kingono

Virginia Giuffre arriving for hearing in the criminal case against Jeffrey Epstein, at Federal Court in New York, U.S., August 27, 2019.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Virginia Giuffre aliwasilisha kesi dhidi ya Mwnamfalme Andrew nchini Marekani

Mwanamke Mmarekani Virginia Giuffre anasema alikuwa muathiriwa wa biashara ya ngono na unyanyasaji huo uliotekelezwa na Jeffrey Epstein na washirika wake wenye mamlaka wakati alipokuwa msichana mwenye umri wa kubalehe.

Sasa yuko katika makabiliano ya kisheria katika kesi maarufu zaidi, baada ya kuanzisha kesi ya kiraia dhidi ya Mwanamfalme wa Uingereza Prince Andrew.

Ufalme umekuwa ukikanusha madai yake ya unyanyasaji wa kingono. Lakini juhudi za mawakili wa Mwanamfalme za kutaka kesi hiyo itupwe katika hatua za mwanzo zimegonga mwamba, na kesi dhidi yake inatarajiwa kuendelea jijni New York katika majira ya vuli.

Haya ndio tunayoyafahamu kumhusu Bi Virginia Giuffre:

'Utoto ulichukuliwa'

Bi Giuffre alizaliwa kama Virginia Roberts katika mwaka 1983 katika jimbo la Marekani la California. Baadaye familia yake kuhamia katika jimbo la Florida.

Akiwa na umri wa miaka saba, alinyanyaswa kingono na rafiki wa familia , na utoto wake ulichukuliwa haraka".

"Nilikuwa tu muoga kiakili tayari katika umri mdogo kiasi kile, na nikakimbia mbali na hilo ,"alikiambia kipindi cha BBC Pamorama katika mwaka 2019.

Baadaye katika utoto wake, alilelewa mara kadhaa na mlezi asiye wa familia yake. Na alipokuwa na miaka takriban 14, alikuwa akiishi mitaani ambako anasema hakupata chochote "isipokuwa, njaa na maumivu na unyanyasaji [zaidi] ".

Ilikuwa mwaka 2000, wakati alipokuwa akijaribu kuyajenga maisha yake upya, ndipo alipokutana na nyota wa kijami Ghislaine Maxwell.

BBC
Maelezo ya picha, Virginia Giuffre: "Ninawataka watu wa Uingereza ...kutokubali hili kama kitu ambacho ni SAWA

Bi Giuffre alikuwa kama mtunzaji wa funguo katika hoteli ya kifahari Donald Trump ya Mar-a-Lago resort iliyoko kwenye eneo la mwambao wa Palm Beach, ana anasema Maxwell alimpa ofa ya kupata mafunzo kama msingaji (mfanya masaji)

"Nilimkimbilia baba yangu ambaye anafanya kazi katika uwanja wa tenisi katika hoteli ya Mar-a-Lago, na anajua ninataka kuinua maisha yangu wakati huo, ndio maana alipata kazi pale. Nilisema : 'Nilimwambia hauwezi kuamini hili baba'," alikumbuka.

Kukutana na Epstein

Wakati Bi Giuffre alipowasili katika nyumba ya Epstein katika Palm Beach, anasema alikuwa amelala chini uchi na alielekezwa na Maxwell kuhusu jinsi anavyopaswa kumsinga.

"Ingawa wakati ule walikuwa wakiniuliza mimi maswali kuhusu nilikuwa nani.

"Walionekana kama watu wazuri kwahiyo niliwaamini, na nikawaambia nilikuwa na kipindi kigumu sana katika maisha yangu hadi wakati ule- Nilitoroka, niliwahi kunyanyaswa kingono, kupigwa…Hilo ni jambo baya sana ambalo niliweza kuwambia kwasababu sasa walijua ni jinsi gani niliweza kunyanyaswa kwa urahisi, aliiambia BBC.

Bi Giuffre alisema kwamba kile alichotarajia kuwa mtihani wa kazi, kiligeuka haraka kuwa miaka ya unyanyasaji.

Maxiwell alipatikana na hatia mwezi uliopita ya kuwaajiri na kuwasafirisha wasichana kwa ajili ya Epstein kuwanyanyasa, na anastahili kuhukumiwa.

Huku Bi Giuffre alielezea mara nyingi mahakamani, hakuwa mmoja wa wanawake wanne ambao walitoa ushahidi katika kesi ile. Maxwell alikana kumyanyasa.

Mwaka 2015, Bi Giuffre aliwasilisha kesi ya kuharibiwa sifa dhidi ya Maxwell, baada ya kumshutumu kuwa muongo. Kesi hiyo ilimalizwa nje ya mahakama.

Madai ya Mwanamfalme Andrew

Bi Giuffre anasema alianzia kunyanyaswa na Epstein hadi "kupokezwa kama sahani ya matunda" miongoni mwa washirika wa karibu, kwani alipelekwa katika maeneo mbali mbali ya dunia katika ndege za kibinafsi aina ya jeti.

Mwaka 2001, akiwa na umri wa miaka 17, anasema Epstein alimleta London na kumfahamisha kwa Mwanamfalme Andrew (Prince Andrew)

Picha maarufu sasa ambayo anasema alipigwa usiku ule inamuonyesha Mwanamfalme Andrew akiwa amezungusha mkono kiunoni mwa Bi Giuffre, huku Maxwell akitabasamu nyuma yao.

Virginia Giuffre describes how she asked Jeffrey Epstein to take this picture of her with Andrew.

Chanzo cha picha, Virginia Roberts

Maelezo ya picha, Virginia Giuffre anasema aliombwa na Jeffrey Epstein kupigwa picha na Mwanamfalme Andrew.

Baada ya kwenda kwenye ukumbi wa usiku wa starehe ( nightclub), Bi Giuffre anasema aliambiwa na Maxwell kwamba "ninatakiwa kumfanyia Mwanamfalme Andrew kile ninachokifanya kwa Jeffrey".

"Ulikuwa ni muda wa kutisha kusema kweli maishani mwangu…Sikuwa nimefungwa mnyororo kwenye sinki, lakini watu hawa maarufu wenye mamlaka walikuwa minyororo yangu," aliiambia BBC.

Katika kesi yake ya kiraia. Bi Giuffre alidai kwamba mwanamfalme alimnyanyasa kingono mara tatu- katika nyumba ya Maxwell mjini London usiku ule, na baadaye katika nyumba ya Epstein iliyopo Manhattan na Little St James katika visiwa vya Virgin.

Mwanamfalme Andrew, ambaye ni mwana wa pili wa kiume wa Malkia wa Uingereza , alisema katika mahojiano na kipindi cha BBC Newsnight mwaka 2019 kwamba hakumbuki kuwa alikutana na Bi Giuffre, na, katika kujibu shutuma kwamba walifanya ngono pamoja nchini Marekani na Uingereza, alisema kwamba "haikutokea".

Kuachana naye

Bi Giuffre aliliambia gazeti la Miami Herald kuwa mwaka 2003 Epstein alikuwa amemchoka na hakuwa na nia naye kwasababu alikuwa mzee sana kwake.

Alisema kuwa alimshawishi tajiri huyo wa fedha kumlipia kupata mafunzo ili awe msingaji wa taaluma na akampangia kupata masomo katika Thailand.

Lakini pia alitarajiwa kumleta nyumbani msichana wa Kithailand ambaye Epstein alikuwa amepanga aje Marekani.

Unaweza pia kusoma:

Badala yake, Bi Giuffre alikutana na mwanaume katika safari hiyo ambaye alimpenda na wakaoana siku 10 baadaye. Alihamia Australia pamoja naye kuanza familia.

Bi Giuffre sasa anaishi katika nyumba kubwa iliyoko ufukweni mwa Perth na mume wake pamoja na watoto wao watatu.

Ameanzisha shirika lisilo la faida linaloitwa, Speak Out, Act, Reclaim (SOAR), linalolenga "kuwaelimisha na kuwatetea waathiriwa wa biashara ya usafirishaji wa watu ".

Kufuatia uamuzi wa mahakama dhidi ya Maxwell mwezi uliopita, Bi Giuffre aliliambia jarida la New York ''bila shaka hili halijamalizika''

" Kuna watu wengi sana wanaohusika na hili ," alisema.