Penalti za laana: Walikosa kufunga penalti hizi na kuwaacha na majonzi mashabiki wa timu zao

Gyan

Kama kuna wakati wenye presha ya hali ya juu katika soka ni wakati wa kupiga penati. Mara nyingi mpiga penati anakuwa kwenye wakati mgumu zaidi kwa kuwa anakabiliana na mlinda mlango tu ambaye wakati huo hana sana cha kupoteza ukiliganisha na Mpiga penati. Akifungwa hana lawama sana kama mpiga penati akipoteza.

Presha kubwa Zaidi ni upigaji wa penati au matuta yanayotafsiri mshindi wa mechi husika. Mara nyingi ni zile penati tano tano, hizi ni penati ngumu na zenye presha zaidi pengine kuliko aina yingine yoyote ya mpira wa kutengwa ama mpira wa kawaida kwenye mchezo wa soka. Katika hali ya kawaida mchezaji soka aliyekamilika hategemewi kukosa penati kirahisi katika yumbali wa mita 12 uliowekwa. Lakini imeshuhudiwa wachezaji wakubwa duniani wakikosa mikwaju ya penati, lakini zipo penati ambazo haziwezi kusahaulika kirahisi katika ulimwengu wa soka. BBC inakuletea mikwaju kumi ya penati iliyokoswa, ambayo imewaliza mashabiki wengi na haitasahaulika kirahisi katika soka.

soka

Chanzo cha picha, Getty Images

10. David Trezeguet (Fainali ya kombe la Dunia 2006 )

Wengi watakumbuka fainali za kombe la dunia za mwaka 2006 , kwa tukio la gwiji la Ufaransa, Zinedine Zidane la kumpiga kichwa Marco Materazzi wa Italia katika dakika za nyongeza. Lakini tukio la kukumbukwa zaidi ni mkwaju wa penati wa David Trezeguet baada ya timu hizo kwenda sare ya 1-1 mpaka dakika 120 zinakatika. Matokeo yakiwa 2-2 , David Trezeguet anakosa mkwaju wake wa penati, ambao kwa kiwango chake cha ufungaji wakati huo, usingedhania angepiga penati juu kama ilivyotokea. Ufaransa walilizwa na penati hii.

Neymar has scored 84 goals in 109 games for PSG

Chanzo cha picha, Getty Images

9: Neymar v Colombia (2012)

Neymar, nyota wa Brazil pamoja na uwezo wake uwanjani usio na mashaka, alikosa penati dhidi ya Colombia kwa kupaisha juu kabisa ya mlingoti wa goli. Baadae akalaumu ubovu wa kiwanja kama kumesababisha kukosa kwake penati hiyo. Wabrazil walilia hawakuamini.

8: Chris Waddle v West Germany (1990)

Penati zimegharimu England kwa miaka miaka mingi, ambapo nyota wakew kadhaa wamekosa mikwaju ya penati na kufanya timu ya taifa hilo kuondolewa kwenye michuano mikubwa. Stuart Pearce, Gareth Southgate, David Batty, David Beckham, Ashley Cole, Steven Gerrard, Jamie Carragher na Frank Lampard have wote walikosa penati kwa nyakati tofauti. Lakini penati ya Chris Waddle katika nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 1990. Penati ya Waddle ilipaa juu ya lango , na kuanzia hapo mara nyingi kwenye mikwaju ya penati England hukutana na dhahma ya kukosa.

7:Landon Donovan v Real Salt Lake (2009)

Wako wachezaji wakienda kupiga penati, huna mashaka kwamba lazima wafunge, Landon Donovan ni mmoja wao. Lakini mwaka 2009, L.A Galaxy ilipovaana na Real Salt Lake kwenye kombe la MLS, Donovan alikosa kwa kupaisha juu na kusababisha vibonde Real Salt Lake kushinda kwa mikwaju 5-4.

6: Peter Devine v Whitley Bay (1992

Penati ya Peter Devine ilikuwa kama mchezo wa kuigiza, kila mtu alishangazwa nayo na kutoamini. Ilikuwa mwaka 1992, wakati Devine anakwenda kupiga mpira alijigonga mwenyewe na kuumia lakini katika kujigonga huko akaugusa mpira ambao ulisogea kidogo tu kama miguu 6 tu kuelekea langoni . Wengi hawaisahau penati hii.

pirez

Chanzo cha picha, Getty Images

5: Robert Pires v Manchester City (2006)

Baada ya kufunga penati nzuri tu katika mchezo huo dhidi ya Man City, Robert Pires wa Arsenal akadhani anaweza kurejea alichokifanya awali lakini kwa namna tofauti . Mwaka 1982 Johan Cruyff alifanikiwa kutoa penati pasi kwa mwenzake aliyemrejeshea na kufunga. Pires badala ya kumpasia Thierry Henry, akaugusa na kukimbia mbele. Ilikuwa penati ya ajabu.

beckham

Chanzo cha picha, Getty Images

4: David Beckham v Portugal (2004

Ni ngumu kukosa waingereza kwenye orodha ya penati za kukumbukwa. Ilikuwa robo fainali ya Euro Euro 2004 ambayo iliwaumiza waingereza wengi wapenda soka. Safari hii David Bekham alikosa mkwaju wa penati, ikiwa ni ya tatu kukosa mfululizo, ikiwemo moja kwenye mashindano hayto hayo.

chelsea

Chanzo cha picha, chelsea

3:John Terry v Manchester United (2008)

John Terry anakiri kwamba anateswa na kukosa kwake penati kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Man Utd mwaka 2008. Palinyesha mvua kidogo jijini Moscow, wakati matokeo ya mikwaju yanasoma 4-4 , kila mmoja akiamini nahodha Terry anakwenda kuwapa ubingwa wa Ulaya Chelsea, Terry anateleza na kupiga nje. Hata hivyo alipoza machungu mwaka 2012 alivyobeba kombe hilo dhidi ya Bayern Munich.

Gyan

2: Asamoah Gyan v Uruguay (2010)

Ilikuwa siku ya kuumiza kwa waghana na Waafrika kwa ujumla. Dakika za lala salama, Nahodha wa Ghana, Gyana anakosa penati kwa kupaisha juu katika robo fainali dhidi ya Uruguay. Kama angepata ingekuwa mara ya kwanza kwa timu ya Afrika kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

baggio

1: Roberto Baggio v Brazil (1994)

Penati hii iliwaumiza si waitalia tu, bali wapenda soka, kwa sabau gwiji huyu, Roberto Baggio alikuwa anapendwa na mashabiki wengi wa soka. Ilikuwa fainali ya kombe la dunia mwaka 1994, alipokosa mkwaju wake muhimu ambao ungeipa ubingwa Italia. Akiwa na jezi namba 10 anapaisha penati yake na kuwafanya Brazil kutwaa kombe la nne la dunia katika historia ya michano hiyo. Iliwaduza wengi.