Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 09.06.2021: Nuno, Pellegrini, Haaland, Niguez, Silva, Loftus-Cheek, Neves, Willems

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wanamtaka Hector Bellerin na huenda wakamuachilia tena kiungo wa kati wa Wales wa miaka 30 Aaron Ramsey katika mkataba wa kubadilishana wachezaji na Gunners. (Sport, in Spanish)
Kocha wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo anakaribia kuteuliwa kuwa meneja wa Crystal Palace. (Telegraph, subscription required)
Liverpool wametangaza dau la pauni milioni 25.8 kumnunua nahodha wa Roma na kiungo wa kati wa Italia Lorenzo Pellegrini, 24, kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Georginio Wijnaldum,30. (Corriere dello Sport, via Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Atletico Madrid wamemtoa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 26, kwa Manchester City ili wampate mshambuliaji wa Ureno Bernardo Silva, also 26. (Times)
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, anapania kujiunga na Chelsea na yuko tayari kusubiri kwa mwaka mmoja kuhamia Stamford Bridge. (Telegraph, subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Liverpool na Japan Takumi Minamino amehusishwa na tetesi za kurejea Southampton ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita baada ya kocha wa Saints Ralph Hasenhuttl kuulizia mpango wa kiungo huyo wa miaka 26. (HampshireLive)
Mhispania Dani Ceballos, 24, amesema anataka kurejea La Liga msimu ujao baada ya nkataba wake wa mkopo Arsenal kutoka Real Madrid kumalizika. (Cadena SER, via Evening Standard)

Chanzo cha picha, EPA
Arsenal wamefanya mazungumzo na Wolves kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, wakati Gunners wakijiandaa kupanga orodha ya wachezaji wanaopigiwa upatu kujaza nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Swizi Granit Xhaka, 28, ambaye anakaribia kujiunga na Roma. (Goal)
Bayern Munich wamefufua mkakati wa kumsaka winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi,20, mabingwa hao wa Champions League wako tayari kupokea ofa ya kumuuza. (Times, subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Brighton Graham Potter bado anagombea kuwa kocha mpya wa Evertonbaada ya Carlo Ancelotti kuondoka. (Athletic, usajili unahitajikaku)
AC Milan wamefahamishwa kwamba kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Brahim Diaz,21, kwa mkataba wa kudumu kutoka Real Madrid kutawagharimu euro milioni 26m, lakini klabu hiyo ya La Liga iko tayari kumtoa tena kwa mkopo nyota huyo. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Roy Hodgson amekataa ombi la West Brom la kumtaka awe kocha wo mpya. (Football Insider)














