Wafahamu makocha 10 matajiri zaidi duniani katika ulimwengu wa kandanda

Chanzo cha picha, Getty Images
Huku makocha wengi wa soka wakiendelea kukosa umaarufu ikilinganishwa na wachezaji wao ,mkufunzi ni kiungo muhimu katika kubaini hatma ya timu uwanjani.
Wakufunzi huchukua jukumu la kuwa washawishi .Ndio wanouhusika na kuwafunza wachezaji kufikia kiwango cha juu cha mchezo.
Ndio wenye jukumu la kutathmini wapinzani na kutafuta mkakati wa kupata ushindi. Ili kufikia kiwango kizuri cha mchezo , klabu kubwa hutafuta wakufunzi bora ili kusimamia klabu hizo.
Hatahivyo wakufunzi bora pia huzigharimu timu zinazowasaka. Katika miongo miwili iliopita baadhi ya makocha wameanza kupokea fedha nyingi zaidi ya wachezaji wao.
Hivyobasi bila kupoteza wakati tuwaangazie makocha kumi tajiri zaidi duniani 2021.
10. Rafael Benítez - Ana thamani ya €13M

Rafael Benítez
Mkufunzi huyo wa zamani wa Real Madrid na Liverpool yupo katika nafasi ya 10 katika orodha ya makocha tajiri zaidi duniani. Kwasasa anaifunza klabu ya Dalian Proffessionals. Huku akipokea mshahara wa €13M, mkufunzi huyo wa Uhispania yupo katika nafasi ya 10.
Benitez alichaguliwa kuwa kocha mpya wa Newcastle mwaka 2016 katika jaribio la kuzuiwa kushushwa daraja.
Alishindwa kuzuia klabu hiyo kushushwa daraja lakini akafanikiwa kuisaidia kupanda tena daraja hadi ligi ya Premia 2019 baada ya kuibuka mshindi katika ligi ya mabingwa nchini England.
Aliondoka katika klabu hiyo 2019 na kujiunga na Daliam Proffessionals , klabu ya China Superleague.
Rafael Benitez alijipatia umaarufu mkubwa wakati klabu yake ya Liverpool ilipotoka nyuma na kuilaza AC Milan katika michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya 2005.
9. Massimiliano Allegri - Ana thamani ya €13.5M

Chanzo cha picha, Getty Images
Allegri ni miongoni mwa wakufunzi tajiri duniani.
Massimiliano "Max" Allegri ni mchezaji wa zamani wa Itali , ambaye mara ya mwisho aliifunza klabu ya Juventus .
Allegri yuko katika nafasi ya tisa. Kocha huyo wa Itali alijishindia mataji manane katika ligi ya Serie A akiifunza Juve.
Pia alifanikiwa kufika fainali mbili na Juventus lakini akashinda kushindwa taji hilo. Wakati Allegri alipokuwa meneja wa klabu hiyo , alifanikiwa kuandikisha ushindi wa asilimia 70 ambapo wakati huo ndio uliokuwa wa juu zaidi katika historia ya klabu hiyo.
Allgeri alikuwa kiungo wa kati aliyechezea klabu tofauti nchini Itali. Akiwa na mapato ya jumla ya €13.5M na thamani ya $5m, Massimiliano Allegri ameorodheshwa katika orodha ya wakufunzi 10 bora duniani.
8. Fabio Cannavaro - ana thamani ya €14m

Chanzo cha picha, Getty Images
Fabio Cannavaro ni mmoja ya wakufunzi tajiri zaidi duniani.
Cannavaro ni mchezaji wa zamani wa Itali na meneja wa sasa wa klabu ya Guangzhou Evergrande. Akiwa mchezaji , Cannavaro alikuwa beki wa klabu tofauti za Itali. Anashikilia rekodi ya kuwa beki wa pekee kushinda taji la Balon d'Or.
Akiwa na thamani ya $45 Million, Cannavaro ni miongoni mwa wakufunzi tajiri duniani. Kandarasi yake kwa sasa inamsaidia kujipatia €12m kwa mwaka. Chini ya usimamizi wake Klabu hiyo ya China imefanikiwa kushinda kombe la China la FA 2018 na ligi ya China 2019.
7. Ernesto Valverde - Ana thamani ya €19M

Chanzo cha picha, Getty Images
Ernesto Valverde
Ernesto Valverde Tejedor ni mchezaji wa mpira wa zamani wa Uhispania ambaye alicheza kama mshambuliaji na sasa ni mkufunzi.
Kama mchezaji, Valverde alifunga mabao 68 katika mechi 264 katika La Liga. Baada ya kustaafu kama mchezaji, aliendelea na kazi kubwa ya kuwa mkufunzi.
Ernesto alishinda mataji mawili na klabu ya Olympiacos 2008-09 na 2011-12 na Barcelona 2017-18. Valverde alifutwa kazi mwaka huu baada ya msimu mbaya na Barcelona , baada ya kupoteza kwa Bayern Munich 8-2.
6. Zinedine Zidane - ana thamani ya €23M

Zidane ni mongoni mwa mameneja 10 tajiri zaidi duniani. Kwa jina maarufu Zizou ni mchezaji wa zamani wa Ufaransa.
Akiwa mkufunzi amekuwa akipokea €23M kwa mwaka na ana thamani ya €62m, thamani inayomfanya kuwa miongoni mwa wakufunzi tajiri zaidi duniani.
Ndiye aliyekuwa mkufunzi wa Real Madrid hadi hivi majuzi alipojiuzulu. Kiungo huyo wa zamani ni miongoni mwa wachezaji wachache walioshinda kombe la klabu bingwa Ulaya akiwa mchezaji na meneja.
Pia anashikilia rekodi ya kushinda mataji matatu ya klabu bingwa akiwa mkufunzi.
5. José Mourinho - Ana thamani ya €23M

Chanzo cha picha, Getty Images
Jose Mourinho ni miongoni mwa wakufunzi bora duniani na tajiri . José Mário dos Santos Mourinho Félix ni raia wa Ureno na aliyekuwa meneja wa klabu ya ligi ya premia Tottenham Hotspurs.
Ana sifa za kuwa miongozi mwa wakufunzi bora akipatiwa jina la The 'Special One'. Baada ya kufutwa Manchester United mwezi Disemba 2018, Jose Mourinho alisalia bila klabu kwa zaidi ya mwaka mmoja huku akikataa ofa kutoka klabu kadhaa kabla ya Tottenham Hotspurs kumsajili Novemba 2019.
Jose Mourinho amejishindia mataji mengi akiwa mkufunzi baada ya kushinda mataji sita katika misimu miwili. Mkufunzi huyo wa Uareno amekuwa akipokea €23M na thamani yake kwa jumla inadaiwa kuwa kati ya $50m - $100m, thamani inayomfanya kuwa mmoja wa mameneja tajiri zaidi duniani.
4. Jürgen Klopp - Ana thamani ya €24M

Chanzo cha picha, Getty Images
Jurgen Klopp
Jürgen Norbert Klopp ni raia wa Ujerumani na mchezaji wa zamani ambaye ndiye meneja wa Liverpool .
Anaonekana na wengi kama mkufunzi bora zaidi. Ni shabiki wa mbinu ya Gegenpressing, ambapo baada ya timu kupoteza mpira , inajitolea kutafuta mpira na kuuchukua tena badala ya kurudi nyuma na kusubiri adui.
Jurgen Klopp amefanikiwa kama meneja , akishinda taji la klabu bingwa na ligi ya Premia akiifunza Liverpool FC.
Jurgen Klopp ana thamani ya $50million, thamani inayomfanya kuwa miongoni mwa makocha tajiri England .
3. Pep Guardiola - Ana thamani ya €27M

Guardiola ndiye mkufunzi tajiri zaidi England . Josep ''pep'' Guardiola Sala ni raia wa Uhispania na mchezaji wa zamani ambaye ndiye mkufunzi wa sasa wa klabu ya Manchester City.
Ana sifa za kuwa mkufunzi aliyefanikiwa zaidi duniani, Akiwa mchezaji , Pep alihudumia wakati wake mwingi akiifuna Barcelona . Akiwa mkufunzi ,Pepe amejishindia mataji chungu nzima akifunza klabu tofauti.
Guardiola amekuwa akipenda sana mbinu ya tikitaka , ambayo ni mbinu ya Uhispania inayoshirikisha pasi fupi na kusonga mbele.
Baada ya kupata ufainisi mkubwa akiifunza Barcelona na Bayern Munich, Pep Guardiola aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Manchester City 2016.
Raia huyo wa Uhispania kufikia sasa amefanikiwa kujenga kikosi bora cha ligi ya premia katika historia ya timu hiyo.
Anapokea €27M kila mwaka kama meneja wa Manchester City na thamani yake ni kati ya $40-60 m hatua inayomfanya kuwa mkufunzi tajiri zaidi England
2. Antonio Conte - Ana thamani ya €30M

Chanzo cha picha, Getty Images
Antonio Conte
Antonio Conte ni mkufunzi wa Itali na mchezaji wa zamani.
Ndiye kocha mkuu wa InterMilan . akicheza kama kiungo wa kati, Conte alianza kucheza soka katika klabu ya U.S Lecce na baadaye kuwa mchezaji mwenye sifa zaidi katika historia ya klabu ya Juventus.
Antonio Conte alijishindia taji la ligi ya Premia katika msimu wake wa kwanza na wa pekee akiifunza Chelsea. Msimu unaofuatia alifutwa kazi na Chelsea lakini akafanikiwa kisajiliwa na Inter Milan .
Ana sifa za kutumia mbinu ya 3-5-2 katika kipindi chake cha ukufunzi . Aliisaidia InterMilan kufika fainali za kombe la Yuropa katika msimu wake wa kwanza ambapo timu yake ilishindwa na Sevilla katika fainali.
Conte anapokea €30M kila mwaka na thamani yake inadaiwa kuwa kati ya $50-60m
1. Diego Simeone - Ana thamani ya €40.5m

Diego Simeone ndiye mkufunzi tajiri zaidi duniani.
Anapokea €40.5M kila mwaka. Pia ni miongoni mwa wakufunzi wanaopokea fedha nyingi z aidi duniani 2021. Raia huyo wa Argentina amefunza klabu kadhaa lakini amepata ufanisi mkubwa akiifunza Atletico Madrid , kwa kuisaidia kushinda taji la La Liga, Copa del Rey, makombe mawili ya Yuropa, makombe mawili ya UEFA Supercup na kuwa katika nafasi ya pili katika kombe la klabu bingwa Ulaya .
Thamani ya Diego Simeone inadaiwa kuwa $130m kulingana na mtandao wa Celebrity net worth na hivyo kuwa mkufunzi tajiri zaidi duniani.












