Tetesi za soka Ulaya Jumanne 25.06.2019: Tierney, Kovacic, Neymar, Pogba, Sancho, Ceballos

Paris St-Germain wameipatia ofa Man United ya kubadilishana na mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba. (Independent)
Arsenal itahitaji nusu ya fedha zao ilizotengewa dirisha la uhamisho kumnunua beki wa Celtic raia wa Uskochi Kierna Tierney mwenye umri wa miaka 22 huku mchezaji huyo akiwa na thamani ya £25m kutoka kwa mabingwa hao wa Uskochi.. (Telegraph)
Hatma ya kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, 25, katika klabu ya Chelsea haijulikani huku mkopo wake katika klabu ya Real Madrid ukitarajiwa kukamilika tarehe mosi mwezi Julai. Klabu hiyo ya Stamford Bridge bado haijamuongezea kandarasi. (Goal)

Chanzo cha picha, TF-Images
United itaimarisha hamu yao ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho, 19, iwapo watamuuza Pogba. (Sun)
Neymar hatoruhusiwa kurudi katika klabu yake ya zamani Barcelona kutoka PSG hadi atakapoomba msamaha kwa mabingwa hao wa Uhispania na mashabiki wake na kukubali mshahara wake kupunguzwa (El Mundo - in Spanish)
Real Madrid haitakubali maombi ya chini ya 47.7m kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, ambaye amevutia hamu ya klabu ya Tottenham nchini Uingereza. (AS- in Spanish)

Chanzo cha picha, Reuters
Spurs inachunguza kinda wa Denmark Andreas Skov Olsen, ambaye anaichezea klabu ya FC Nordsjaelland na ana thamani ya £15m. (Mirror)
Arsenal wanakataa ofa kutoka AC Milan kumuuza kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, 23. (Mirror)
The Gunners wana hamu ya kumsajili winga wa klabu ya Dalian Yifang Yannick Carrasco, lakini bado hawajawasilisha ofa yoyote kwa mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 25 (Football.London)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi mpya wa Juventus Maurizio Sarri ana hamu ya kumsajili beki wa kulia wa Tottenham Kieran Trippier, 28, kama mchezaji ambaye anamlenga sana lakini anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Napoli ambao tayari wamewasiliana na mchezaji huyo.. (Mirror)
Mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, ambaye alihudumu misimu miwili kwa mkopo akiichezea Bayern Munich, hana uhakika iwapo atasalia katika klabu hiyo ya Bernabeu msimu ujao. (Marca)
Newcastle United haina haja na mshambuliaji wa West Brom na Venezuela Salomon Rondon - ambaye alihudumu msimu uliopita akiichezea klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza - licha ya uamuzi wa mkufunzi Rafael Benitez kuondoka katika klabu hiyo. (Star)

Aston Villa inataka kumnunua beki wa klabu ya Luton Town na Uingereza James Justin huku klabu ya Leicester pia ikiwa na hamu ya mchezaji huyo. (Birmingham Chronicle)
Beki wa klabu ya Manchester United na Uingereza Axel Tuanzebe, 21, ambaye alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa anataka hakikisho kuhusu hatma yake katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Sun)
Mchezaji anayelengwa na Arsenal Dominik Szoboszlai, 18, anafikiria kuondoka katika klabu ya Red Bull Salzburg, huku Barcelona na Borussia Dortmund zikimnyatia mchezaji huyo wa Hungary. (Football.London)
TETESI JUMATATU

Mchezaji wa Leicester City na Uingereza Harry Maguire, 26, anatarajiwa kuwa beki ghali zaidi duniani wiki hii wakati atakapojiunga na Manchester City kwa dau la £80m baada ya kukataa kujiunga na Manchester United. (Mirror)
Liverpool na Manchester United watapigania saini ya mchezaji wa Uhispania na Real Betis beki wa kushoto Junior Firpo, 22. (Marca)
Manchester United watatumia kifungo cha sheria ya kumuongezea miezi 12 Marcus Rashford katika kandarasi yake uku kukiwa na hofu kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 huenda akaondoka man United wakati mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu ujao. (Sun)


Chanzo cha picha, Getty Images
Inter Milan haijaafikia kiwango cha £22.3m kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)
Newcastle United inatarajiwa kufanya majaribio ya mwisho kumrai mkufunzi Rafael Benitez kuongeza kandarasi yake.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 , ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa mwezi Juni ameripotiwa kupata kazi nchini China. (Evening Chronicle)

Real Betis wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi, 24. (Estadio Deportivo, in Spanish)
Klabu ya Brighton imekubali kumsajili winga wa Ubelgiji Leandro Trossard, 24, kutoka Genk kwa dau la £18m. (Sky Sports)
Mchezaji anayelengwa na Liverpool Nicolas Pepe anawaniwa na InterMilan kwa dau la £80m.

Chanzo cha picha, Getty Images
Timu hiyo ya Ligi ya Serie A Inter Milan ni miongoni mwa klabu nyingi zilizo na hamu ya kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Lille na Ivory Coast . (L'Equipe, in French)
Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amewasilisha ombi la kibinafsi kwa afisa mkuu mtendaji -mwenyekiti Ed Woodward kuharakisha ili kumsajili kiungo wa kati wa Lisbon na Portugal Bruno Fernandes , 24, (Record, in Portuguese, subscription required)

Wakati huohuo Manchester United wako katika harakati za kumsaini winga wa Uhispania mwenye umri wa miaka 16 Mateo Mejia kwa dau la £600,000 kutoka klabu ya Real Zaragoza. (Sun)
Arsenal inafikiria kumuuza Lucas Torriera, 23, baada ya AC Milan kuwasilisha ombi lao la kwanza kwa kiungo huyo wa Uruguay. (Sport Mediaset, in Italian)
Mkufunzi wa Leicester Brendan Rodgers ameambiwa kwamba anapoteza wakati kujaribu kumsaini kiungo wa kati wa Uskochi mwenye umri wa miaka 26 Callum McGregor kutoka klabu yake ya zamani Celtic. (Scottish Daily Mail)

Klabu ya Uholanzi ya AZ Alkmaar imethibitisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Southampton Jordy Clasie, 27. (Daily Echo)
Burnley wamemwambia beki Ben Gibson,26, anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu.
Anston Villa ambao wamepanda daraja la ligi ya Premier pamoja na Sheffield United ni miongoni mwa kundi la klabu zilizo na hamu ya kumsaini mchezaji huyo wa Uingereza kwa dau la £15m. (Teamtalk)
Aston Villa wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili beki wa Bournemouth Tyrone Mings,26. Mchezaji huyo wa Uingereza alikuwa kiungo muhimu katika kupandishwa daraja kwa Villa wakati alipoichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita.. (Birmingham Mail)
TETESI ZA SOKA JUMAPILI

Chanzo cha picha, Getty Images
Inter Milan wanataka kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, 26, lakini watalazimika kumuuza mshambuliaji wao wa sasa Muargentina Mauro Icardi,26 kufadhili mkataba wa Lukaku. (Guardian)
Real Madrid wanampango wa kumnunua Paul Pogba kutoka Manchester United msimu huu wa joto kabla ya kumsaini mchezaji nyota wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Goal)
Tottenham watamchukua winga wa Uhispania wa miaka 22 Marco Asensio kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa Eriksen kwenda Madrid . (Sun)
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu hiyo imuuza Pogba kwa klabu itakayoweka dau kubwa zaidi, japo Juventus wameonesha nia ya kutaka kumnunua. (Star)

Chanzo cha picha, Reuters
Tottenham inatarajia Juventus itaweka dau la kumnunua beki wa kulia Kieran Trippier, 28, na wako tayari kumuuza kiungo huyo wa kimataifa kwa karibupauni milioni 25. (Telegraph)
Paris St-Germain wameiambia Barcelona kuwa hawamuuzi Neymar, 27 kwa udi na uvumba. (Mail)
Real Madrid wanampango wa kusaini Ian Kylian Mbappe,26 kutoka PSG msimu ujao lakini wanataka mchezaji huyo raia wa Ufaransa kutoa ombi la kutaka uhamisho. (AS)

Chanzo cha picha, Reuters
Atletico Madrid wanamtaka beki wa Arsenal Mhispania Hector Bellerin, 24, na wako tayari kumwachilia winga Vitolo, 29, kama sehemu ya mkataba wa usajili wake. (Telegraph)
Chelsea hawajaamua kumuuza mlinzi wao Mfaransa Kurt Zouma, 24, kwa Everton hadi watakapopata kocha mpya. (Star)
The Blues wanajiandaa kuilipa Derby pauni milioni 4 zinazohitajika kutimiza masharti ya mkataba wa Frank Lampard kabla hawajakamilisha mchakato wa kumuajiri kama kocha wao mpya wiki ijayo. (ESPN)
Chelsea wamempatia kipa Petr Cech la kiufundi na mshauri wa michezo wakiwa na matumaini kuwa atashirikiana kwa karibu na Lampard. (Guardian)

Chanzo cha picha, AFP
Klabu ya Shanghai Greenland Shenhua kutoka China imetoa ofa ya pauni milioni 17.8 kumnunua Willian, 30, lakini mchezaji huyo wa Brazil huenda asikubali kujiunga nao kwasababu bado anataka kusalia Chelsea. (UOL Esporte, via Metro)
Mpango wa Arsenal wa kumnunua winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco au mshambuliaji wa Bournemouth Ryan na Uskochi Fraser huenda umekwama. (Evening Standard)
Meneja mpya wa Juventus Maurizio Sarri amesema hana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 27, kutoka Chelsea. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Tetesi Bora Ijumaa
Juhudi za kocha Ole Gunnar Solskjaer kuimarisha kikosi chake huenda zikagonga mwamba kwa sababu Manchester United ni klabu ambayo hutoa ofa ya chini kwa wachezaji wanaotaka kuwasajili. (Evening Standard)
Solskjaer anataka kumuuza kiungo wa kati wa Man Utd Mfaransa Paul Pogba, 26, bada ya kufahamishwa kuwa ana pauni milioni 100 ya kuwasajili wachezaji wapya msimu huu. (Star)

Chanzo cha picha, Reuters
Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, hana mpango wa kuchezea tena Paris St-Germain. (Sport - in Spanish)
Real Madrid wameweka dau la euro milioni 130 kumnunua Neymar, kutoka PSG, mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, au mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester City wanapigiwa upatu kuipiku Man Utd katika usajili wa Harry Maguire, 26, kutoka Leicester kwa kima cha pauni milioni 65 baada ya kiungo huyo wa England kupita vipimo vya matibabu. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Mhispania Rodri, ameamua kujiunga na Man City badala ya Bayern Munich na kuhamia City kawa malipo ua £62m. (Kicker - in German)
Everton wameanza maungumzo na Chelsea kuhusu usajili wa Kurt Zouma kwa mkataba wa kudumu baada ya mlinzi huyo wa Ufaransa, 24, kucheza Goodison Park msimu uliopita kwa mkopo katika. (Telegraph)












