AFCON 2019: Wenyeji Misri waichapa Zimbabwe 1-0

Mahmoud Trezeguet

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Trezeguet afunga bao lake la tano la Kimataifa na kuipatia Misri Ushindi katika mechi ta ufunguzi

Wenyeji wa michuano ya kombe la taifa bigwa Afrika Misri waeanza kampeini yao ya kuwania taji hili maarufu la soka Afrika kwa kuilaza Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa mjiniCairo.

Mahmoud Trezeguet alifunga bao la kipekee la mchezo huo kabla ya muda wa mapumziko..

Mashambuliaji wa Liverpool Mo Salah alikaribia kutia kimyani bao la pili katika kipindi cha pili lakini kipa wa Zimbabwe Edmore Sibanda hakumpatia nafasi.

Ovidy Karuru aliipotezea Zimbabwe nafasi nzuri ya kusawazisha bao hilo la Misri katika mashambulizi ya dakika za mwisho.

Mashindano ya mwaka huu ya Afcon ambayo inajumuisha timu 24 ndio makubwa zaidi kuchezwa msimu wa joto wa Ulaya.

Sherehe ya ufunguzi wa mashindano hayo zilisheheni mbewe mbwe za kila aina huku mashabiki 75,000 waliojitokeza kushangilia timu yao ya nyumbani katika uwanja wa Kimataifa Cairo.

Lakini mchezo wenyewe haukufikia kiwango cha msisimko wa sherehe ya kuvutia ya ufunguzi baada ya Misri kutawala mchezo huo bila kumfikia kipa Sibanda wa Zimbabwe kama ilivyotarajiwa.

Mo Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki Mo Salah waalijitokeza kumshangilia

Salah aliongeza nakshi mchezo huo kwa kufanya mashambulizi mara kadhaa katika kipindi cha kwanza japo hakupata fursa ya kutia kimya hata bao moja kwani kipa Sibanda kadhaa alikuwa macho.

Zimbabwe waliaanza kufurahia mkondo wa mchezo kwa wakati mchache kabla ya Misri kuchukua uongozi katika kipindi cha kwanza.

Ushirilkiano mzuri wa Trezeguet na wachezaji wenzake uliiwezesha Misri kufika karibu na lango la Zimbabwe lakini washabuliaji wa Misri walivyoshindwa kupenya ngome ya wapinzani wao wakalazimisha kona.

Kuanzia hapo Misri ilitulia na kupunguza kasi ya mashambulizi hali ambayo ilikosesha mchezo huo mahanjam.

Salah aliongeza juhudi na kuonesha umahiri wake lakini lakini usiku huo haukua wake kwani Kipa Sibanda hakumruhusu kutoka na pasi za mlinzi Trezeguet ambazo hazikumfikia kama alivyotarajia.

Nyota huyo anaechezea klabu ya Liverpool aling'ang'ana kupata bao lakini juhudi zake zilizimwa na kipa wa ziada wa Zimbabwe, Elvis Chipezeze, ambaye aliingia uwanjani baada ya Sibanda kujeruhiwa dakika 10 za mwisho wa mchezo huoo.

Ushindi huo wa Misri umeiweka katika nafasi ya kwanza ya kundi A, ambayo pia inajumuisha DR Congo na Uganda. ambao watamenyana leo Jumamosikatika uwanja wa Cairo.

Msiri wanastahili kuimarisha mchezo wao -Uchambuzi

Mwandishi wa BBC Mohamed Qoutb

Misrihuenda walifunga bao mapema lakini baada ya hapo walituliza kasi ya mchezo hali ambayo ilishukisha chini morali ya mashabiki kwa wachezaji wake.

Hata baada yaTrezeguet kufunga bao, ushndi huo haukiimarisha utendakazi wa timu hiyo kama ilivyotarajiwa katika kipindi cha pili.

Timu hiyo pia haikuwa na haraka ya mchezo hali ambayo ingeliwapatia bao Zimbabwee laiti wangeliongeza juhudi.

Afcon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Shere ya ufunguzi wa Afcon ilikuwa ya kuvutia
Afcon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Misri wanaandao mishuano hiyo kwa mara ya tano.
Afcon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kombe linalofanana na lile linaloshindaniwa katika mashindano hayo lilizinduliwa katia sherehe ya Ufunguzi.