Samwel Kalu azimia uwanjani kwa kukosa maji mwilini

Muda wa kusoma: Dakika 1

Samwel Kalu alianguka alipokuwa akifanya mazoezi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Samwel Kalu alianguka alipokuwa akifanya mazoezi

Mshambuliaji wa timu ya Nigeria Samuel Kalu amepelekwa hospitalini wakati timu yake ikijiandaa kucheza mchezoo wa kwanza katika michuano ya kuwania kombe la mataifa barani Afrika baada ''kukosa maji mwilini''

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21, anayecherzea timu ya Ufaransa ya Bordeaux, alianguka alipokuwa mazoezini Ijumaa.

Nigeria inacheza na Burundi mjini Alexandria Jumamosi, huku joto lilitarajiwa kupanda hadi kiwango cha nyuzi joto 40.

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) linapanga kuwa na vipindi viwili vya mapumziko ya kunywa maji ili kushusha joto la mwili kulingana na sheria za Fifa.

Kalu mwenye umri wa miaka 21, pia anachezea timu ya Ufaransa ya Bordeaux

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kalu mwenye umri wa miaka 21, pia anachezea timu ya Ufaransa ya Bordeaux

Mwandishi wa BBC wa masuala ya Soka Oluwashina Okeleji anasema Kalu alizimia alipokuwa akijiandaa kupiga mpira wa kona katika mazoezi na hivyo kusababisha mchezo huo kucheleweshwa kwa dakika takriban 25.

Msemaji wa timu ya Nigeria Toyin Ibitoyeamesema kuwa Kalu yuko katika hali "thabiti " baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali na hataweza kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Misri.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe