Samwel Kalu azimia uwanjani kwa kukosa maji mwilini

Muda wa kusoma: Dakika 1

Mshambuliaji wa timu ya Nigeria Samuel Kalu amepelekwa hospitalini wakati timu yake ikijiandaa kucheza mchezoo wa kwanza katika michuano ya kuwania kombe la mataifa barani Afrika baada ''kukosa maji mwilini''

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21, anayecherzea timu ya Ufaransa ya Bordeaux, alianguka alipokuwa mazoezini Ijumaa.

Nigeria inacheza na Burundi mjini Alexandria Jumamosi, huku joto lilitarajiwa kupanda hadi kiwango cha nyuzi joto 40.

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) linapanga kuwa na vipindi viwili vya mapumziko ya kunywa maji ili kushusha joto la mwili kulingana na sheria za Fifa.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya Soka Oluwashina Okeleji anasema Kalu alizimia alipokuwa akijiandaa kupiga mpira wa kona katika mazoezi na hivyo kusababisha mchezo huo kucheleweshwa kwa dakika takriban 25.

Msemaji wa timu ya Nigeria Toyin Ibitoyeamesema kuwa Kalu yuko katika hali "thabiti " baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali na hataweza kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Misri.