Wachezaji 5 wa Afrika wanaoweza kujiunga na Primia Ligi baada ya AFCON 2019

Ziyech aling'ara sana kimchezo akiwa na klabu ya Ajax Amsterdam

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ziyech aling'ara sana kimchezo akiwa na klabu ya Ajax Amsterdam
Muda wa kusoma: Dakika 3

Tayari mashindano ya 32 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON2019) yameng'oa nanga nchini Misri, yakitarajiwa kufichua zaidi vipaji vya vijana wa kiafrika katika soka.

Huku wengi wakiwa wanayafahamu majina ya wachezaji wa Primia Ligi kama vile Mohamed Salah, Sadio Mane, Victor Wanyama, Riyad Mahrez, Alex Iwobi na John Obi Mikel yanayojitokeza katika kinyang'anyiro hiki cha Afrika , kuna wale ambao wako nje ya Ligi hiyo ya England ambao hata hivyo wamefanbya vema katika Ligi zao.

Kwa hivyo basi wataraka kutumia mechi za kombe la AFCON kama mahala pa kuonyesha umahiri wao wa kimcheza na kujinadi zaidi kwa ajili ya soko la nje la soka.

Wachezaji watano wanaoweza kuhamia Primia Ligi baada ya AFCON msimu huu:

1. Hakim Ziyech

Ziyech ambaye ni raia wa Morocco aling'ara sana kimchezo akiwa na Ajax Amsterdam msimu uliopita, akichangia mabao 29 goals 29 katika mechi za ligi ambapo timu hiyo ya Uholanzi ilishinda taji la ligi ya nchi hiyo.

Tayari amekwishazivutia timu za Ualya, huku Arsenal, Manchester United na hata Real Madrid wakitajwa kumtaka sana. Hata hivyo anaweza kuongeza mvuto zaidi wa soko lake atakapowaongoza Atlas Lions katika mezi za kundi lao ambapo wamewekwa na Namibia, Afrika Kusini na Ivory Coast. kwenye ukurasa wa Tweeter wataalam wa Soka Ulaya wamekuwa wakimjadili:

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Mbwana Samatta amecheza misimu minne katika timu ya daraja la kwanza nchini Ubelgiji, lakini mchezo wake wa 2018/19 unadaiwa kuwa bora zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwana Samatta amecheza misimu minne katika timu ya daraja la kwanza nchini Ubelgiji, lakini mchezo wake wa 2018/19 unadaiwa kuwa bora zaidi

2. Mbwana Samatta

Akiwa mchezaji wa safu ya mashambulizi Mbwana Samatta ni Mchezaji mahiri wa Tanzania ambao mashabiki wengi wa soka huenda wasimfahamu. Lakini kwa Wabelgiji kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 ni jina maarufu sana.

Amecheza misimu minne katika timu ya daraja la kwanza nchini Ubelgiji, lakini mchezo wake wa 2018/19 unadaiwa kuwa bora zaidi. Mshambuliaji huyo amesifiwa kwa mafanikio ya timu ya Genk , ambapo alitikisa nyavu mara 32 katika mechi 53 katika mashindano yote.

T

Gazeti la SunSport limeripoti kuwa Marega tayari analengwa na Wolves pamoja na Chelsea

Chanzo cha picha, Moussa Marega/tweeter

Maelezo ya picha, Gazeti la SunSport limeripoti kuwa Marega tayari analengwa na Wolves pamoja na Chelsea

Taarifa ya azama ya Liverpool ya kumnunua Moussa marega imekuwa ikielezewa pia kwenye mitandao ya kijamii:

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

3. Moussa Marega

Moussa Marega ni Mshambuliaji hatari wa Mali ambaye kusema ukweli hahitaji maelezo zaidi hasa kwa wale waliotazama michuano ya Championi Ligi msimu huu.

Mshambuliaji wa FC Porto amekuwa na msimu mzuri na timu hiyo kubwa ya Ureno akifanikiwa kutikisa nyavu mara 17 tkatika mashindano yote.

Gazeti la SunSport limeripoti kuwa Marega tayari analengwa na Wolves pamoja na Chelsea.

4. Andre Onana

Manchester United o tayari imeonyesha haja kubwa ya kusaini mkataba na Andre Onana na huenda akachukua nafasi ya David De Gea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester United o tayari imeonyesha haja kubwa ya kusaini mkataba na Andre Onana na huenda akachukua nafasi ya David De Gea

Mcheza huyu mchanga mfupi wa kimo kutoka taifa la Cameroon amejitengenezea jina akiwa katika klabu ya Ajax Amsterdam msimu huu. Kwa kiasi kikubwa amesifiwa kwa mafanikio aliyoyapata katika klabu hiyo msimu huu, ambapo aliisaidia kufiukia nusu fainali katika Championi Ligi.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Manchester United ndio timu kuu ambayo tayari imeonyesha haja kubwa ya kusaini mkataba na Andre Onana na huenda akachukua nafasi ya David De Gea.

5. Nicolas Pepe

Nicolas Pepe anamezewa mate na timu za England

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nicolas Pepe anamezewa mate na timu za England

Pepe kutoka nchini Ivory Coast anajulikana sana kwa kasi isiyo ya kawaida uwanjani na ujuzi wake kusakata mpira, ikiwa ndio sababu anapendwa Ulaya. Aling'ara katika timu ya Lille ya daraja la kwanza nchini Ufaransa msimu huu ambako alifunga mabao 22 katika msimu huu wa Ligi na akafunga mabao 11 katika michezo mingine 37 aliyocheza.

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 4

Timu za Ligi ya England Manchester City, Arsenal na Liverpool wanamezea mate huduma zake uwanjani. Imebaki tu kuona ikiwa atasaini mkataba wa kuhamia katika EPL msimu huu.