AFCON 2019: Tanzania na Kenya zalazwa na Senegal na Algeria

Keita Balde akishangilia

Chanzo cha picha, CAF

Maelezo ya picha, Keita Balde alikuwa mwiba mchungu kwa Taifa Stars
Muda wa kusoma: Dakika 3

Kiuhalisia, ni matokeo ambayo hayashangazi.

Japo Watanzania walikua wakiomba dua njema za kupata ushindi wa kwanza katika historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), mioyoni mwao walikuwa wakijua fika kuwa mlima ulipo mbele yao ni mrefu kuupanda.

Senegal, ama Simba wa Teranga wamewalaza Tanzania maarufu kama Taifa Stars goli 2-0 katika mchezo wa kufungua dimba katika kundi C.

Simba hao waliuanza mchezo kwa kasi, huku washambuliaji wao wakilisakama lango la Stars, na ndani ya dakika 10 za mwanzo wakawa wameshapoteza nafasi za wazi karibia tatu.

Wakati huohuo winga wa klabu ya Manchester City Riyad Mahrez alifunga goli moja huku Algeria ikipanda sawa na Senegal katika kundi C Kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuilaza Kenya 2-0.

Baghdad Bounedjah alifunga goli la mkwaju wa penalti kunako dakika 34 mjini Cairo baada ya Youcef Atal kuangushwa katika lango la Harambee Stars.

Mahrez baadaye akafunga goli la pili kupitia mkwaju uliomgusa beki wa Kenya na kuingia wavuni dakika mbili kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Algeria inajiunga na Senegal ikiwa na pointi tatu , baada ya kikosi cha Aliou Cisse kuilanza Tanzania 2-0 hapo awali.

Algeria wakifunga goli la penalti dhidi ya Kenya

Chanzo cha picha, Caf/Twitter

Algeria itajaribu kushinda michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu 1990, walihitaji kushinda mechi hiyo dhidi ya Kenya ambayo ilikuwa inarudi katika michuano hiyo tangu ishiriki mara ya kwanza 2004.

Baghdad Bounedjah karibia afunge bao jingine huku Algeria ikitawala mchezo katika muda mrefu wa kipindi cha kwanza huku Youcef Belaili akipiga shambulio kali lilioenda katika mikono ya kipa wa Kenya Patrick Matasi alipopata pasi nzuri kutoka kwa Sofiane Feghouli.

Kenya ikiongozwa na kiungo wa kati wa Tottenham Victor Wanyama waliimarika kimchezo katika kipindi cha pili huku mshambulaiji Michael Olunga akishinda kufunga dakika za lala salama.

Algeria sasa itakabiliana na Senegal huku kenya ikichuana ana Tanzania baadaye siku hiyo.

Kipa wa Taifa Stars, Aishi Manula aliokoa michomo kadhaa ambayo ingeweza kuleta madhara kwenye lango la Tanzania.

Iliwachukua dakika 28 kwa Senegal kutangulia kwa kupata goli la kuongoza kwa shuti la karibu la mshambuliaji Keita Balde.

Balde ambaye anachezea miamba ya soka nchini Italia, klabu ya Inter Milan aliendelea kuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Stars kwa kosa kosa zake.

Baada ya hali kuzidi kuwa ngumu, kocha wa Tanzania Mnigeria Emmanuel Amunike alilazimika kumtoa Feisal Salum katika dakika ya 43 na nafasi yake kuchukuliwa na Farid Mussa.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika, Senegal ilikuwa imemiliki mchezo kwa asilimia 61, na kupiga mashuti 13 langoni mwa Tanzania.

Tanzania ilikuwa imemiliki mchezo kwa asilimia 39, na kuambulia mashuti mawili kwenye lango la Senegal.

Kipindi cha pili kikaanza kaama ilivyokuwa kwa kipindi cha kwanza kwa Senegal kushambulia kwa nguvu langoni mwa Tanzania.

Krepin Diatta aliachia shuti kali katika dakika ya 65 amabalo kipa wa Tanzania Manula lilimshinda kulizuia na kulisindikiza kwa macho mpaka nyavuni.

Na huo ndio ukawa msumari wa mwisho kwenye jeneza la Tanzania.

Diatta

Chanzo cha picha, CAF

Maelezo ya picha, Krepin Diatta ameibuka mchezaji bora wa mechi ya Senegal vs Taifa Stars.

Umiliki wa mpira baada ya dakika 90 ulisalia kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza, Senegal 61% na Tanzania 39%.

Hata hivyo kwenye mashuti langoni, Senegal wamepiga michomo 23, kati ka hiyo 13 ikilenga lango.

Tanzania imepiga mashuti 3 na yote hayakulenga goli.

Ni dhahiri kuwa Senegal ambayo ilimkosa mshambuliaji wake tegemezi na nahodha Sadio Mane ingeweza kushinda kwa magoli mengi zaidi.

Samatta

Chanzo cha picha, CAF

Maelezo ya picha, Safu ya ulinzi ya Senegal ilimficha vilivyo Samatta

Baadhi ya mashabiki wa kandanda wameoneka na kuelekeza lawama zao kwa kocha Amunike.

Bado hasira za kuachwa kwa viungo nyota Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu angali zimo kwenye fikra za wengi.

Mshambuliaji na nahodha wa Stars Mbwana Samatta alikabwa vilivyo kwenye mchezo huo na safu ya ulinzi ya Senegal inayoongozwa na Khalidou Kulibally.