Red Star Belgrade 2-0 Liverpool: Liverpool wapata kipigo wasichotarajia

Red Star Belgrade fans celebrate scoring against Liverpool

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfunganji wa Red Star Belgrade goalscorer Milan Pavkov

Meneja Jurgen Klopp anasema Liverpool walikuwa na wakati mgumu kucheza kwa kuwa mabao mawili ya mapema kutoka kwa Milan Pavkov yaliwapa Red Star Belgrade ushindi wa usiotarajiwa.

Ushindi ungewapeleka Liverpool pointi tatu mbele katika kundi la C lakini sasa wameteremka hadi nafasi ya pili kifuatia droo kati ya Napoli na PSG nchini Italia.

Mshambuliaji Pavkov aliongoza kikosi chake kufunga bao la kwanza baada ya dakika ya 21 na la pili kufikisha mabao 2-0 baadaye.

Daniel Sturridge wa Liverpool alitupa nafasi safi dakika ya 17.

Upande wa Klopp ulidhibiti mpira kwa zaidi ya asilimia 80 lalini Red Star walipata ushindi wao wa kumi kwenye mechi 15 ambazo wamecheza nyumbani.

Hatari ya kufuzu

Mohamed Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohamed Salah

Liverpool walikosa kasi yao huko Serbia na wakaadhibiwa kwa hilo.

Mechi kali iliyotoka droo dhidi ya Arsenal wikendi iliyopita ilionekana kukilemea kikosi cha Jurgen Klopp kwa sababu ilikichukua muda kudhibiti kikosi cha Arsenal.

Liverpool waliweza kujimarisha katika kipindi cha pili na Salah akakaribia lango mara kadhaa lakini Red Star ilizuzia kabisa jitihada zake.

Champions League group C

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Liverpool wako pointi sawa na Napoli

Meneja wa Red Star Belgrade akiongea mapema, alizungumzia jinsi mechi hiyo ilikuwa yenye amuhimu kwao kabala ya kuanza kwa mechi na alikuwa na matumaini kuwa kucheza kwao nyumbani kungekuwa kwa manufaa kwao.

'Lazima tukabiliane na hili'

Jurgen Klopp: Vijana wamekasirika sana, mimi pia nimekasirika sana ni lazima tufanye vizuri. Tutahitaji kufanya vizuri kwa kuwa tunweza kufanya vizuri lakini leo hii tumechelewa sana.

Walikuwa katika hali nzuri na tulihitaji kukabiliana nayo, Sio kiytu tulikuwa tunakitaka na tutaziendea mechi zingine mbili kwa asoilimia 100. Lazima tukabiliane nayo sasa.

Mambo makuu

  • Liverpool imepoteza mechi tatu za Ligi ya Mabingwa mara tatu mfululizo kwa mara ya kwanza.
  • Pavkov alikuwa mchezaji wa kwanza raia wa Serbia kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa tangu Aleksandar Prijovic wa Legia Warsaw afunge dhidi ya Borussia Dortmund Novemba 2016.
  • Red Star Belgrade wameshinda mechi zao zote za nyumbani dhidi ya Liverpool.
  • Liverpool wamepotza mechi zao mbili kati ya tatu za mwisho za makundi za Champions League.

Mchezaji bora wa mechi - Milan Pavkov (Red Star Belgrade)

Milan Pavkov

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Milan Pavkov alifunga mabao yote ya Red Star

Kipi kinafuatia?

Liverpool itawaalika Fulham katika Premier League siku ya Jumapili lakini kabla ya mechi ya Champions League dhidi ya Paris St-Germain tarehe 28 Novemba.