Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 26.10.2018: De Gea, Sanchez, Martial, Gundogan, Young, Cahill, Lambert, Pope

David De Gea 27

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Golikipa wa Manchester United, David De Gea 27

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anahofia kumpoteza golikipa wake kutoka Spain David De Gea 27 ambaye anaweza kuhamia Juventus, wakati ambapo mkataba wake utaisha msimu ujao wa kiangazi. (Irish Sun)

Mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 29,yoko tayari kuondoka Manchester United mwezi januari na amejipanga kuhamia Paris St-Germain. (Mirror)

Mshambuliaji wa ufaransa Anthony Martial, 22, amekaukataa mkataba mpya ambao amepewa na timu ya Manchester United lakini mazungumzo ya makubaliano yanaendelea.

Kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 28,ambaye Ajax inamuwania, yuko tayari kuwa na timu ya Manchester City kwa muda mrefu kwa siku za usoni na kusaini mkataba mpya. (Sun)

Ashley

Chanzo cha picha, Getty Images

Mchezaji wa Manchester United Ashley Young, 33, anataka mkataba mpya wa miaka miwili na timu yake. (Mirror)

Beki wa Kati wa Chelsea Gary Cahill, 32,amekubali kubaki katika timu yake licha ya kuwa kabla alisema anaweza kuondoka mwezi Januari. (Sun)

Mchezaji wa Chelsea kutoka Nigeria Victor Moses, 27

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mchezaji wa Chelsea kutoka Nigeria Victor Moses, 27

Mchezaji wa Chelsea kutoka Nigeria Victor Moses, 27 anaona kuwa hapo baadae atakosa muda wa kutosha wa kucheza. (Evening Standard)

Ipswich Town anamuona kuwa Paul Lambert ndiye atakuwa meneja wao baada ya kufukuzwa kwa Paul Hurst. (Independent)

Tottenham inavutiwa na golikipa wa Burnley na England Nick Pope, 26. (Mirror)

Crystal Palace itamrudisha meneja Roy Hodgson mwezi Januari katika dirisha la uhamisho ya orodha ya wafungaji ambayo alikuwa anaiwania.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez
Maelezo ya picha, Rais wa Real Madrid Florentino Perez

Rais wa Real Madrid Florentino Perez anataka kumfukuza meneja wa timu Julen Lopetegui baada ya mashindano dhidi ya Viktoria Plzen siku ya jumanne lakini alishawishika kusubiri mpaka baada ya mechi ya mwisho wa juma na El Clasico. (Sport )

Bosi wa zamani wa Chelsea Antonio Conte hakuwa katika mkataba na Real Madrid, kwa mujibu wa kaka yake. (Cadena SER )

Kocha msaidizi wa Harvard amesema kuwa anaikaribisha walinzi wa kati wa Juventus Giorgio Chiellini na Leonardo Bonucci baada ya bosi wa Manchester United Jose Mourinho kudai kuwa wawili hao wataenda chuo Marekani kupata mafunzo ya kuwa walinzi wa kati. (TuttoJuve)