Waendesha baiskeli kutoka Algeria wanawiri mashindano ya Tour du Rwanda.

Waendeshabaskeli kutoka Algeria wamenawiri mnamo mwanzo wa mashindano ya baiskeli ya Tour du Rwanda.
Amekuwa Lagab Azzedine aliyenyakua mbio za awamu ya kwanza jumapili hii za kuzunguka umbali wa kilomita 97 katika mji wa Rwamagana mashariki mwa Rwanda.

Lagab wa timu ya GSPA ya Algeria ametimka mbio hizo kwa muda was aa 2 dakika 12 na sekunde 21 na kuacha nyuma yake kwa sekunde 9 kundi la waendeshabaiskeli wengi wakiwemo Mnyarwanda Valens Ndayisenga ambaye ameishanyakua mashindano hayo mara mbili.
Mashindano ya mwaka huu yanashirikisha timu 16 kutoka sehemu mbali mbali duniani,Afrika ,ulaya na Marekani jumla ya waendeshabaiskeli 80 wakiwa wanashiriki.

Ukanda wa afrika mashariki zinashiriki timu za Rwanda,Kenya na Ethiopia.
Ushindani mkubwa unatarajiwa baina ya waendeshabaiskeli kutoka Rwanda na timu ya Algeria baada ya Eritrea ya kwanza Afrika kushindwa kushiriki mbio hizo kutokana na ukosefu wa fedha.
Kesho mbio zitaelekea kusini mwa Rwanda katika mji wa Huye ,umbali wa kilomita 120.

Mashindano haya ni ya ngazi inayofahamika kama 2.2 ambayo ni ngazi ya pili barani afrika kwa viwango vya shirikisho la mbio za baiskeli ulimwenguni UCI lakini ni ya mwisho kuandaliwa na Rwanda kwani mwaka kesho mbio za Tour du Rwanda zitapandishwa ngazi na kuwa katika ngazi ya kwanza ya 2.1, ambayo ndiyo kubwa zaidi barani afrika.
Hii ina maana kwamba hata zawadi za pesa zinazotolewa kwa washindi zitaongezeka mara dufu na kuvutia waendeshaji baiskeli maarufu duniani.












