McGregor atamba kumtwanga Mayweather mzunguko wa nne

Mayweather anatajwa kuwa miongoni mwa wanamichezo wenye mvuto mkubwa duniani
Maelezo ya picha, Mayweather anatajwa kuwa miongoni mwa wanamichezo wenye mvuto mkubwa duniani

Bondia Conor McGregor ameahidi kumtangwa Floyd Mayweather ndani ya Round nne wawili hao walipokutana katika kulizungumzia pambano lao la Agosti 26.

Wametokea mbele ya maelfu yamashabiki wao katika mkutano na waandishi wa habari mjini Los Angeles.

McGregor amesema anashangaa nini kilifanya wapiganaji wengine wakashindwa kumtwanga Mayweather

Chanzo cha picha, Reauters

Maelezo ya picha, McGregor amesema anashangaa nini kilifanya wapiganaji wengine wakashindwa kumtwanga Mayweather

''Upinzani atakaoupata kutoka kwangu hajawahi kuupata kamwe'', alisema McGregor, 28.

Mayweather akajibu ''Nakuhakikishia nitaharibu uso wako''.

McGregor na Mayweather wakitambiana
Maelezo ya picha, McGregor na Mayweather wakitambiana

Mpambano huo unatajwa kuwa miongoni mwa itakayovutia zaidi duniani.