Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
McGregor atamba kumtwanga Mayweather mzunguko wa nne
Bondia Conor McGregor ameahidi kumtangwa Floyd Mayweather ndani ya Round nne wawili hao walipokutana katika kulizungumzia pambano lao la Agosti 26.
Wametokea mbele ya maelfu yamashabiki wao katika mkutano na waandishi wa habari mjini Los Angeles.
''Upinzani atakaoupata kutoka kwangu hajawahi kuupata kamwe'', alisema McGregor, 28.
Mayweather akajibu ''Nakuhakikishia nitaharibu uso wako''.
Mpambano huo unatajwa kuwa miongoni mwa itakayovutia zaidi duniani.