Shabiki wa Sunderland Bradley Lowery aliyegusa nyoyo za wengi afariki

Bradley Lowery

Chanzo cha picha, PA

Shabiki wa klabu ya Sunderland wa umri wa miaka sita Bradley Lowery, ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za wengi amefariki dunia.

Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao kwa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.

Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.

Bradley alisherehekea siku yake ya kuzaliwa Mei akiwa na Jermain Defoe na Vito Mannone

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Bradley alisherehekea siku yake ya kuzaliwa Mei akiwa na Jermain Defoe na Vito Mannone

Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.

Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya kijamii.

"Mvulana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo.

"Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake."

Gemma

Chanzo cha picha, Owen Humphreys

Maelezo ya picha, Mamake Bradley Gemma Lowery alikuwa awalia mesema mvulana huyo alikuwa amedhoofika sana

Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana.

Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na hangeweza kutibiwa.

Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".

Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.

Bradley Lowery

Chanzo cha picha, Picha ya Familia

Maelezo ya picha, Bradley alitawazwa Mtoto wa Ujasiri katika tuzo za Fahari ya Kaskazini Mashariki
Bradley Lowery

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Bradley aliipenda sana Sunderland AFC na alikaribishwa uwanjani Stadium of Light
Bradley Lowery

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Mkusanyiko wa picha za Bradley zilizotolewa wakati wa sherehe za siku ya sita ya kuzaliwa ya Bradley mwezi Mei mwaka huu
Sunderland fans held up a banner of support for Bradley

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mashabiki wa Sunderland walikuwa na bango kubwa uwanjani la kumuunga mkono Bradley wakati wa mechi yao dhidi ya Swansea mwezi Mei
Bradley Lowery

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Bradley alitembea kwenye zulia jekundu wakati wa hafla ya Tuzo za Mchezaji Mashuhuri wa Mwaka wa BBC 2016
Bradley

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bradley na babake Carl mechi kati ya Everton na Sunderland

Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi mwaka jana, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.

Bradley Lowery and Jermain Defoe

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Bradley aliunda urafiki na Jermain Defoe