DRC na AFC/M23: Tunayoyafahamu kuhusu mkataba wa amani uliosainiwa Qatar

Wawakilisi wa Serikali ya DRC imetia saini mkataba wa makubaliano na wawakilishi wa kundi la waasi wa AFC/M23 katika hafla iliyoandaliwa jijini Doha chini ya usimamizi wa uongozi wa Qatar.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi na Laillah Mohammed

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho.

  2. Habari za hivi punde, Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi akamatwa

    Taarifa zinazotufikia hivi punde zinasema Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi amekamatwa muda mfupi uliopita.

    Taarifa ya kukamatwa kwake imethibitishwa na Mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu, Vocal Africa Hussein Khalid ambaye ameiambia BBC kuwa mwanaharakati huyo wa haki za binadamu ''amekamatwa jioni hii ya Jumamosi Julai 19''.

    Kulingana picha za video ambazo zimechapishwa na mke wake Njeri kwenye mtandao wa kijamii wa X, watu ambao amewataja kama maafisa wa polisi wanapekua makazi yao ya “Courage Base” yaliyopo katika kaunti ya Machakos nchini Kenya wa ajili ya kutafuta na kubeba Ushahidi ambao Njeri anautaja kuhusiana na tuhuma dhidi ya Mwangi ili kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na kuchoma mali ya umma kwa kukusudia.

    “Wamechukuwa simu na tarakilishi zake zote wakisema kwamba wanamepeleka katika makao makuu ya idara ya uchunguzi wa jinai, DCI. Ninashindwa kupumuwa” aliandika Njeri.

    g

    Chanzo cha picha, Njeri/X

    Boniface Mwangi alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa nchini Tanzania mwezi uliopita, pamoja na mwanaharakati wa Uganda Agather Atuhaire.

    Wawili hao wakisimulia madhila mikononi mwa polisi nchini Tanzania, hali ambayo serikali ya Tanzania imekanusha.

    Tayari wamewasilisha kesi dhidi ya Tanzania kwenye mahakama ya haki kule Arusha siku ya Ijumaa.

    Serikali ya Kenya imeripoti wiki iliyopita kwamba watu 1500 wamekamatwa kwa tuhuma mbali mbali za uhaini, ugaidi, kuchoma mali kwa kukusudia, ubakaji na dhuluma za kingono miongoni mwa mashtaka mengine mengi.

    Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen katika kikao cha wanahabari siku ya Jumatano alisema kwamba serikali inawafuatilia waliofadhili, na kuwachochea vijana kuvamia na kuchoma taasisi za kiserikai kama vile kuvamia vituo vya polisi, mahakama na ofisi za usimamizi wa kaunti katika maandamano ya Juni 25 na Julai 7.

    Rais William Ruto ametaja pia kwamba hatokubali yeyote kujaribu kupanga na kuwatumia vijana kutekeleza alichokitaja kama njama ya kupindua serikali yake, huku akisema kwamba kamwe hatokubali serikali na raia kupata hasara kupitia mali yao kuchomwa.

    Unaweza pia kusoma:

  3. Habari za hivi punde, DRC na AFC/M23: Tunayoyafahamu kuhusu mkataba wa amani uliosainiwa Qatar

    g
    Maelezo ya picha, Kiongozi wa AFC/M23 Corneille Nangaa (kushoto), na Rais wa DRC Felix Tschisekedi

    Serikali ya DRC imetia saini mkataba wa makubaliano na kundi la waasi wa AFC/M23 katika hafla iliyoandaliwa jijini Doha chini ya usimamizi wa uongozi wa Qatar.

    Tangazo hilo la azimio la kurejesha amani mashariki mwa DRC lilitolewa muda mfupi uliopita na unatoa maelekezo kuhusu mchakato wa kufanya mazungumzo zaidi ya kuleta amani.

    Haya ni ndio yaliyoafikiwa na pande mbili:

    • Pande hizo zimetambuwa kwamba amani ni msingi muhimu wa kujenga taifa lililo na umoja na thabiti kwa manufaa ya raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Aidha wamekubaliana kushirikiana na kujihusisha pakubwa kwenye juhudi za jamii ya kimataifa kuwalinda rai ana kuendeleza utekelzwaji wa masuala kuu yaliyoakubaliwa kwenye kikao cha Julai 19.
    • Pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya moja kwa moja ya amani baada ya kuafikiana kuhusu masuala muhimu yanayohusu mzozo. Mazungumzo haya yatakuwa sawa na yale yaliyotiwa saini jijini Washinton DC – Marekani kati ya DRC na Rwanda mnamo Juni 27 , 2025.
    • Wamekubaliana kwamba mazungumzo hayo ya amani yanapaswa kupata suluhu na kutiwa saini ifikapo Agosti 18 2025.
    • Kuhusu makubaliano ya amani ya kudumu – pande zote zimetambuwa kwamba kuwepo kwa mkataba wa amani ambao unahakikisha usalama, maendeleo, haki za kijamii, na ulinzi wa haki za raia wa DRC na kurejea nyumbani kwa wakimbizi ni jambo muhimu huku wahusika wakiangazia vyanzo vya mzozo.
    • Kuhusu kusitsihwa vita kabisa – pande husika zimetambuwa kwamba amani, usalama nae neo kuwa na uthabiti ni mambo muhimu kwa ajili ya kuongeza nafasi za maendeleo, kuboresha hali ya kaisha na kulinda hadhi ya binadamu.
    • DRC na M23 wamekubaliana kuendeleza hali ya kusitisha mapigano na kufanya juhudi za kurejesha amani ya kudumu kwa kusitisha mashambulizi ya angani, kusitisha matamshi ya uzushi, na kutolazimisha vikosi vya pande zote kusogea mbele kutoka maeneo yaliyopo kwa sasa.
    • Kuhusu juhudi za kujenga matumaini na Imani kwa mchakato wa amani pande zote zimejitolea kuhakikishia jamii ya taifa la DRC kwamba kutakuwa na mazingira mazuri ya kuanzisha na kuendeleza mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu.
    • Kuhusu kurejeshwa kwa uongozi wa serikali kuu katika maeneo ambayo M23 inayadhibiti – pande husika zimetambua kwamba kurejeshwa kwa uwakilishiwa serikali kuu katika maeneo hayo ni jambo ambalo linafaa baada tu ya kuangazia masuala au vyanzo vya mzozo huu ambavyo vitakuwa suluhu inayofuatwa kwenye makubaliano ya amani.
    • Kuhusu kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa ndani na waliopo kwenye nchi Jirani – pande zote zimesema kwamba zitatoa nafasi ya raia kurejea nyumbani kwa njia salama, kwa kujitolea na katika hali ambayo inahifadhi hadhi na haki zao za kibinadamu.
    • Kuhusu kudumisha usalama unaotolewa na kikosi cha kimataifa cha MONUSCO na mengine ya kikanda – pande husika zimekubaliana kwamba vikosi hivyo vitaendelea kudumisha usalama kw amuda ambao walikubaliana na kwamba watasaidia pia kuhakikisha kwamba amnai inadumu na hatua ya kusitisha mapigano inadumishwa.

    Unaweza pia kusoma:

  4. Tahariri: Kwanini Polepole amejiuzulu?, Na Sammy Awami

    h

    Chanzo cha picha, Hamfrey Polepole/Facebook

    Maswali bado ni mengi juu ya sababu hasa ya Balozi Polepole kujiuzulu:

    • Je, ni kwasababu ya madai ya kuhujumiwa kazini?
    • Mwenendo wa CCM? au
    • Vitendo vya utekaji vinavyoendelea?

    Baada ya kuitazama hotuba yake mara kadhaa nakuitathmini kwa makini zaidi, nimefikia hitimisho binafsi kwamba sababu yake kuu ni madai ya kuhujumiwa kazini.

    Kwanza, haya ndio madai ambayo Polepole anasema amekwenda kulalamika kwa viongozi wa ngazi za juu

    Pili, anadai kwamba kwa kuhujumiwa huku ameshindwa kupata matokeo katika kazi yake. Na amesisitiza mwenyewe kwamba yeye anasukumwa na matokeo, si fedha - na asipopata matokeo hawezi kuvumilia.

    Tatu, Safari ya ubalozi ya Polepole imetafsiriwa na wengi kwamba ni ya kisiasa, na kwamba kupelekwa kwake Malawi na Cuba kulilenga kumuweka mbali na siasa za nchi - ni ngumu kuona anawezaje kupata matokeo kwa uteuzi wa mazingira kama haya

    Hili la mwenendo CCM na utekaji unaweza kusema amepata ujasiri na fursa wa kuyazungumzia kwasababu tu sasa hana tena kizuizi cha utumishi wa umma.

    Lakini wapo ambao wamevunjwa moyo kwa namna moja au nyingine - au hata kumuona mbinafsi- hasa wale waliotarajia kwamba sababu kuu ya kujiuzulu ingekuwa masuala ya mapana ya kitaifa kama malamiko ya utekaji na watu kupotezwa.

    Kundi hili wanaweza kumlaumu kwamba kwasababu tu mambo yake binafsi yamekwama, Sasa anaibuka kuzungumzia mambo ya chama- ambayo yametokea miezi mingi iliyopita na utekaji ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu sasa, na wengine wakimlaumu kwa kutoyapigia kelele wakati wa awamu ya tano alipokuwa na ushawishi zaidi.

    Unaweza pia kusoma:

  5. Tuzo ya Mandela ya Umoja wa Mataifa: Kennegy Odede ndiye mshindi wa 2025

    g

    Chanzo cha picha, Kennedy Odede/X

    Kennedy Odede - Mjasiriamali na mwanzilishi wa shirika la kijamii la Shining Hope for communities {Shofco}, ndiye mshindi wa tuzo yam waka huu ya UN Mandela. Odede aliyekabidhiwa tuzo hiyo katika makao makuu ya umoja wa mataifa jijini New York, Marekani ametambuliwa kwa juhudi zake za kuboresha hali ya maisha katika jamii ambazo zinakipato cha chini na zinaishi kwenye vitongoji duni vya jiji kuu la Nairobi.

    Tuzo hiyo iliyopata jina lake kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Rolihlahla Mandela, inatambuwa ujasiri na juhudi wa vijana wa bara Afrika kubadili maisha katika jamii zao.

    Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya Mandela - Mandela Day, Kennedy amesema kwamba amefurahi kutambuliwa na kwamba inampa motisha kuendelea kuitumikia jamii yake akiwa mwenyewe alizaliwa na kulelewa katika mtaa wa mabanda wa Kibera jijini Nairobi.

    “Nilifurahi sana kutambuliwa hivi. Nelson Mandela ni mtu ambaye ninamuenzi pakubwa kwa uongozi wake na juhudi zake za kupigana na uongozi wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

    Kwa Umoja wa mataifa kutambua kazi inayofanywa na shofco ni jambo nzuri kabisa,’ alisema Odede.

    Tuzo ya UN Mandela hutolewa kila baada ya miaka mitano na huangazia vijana wa bara Afrika wanaojishughulisha na majukumu ya kubadilisha na kuboresha maisha katika jamii au hata katiak uongozi.

    Tuzo hiyo iliyotolewa kwa mara ya kwanza 2015.

    Washindi wa 2025 ni Brenda Reynolds wa Canada na Kenendy Odede wa Kenya walioteuliwa na kamati ya uteuzi iliyowasilisha majina yao kwa umoja wa mataifa.

    “Kwangu mimi na shirika langu, utambulisho huu ni mkubwa na inatupa matumaini kwamba tunaweza kushawishi mashirika mengine kama yetu yaliyo barani Afrika kuendeleza kazi ambazo zinafaidi jamii,’ alisema Odede.

  6. Zelensky: Ukraine imeshambuliwa na droni zaidi ya 300 za urusi na makombora 30 usiku

    h

    Chanzo cha picha, Odessa State Emergency Service

    Rais wa Ukraine alizungumzia kuhusu shambulizi kubwa la Urusi na kuripoti kwamba ndege zisizo na rubani bado zimesalia katika anga ya nchi hiyo.

    "Donetsk, Kirovohrad, Dnipropetrovsk, Sumy, Kherson, Volyn, Zaporizhia, Mykolaiv, Odessa na mikoa ya Zhytomyr iliteseka, alisema.

    Miundombinu muhimu iliharibiwa huko Sumy - familia elfu kadhaa ziliachwa bila ugavi wa umeme. Mashambulizi ya mkupuo yalifanyika dhidi ya Shostka. Jengo la makazi liliharibiwa katika Odessa.

    Aliongeza kuwa ''Kwa bahati mbaya, watu sita walijeruhiwa.

    Pia aliwahutubia viongozi wa dunia, akawashukuru kwa msaada wao na akasisitiza haja ya kuanzisha uzalishaji wa zana za kijeshi nchini Ukraine.

    "Uzalishaji wa pamoja wa silaha, uwekezaji katika utengenezaji wa ndege zisizo na rubani nchini Ukraine, hasa ndege zisizo na rubani, utoaji wa mifumo ya ulinzi wa anga na makombora kwa ajili yake, pamoja na uwezekano wa uzalishaji wake hapa Ukraine - yote haya yanaokoa maisha na yanahitajika Ukraine hivi sasa," Zelensky aliandika.

    Unaweza pia kusoma:

  7. 'Gangsta Debbs' – Mongwe aliyetumia familia yake kuendesha biashara ya madawa ya kulevya

    h

    Chanzo cha picha, Met Police

    Mapema asubuhi ya Aprili 2023 maafisa wa ujasusi walimtazama mwanamke akipakia masanduku kwenye gari la kukodi kwenye duka la bidhaa za reja reja karibu na bandari ya Harwich huko Essex.

    Walipata taarifa kuhusu gari lililokuwa limesafiri kutoka Islington usiku huo.

    Gari hilo liliendeshwa kuelekea Ipswich, ambapo mwanamke huyo alikabidhi begi zito la nguo kwa mtu asiyejulikana.

    Hakuonekana kama mtu ambaye ungetarajiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya - wakili wake wa utetezi alisema "bila shaka alitajwa kama mtu ambaye hangevutia macho".

    g

    Chanzo cha picha, Met Police

    Maelezo ya picha, Deborah Mason alijiita Gangsta Debbs. Binti yake, Demi Bright, alihifadhi nambari ya mamake kwenye simu yake kama 'Queen Bee'.

    Mwanamke huyo alikuwa Deborah Mason, anayejulikana kwa familia kama Gangsta Debbs au Malkia Bee: bibi na mama mkuu wa familia ya uhalifu ambayo ilifanya kazi kote kusini mashariki mwa Uingereza.

    Mason alikuwa amewaajiri watoto wake wanne, dada yake na watu wengine wa karibu wa familia kusaidia usambazaji wa Kokeini kote nchini - kufadhili maisha ya kifahari ambayo yalijumuisha bidhaa za mbuni wa Gucci zilizonunuliwa kwa paka wake na birika la kifahari la Bugatti la pauni 192.

    Siku ya Ijumaa, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 65 alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kula njama ya kusambaza dawa za Daraja A katika Mahakama ya Woolwich Crown.

    Wengine katika genge hilo walipata hukumu ya vifungo vya kati ya miaka 10 na 15 kwa mashtaka sawa.

  8. Marekani yahimiza amani DRC huku mkataba wa usitisha mapigano kati ya serikali na M23 ukiafikiwa

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, hatua hii ni ishara ya hatua iliyopigwa baada ya mazungumzo yaliyochukuwa miezi kadhaa iliyoandaliwa nchini Qatar

    Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kundi la waasi la M23, wamekubaliana kutia saini azimio la kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa DRC.

    Kwa mujibu wa waangalizi wa mzozo huo, hatua hii ni ishara ya hatua iliyopigwa baada ya mazungumzo yaliyochukuwa miezi kadhaa iliyoandaliwa nchini Qatar, japo taarifa za ziada kuhusu walichokizungumzia na kukubaliana hazijawekwa wazi.

    Azimio hilo linalotarajiwa kutiwa saini Jumamosi hii jijini Doha, linatangazwa wakati ambapo Marekani imezidisha shinikizo lake kwa pande husika kukamilisha masuala muhimu kwenye majadiliano hayo yanayotarajiwa kurejesha amani katika eneo la Mashariki mwa Congo.

    Hatua hii huenda ikavutia wawekezaji kutoka wa mataifa ya Magharibi ambao wanatarajiwa kuwekeza mabilioni ya dola za Marekani kwenye eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini kama vile tantalum, dhahabu,cobalt, shaba nyekundu, lithium miongoni mwa mengine mengi.

    Kundi la M23, lililoyateka maeneo ya mashariki mwa nchi limekuwal ikikabiliana na jeshi la FARDC mashariki mwa DRC, hatua yao kubwa ya hivi maajuzi ilikuwa kuteka na kudhibiti mji wa Goma, mwezi Januari na baada ya hapo limepiga hatua kubwa ya kudhibiti na kukalia eneo kubwa katika majimbo mawili ya Kivu Kusini na Kivu Kasakazini.

    Vita hivyo vimesababisha maafa ya maelfu ya watu na kuwalazimu mamilioni zaidi kukimbia makwao kwa ajili ya usalama wao.

    Makabiliano hayo kwa wakati mmoja yalitishia kuzua vita vikuu katika eneo hilo, na kusambaa hadi katika ukanda mzima na kuyahusisha mataifa jirani. Mataifa Jirani yametuma majeshi yao kwenye eneo hilo.

    Unaweza pia kusoma:

  9. Mkurugenzi Mtendaji wa Teknolojia wa Marekani asimamishwa kazi baada ya kumkumbatia mwanamke

    Maelezo ya video, Ulikuwa wakati mgumu kwa wanandoa hawa ambao kila mmoja ana ndoa yake kuonekana kwenye skrini kwenye tamasha la Coldplay

    Kampuni ya teknolojia nchini Marekani imemuweka likizoni Mkurugenzi Mtendaji wake baada ya picha ya skrini iliyomuonyesha akikumbatiana na mwanamke kwenye tamasha la Coldplay - linalodaiwa kuhusisha wafanyakazi wake wawili - kusambaa kwa kasi.

    Katika klipu hiyo, ambayo awali ilionekana kwenye skrini kubwa kwenye Uwanja wa Gillette huko Foxborough, Massachusetts, watu wawili wanaonekana wakiwa wamekumbatiana na kushikana mikono.

    Nyuso zao zinapoonekana kwa maelfu ya watu, mwanamume na mwanamke huyo ghafla walionekana wakijificha na kuonekana waondoka kwenye kamera.

    Ripoti kwamba wote wawili ni wasimamizi wa kampuni ya Mnajimu na uvumi wa uhusiano uliochochewa na maoni ya kiongozi wa bendi, kisha zilienea mtandaoni. Siku ya Ijumaa, kampuni hiyo ilithibitisha kwenye X kwamba Mkurugenzi Mtendaji wake Andy Byron alikuwa amewekwa likizo.

    Video ya wawili hao wakicheza muziki, kisha kujaribu kujificha haraka ilisambaa kwa kasi kwenye mtandao baada ya tamasha Jumatano usiku.

    Chris Martin, muimbaji mkuu wa Coldplay, baada ya kuwaona wawili hao wakijificha, aliuambia umati: "Ama wana uhusiano wa kimapenzi, au wana aibu sana."

    Video ya kwanza iliyotumwa kwa TikTok ilipokea mamilioni ya maoni. Kisha ilishirikiwa kwenye majukwaa, ikageuzwa kuwa meme na kukejeliwa kwenye vipindi vya televisheni.

    Unaweza pia kusoma:

  10. Syria na Israel zafikia makubaliano ya kusitisha mapigano 'kwa msaada wa Jordan na Uturuki'

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Vikosi vya usalama vya Syria vimesimama kwenye kifaru mnamo Julai 15, 2025, karibu na mkoa wa kusini wa As-Suwayda

    Balozi wa Marekani nchini Uturuki na Mjumbe Maalumu wa Syria Tom Barrack amesema kuwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkuu wa mamlaka ya mpito nchini Syria Ahmad al-Sharaa walikubaliana kusitisha mapigano kwa msaada wa Uturuki, Jordan na nchi jirani.

    "Tunatoa wito kwa Druze, Bedouins, na Wasunni kuweka chini silaha zao na kufanya kazi na watu wengine walio wachache kujenga utambulisho mpya wa Syria," Barrak alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Twitter.

    Siku ya Jumatano, Israel ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Damascus, yakilenga majeshi ya serikali ya kusini, na kutaka waondoke, ikisema wakati huo "ililenga kulinda kuwalinda watu wa jamii ya Druze ya Syria."

    Damascus iliweka vikosi hivi kufuatia mapigano kati ya makabila ya Bedouin na wanamgambo wa Druze.

    Unaweza pia kusoma:

  11. Kansela wa Ujerumani aiambia BBC jinsi Ulaya inavyojitegemea kutoka kwa Marekani

    h

    Chanzo cha picha, Jeff Overs/BBC

    Maelezo ya picha, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz

    Katika nyanja ya usalama, Ulaya tayari imeacha "kuendesha gari bila kuilipa Marekani" na inaanza kuwekeza kwa umakini katika utetezi wake, wakati Urusi inatishia sio Ukraine tu, bali Ulaya yote, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz alisema katika mahojiano na kipindi cha BBC Today.

    "Tunaona tishio kubwa - na hiyo ni Urusi. Tishio hili si dhidi ya Ukraine pekee. Ni tishio kwa amani yetu, uhuru wetu na utaratibu wa kisiasa wa Ulaya," alisema Merz, ambaye alikuja Uingereza kutia saini makubaliano ya kihistoria ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika maeneo mbalimbali, ambayo yaliitwa Mkataba wa Kensington. Pia ina maana ya kuimarisha uhusiano wa kiulinzi kati ya Ujerumani na Uingereza.

    Merz alikuwa mfuasi mkubwa wa Ukraine wakati wa kampeni za uchaguzi na alisafiri hadi Kyiv kwa treni siku nne baada ya kuchukua madaraka, pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

    Hata kabla ya kuchukua madaraka rasmi, Merz alikuwa amesukuma mabadiliko ya katiba ya Ujerumani ili kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi ya ulinzi, akitangaza kwamba kanuni kuu ya ulinzi ya FRG sasa ilikuwa "kufanya chochote kinachohitajika."

    "Hatuna nguvu za kutosha, jeshi letu halina nguvu za kutosha - ndiyo maana tunatumia pesa nyingi," aliambia BBC.

    Anakubaliana na maoni ya uongozi wa Marekani kwamba Ulaya inachangia kidogo sana kwa ajili ya ulinzi na usalama wake - lakini anaamini kuwa hali sasa imebadilika.

    "Tunajua kwamba tunapaswa kufanya zaidi [katika eneo hili] kwa kujitegemea, na kabla ya 'tulikuwa hatulipi,'" alieleza. "Wao [Marekani] wanatuomba kufanya zaidi - na kwa kweli tunafanya zaidi.

    Unaweza pia kusoma:

  12. Urusi yazipiga ndege 87 zisizo na rubani za Ukraine katika muda wa Chini ya saa tano

    g
    Maelezo ya picha, Ndege aina ya Raybird anaweza kuruka bila kusimama zaidi ya kilomita 1,000 ili kupeleleza na kugonga shabaha ndani ya Urusi

    Moscow, mifumo ya ulinzi wa anga imeharibu na kuzidungua ndege 87 za angani zisizo na rubani, Wizara ya Ulinzi ya Urusi iliripoti kwenye chaneli yake ya Telegram.

    Imebainika kuwa ndege tano zisizo na rubani zilidunguliwa katika eneo la mkoa wa Moscow, zikiwemo mbili zilizokuwa zikielekea Moscow. Angalau ndege zisizo na rubani mbili zilipigwa risasi wakati wa kipindi maalum, Meya wa Moscow Sergei Sobyanin na mkuu wa utawala wa Dmitrov katika mkoa wa Moscow alisema.

    Nyingine 48 walipigwa risasi juu ya mkoa wa Bryansk, 12 juu ya mkoa wa Oryol, 10 juu ya mkoa wa Kaluga, nane juu ya mkoa wa Rostov, na moja katika mikoa ya Tula, Kursk, Smolensk, na Voronezh, jeshi la Urusi liliandika kwenye Telegram yake maalumu

    Bado hakuna uthibitisho huru wa taarifa hii au majibu kutoka kwa upande wa Ukraine.

    Unaweza pia kusoma:

  13. Hujambo na karibu kwa matangazo haya mubashara ya Jumamosi 19.07.2025 tukikuletea habari za kikanda na kimataifa