Kwanini majirani wa Urusi wanazitaka nchi za Nato kurudisha huduma ya kijeshi?

fcv
Maelezo ya picha, Toivo Saabas ni miongoni mwa vijana wa Kiestonia wanaopitia utumishi wao wa kijeshi

Toivo Saabas, mwanaume mwenye umri wa miaka 25 anasimama. Akitengeneza mstari akiwa na wapiganaji zake, anapitia kwenye miti kusonga mbele.

Ni mhitimu wa uhandisi wa mitambo, Chuo Kikuu cha Southampton.

"Tunafanya mazoezi. Tuko tayari kwa lolote litakalokuja Estonia na tuko tayari kutetea nchi yetu,” anasema.

Toivo, kutoka mji mkuu wa Tallinn, ni miongoni mwa vijana wa Kiestonia wanaopitia utumishi wao wa kijeshi - jukumu ambalo wanaume wote wenye umri wa zaidi ya miaka 18 wanaombwa kulitekeleza. Kwa wanawake, ni hiari.

Vita Baridi vilipoisha, na kukawepo uhusiano na Urusi ya baada ya Sovieti katika miaka ya 1990, uandikishaji wa mafunzo ya kijeshi ulionekana kuwa ni jambo lililomaliza katika sehemu nyingi za Ulaya.

Lakini si Estonia. Kufuatia uvamizi wa Rais Putin nchini Ukraine, usajili wa kijeshi unaanzishwa upya na kupanuliwa kote Ulaya, huku wale wanaoishi kwenye mpaka na Urusi wakiwataka washirika wao wa Nato, ikiwa ni pamoja na Uingereza, kuiga mfano huo.

Wiki hii Norway ilitangaza kuwa inaongeza idadi ya wanajeshi baada ya Denmark kusema mwezi uliopita inakusudia kuongeza muda wa kujiandikisha kwa wanawake na kuongeza muda wa kuhudumu.

Latvia na Sweden zilianza tena mafunzo ya kijeshi kwa vijana. Nayo Lithuania ilirudisha mpaka kama huo baada ya Urusi kunyakua Crimea 2014.

Toivo aliyezama, anasema mafunzo hayo ndio jambo gumu zaidi maishani mwake.

"Lakini mwishowe, ni huduma kwa ajili ya nchi yako. Kuwa tayari kwa lolote ni bora kuliko kutoroka na kujaribu kukwepa huduma hii."

Miaka 75 ya Nato

FCV
Maelezo ya picha, Waestonia wana wasiwasi kuhusu kile ambacho Vladimir Putin anaweza kufanya baadaye, anasema Waziri Mkuu Kaja Kallas
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Urusi haijawahi kushambulia nchi ndani ya Nato, ambapo makubaliano ya pamoja ya ulinzi yanamaanisha shambulio dhidi ya mwanachama mmoja ni shambulio kwa wote.

Nchi tatu za Nato - Uingereza, Marekani na Ufaransa - kila moja ina silaha za nyuklia, kama ilivyo kwa Urusi, hivyo kuna wasiwasi kuongezeka hatari ya vita vya nyuklia kutokana na mzozo huo.

Muungano wa kijeshi wa Nato sasa ni klabu ya nchi 32 wakiwemo wanachama wapya Finland na Sweden. Wiki hii inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75.

Kwake, washirika wa Nato kutimiza ahadi yao ya 2% ya Pato la Taifa katika ulinzi ni nini muhimu. Mwaka 1938, ilikuwa wazi kwamba vita vinakuja hivyo matumizi ya ulinzi yaliongezwa kwa 100% lakini tayari ilikuwa imechelewa.

Mwaka 2024, chini ya theluthi mbili ya wanachama wa Nato wako kwenye jitihada ya kufikia lengo lao la ufadhili la 2%, upungufu ambao ulimkasirisha sana Rais wa Marekani, Donald Trump wakati akiwa katika Ikulu ya Marekani.

Waziri Mkuu wa Estonia, Kaja Kallas, ambaye ameiongoza tangu 2021, anaona vijana kuandikishwa jeshini ni jambo muhimu kutoa upinzani dhidi ya Urusi lakini pia ulinzi mkali zaidi ikiwa itashambulia.

"Tuna jeshi la akiba la watu 44,000. Na kila nchi inajiamulia yenyewe, lakini napendekeza nchi kuongeza jeshi la akiba."

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Uingereza aliiambia BBC kwamba "hakuna pendekezo lolote la kurejeshwa kwa jeshi mafunzo ya kijeshi kwa vijana."

Serikali ya Uingereza inasema pauni bilioni 50 inawekezwa katika vikosi vyake vya kijeshi mwaka 2024 ili kukabiliana na vitisho, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, na kuongeza uandikishaji na kuboresha jeshi ni vipaumbele vyao."

VC
Maelezo ya picha, Wanamuziki Villem Sarapuu na Hendrik Tamberg wanaamini kuwa kuna njia zingine za kuwakilisha Estonia

Huduma ya kijeshi inaweza kuwa inafufuliwa, lakini haimaanishi Waestonia wote vijana wan shauku ya kujiunga.

"Mimi sio mwanajeshi" anaimba Villem Sarapuu mwenye umri wa miaka 25 katika wimbo wao wake wa Smokin' Aces.

"Sidhani kama kuna watu wengi ambao wanaenda huko kwenye jeshi kwa hiari.

Baada ya mafunzo ya awali ya kimwili, Villem alitumia miezi yake sita iliyobaki na hatimaye alitumbuiza kwenye gwaride la Siku ya Uhuru.

Aliyeketi karibu naye ni mshiriki wa bendi Hendrik Tamberg, 28.

Akiwa amekataa kujiunga na jeshi na badala yake alitumia mwaka mzima kuwatunza watu wazima walio hatarini waliokuwa na matatizo ya akili.

Kuhusu mwimbaji mkuu Villem, anasema sasa anatazama nyuma katika mafunzo yake ya kijeshi akiwa na kumbukumbu za furaha na anasema ni tofauti kabisa na hali ya wasiwasi ambayo kizazi chake kinahisi nayo.

"Katika nchi kama vile Estonia, ndogo sana, ni muhimu kuajiri watu kujiunga na jeshi. Au nchi hii haitakuwepo tena," anasema Villem.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah