'Kuzuiwa kuingia Angola ni shambulizi dhidi ya Diplomasia na Demokrasia Afrika'- Masoud

Chanzo cha picha, ACT
Kundi la vyama vya upinzani barani Afrika kupitia Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD), limetaja kitendo cha serikali ya Angola kuwazuia wanasiasa wakuu wa upinzani kutoka barani kote kuingia nchini humo ni shambulizi dhidi ya demokrasia
Katika taarifa yao ya pamoja, limesema kitendo cha Mamlaka za Angola kuzuia karibu viongozi wakubwa wa upinzani karibu 40 kutoka nchi zaidi ya 20 ni kampeni ya kimfumo na ya kijinga ya kushambulia na kudhoofisha maendeleo kuelekea demokrasia na uwajibikaji barani Afrika.
Viongozi hao walizuiwa katika uwanja wa ndege wa Luanda, wilipowasilia kushiriki katika mjadala wa siku nne wa Jukwaa la Demokrasia Afrika, yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation, ambayo yalianza Machi 13 na yatakamilika Machi 16.
Baadhi ya viongozi waliozuiwa hapo jana, kunyanganywa hati zao za kusafiria na wengine kuzuiwa kwa zaidi ya masaa 9 kwenye uwanja huo wa ndege, ni pamoja na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud, ambaye amelaani kitendo hicho.
'Kitendo kile ni shambulio dhidi ya Diplomasia na Demokrasia Afrika', alisema Masoud.
Mbali na kiongozi huyo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo Tanzania, alikuwepo pia rais wa zamani wa Botswana, Ian Khama, Waziri mkuu wa zamani wa Lesotho Moeketsi Majoro, rais wa zamani wa Colombia, Andrés Pastrana Arango na wapinzani wengine 24 ambar walishikiliwa kwa saa 9 kwenye uwanja huo.
Wapinzani wengine waluozuiwa ni pamoja na mwenyekiti wa chama kikuu cha Upinzani Tanzania, CHADEMA, Tundu Lissu, Kiongozi wa upinzani Uganda, Robert Kyagulanyi (Bbobi Wine), na Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna.
Wapo waliozuiwa kwa muda na kurudishwa katika nchi sao, kabla ya bade kuruhusiwa kuingia nchini humo.
Mamlaka za Angola zinasema, kilichotokea ni masuala ya uhamiaji zikigusia kuhusu utaratibu wa vibali vya kuingia nchini humo vilivyopaswa kufuata utaratibu wa sheria.















