Viongozi wa waasi Syria wasema wamejiondoa kutoka kwa historia yao ya jihadi- je, wanaweza kuaminika?

gg
    • Author, Mina Al-Lami
    • Nafasi, Chief jihadist media specialist, BBC Monitoring
  • Muda wa kusoma: Dakika 9

Wiki jana ,akizuru katika eneo la Damascus ,kiongozi mpya wa Syria Ahmed al - Sharaa ( anayejulikana kama Abu Mohammed al - Jolani) aliombwa na mwanamke mmoja wapige picha kwa pamoja.

Kwa upole alimuomba ajisitiri kichwa chake kabla ya kupiga naye picha.

Tukio hilo liligonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari katika mataifa ya kiarabu na kuzua hisia mseto.

Kilichotokea huenda kikaonekana sio jambo kubwa , lakini ilikuwa ina maana kuwa viongozi wapya wa Syria Hayat Tahrir al- Sham (HTS) - ambao wamekuwa wakitajwa kama kundi la wanamgambo na Marekani,Umoja wa mataifa ,Umoja wa Ulaya na Uingereza - watakuwepo.

Kwa upande mmoja kuna jamii ya Syria yenye utofauti na, katika baadhi ya matukio, jamii ya kidemokrasia, pamoja na jumuiya ya kimataifa, ambayo kuwaidhinisha itakuwa muhimu kwa kundi hilo la HTS kuendelea kuhudumu na kudumisha uhalali wao.

Kwao, tukio la kufunika nywele lilionyesha wasiwasi kuhusu mustakabali wa Syria chini ya HTS, na hofu kwamba sera za kihafidhina zinaweza kupelekea wanawake wote kulazimishwa kuvaa hijabu.

Kwa upande mwingine wanaharakati wa kiislamu wamemkosoa al - Sharaa kwa kupiga picha na mwanamke, wakimsawiri mwanamke kama ''mutabarijah'' - neno linalotumika kumuelezea mwanamke anayeaminika kuwa anavalia mavazi yasiyofaa au kujipodoa - na kusisitiza kitendo chake kilikiuka sheria za kidini.

Wanaharakati hawa wana ushawishi mkubwa katika makundi ya kijihadi na wanaweza kuhamasisha upinzani ndani ya kundi la al-Sharaa lenye misingi ya Kiislamu.

HTS inakabiliwa na changamoto ya kujitahidi kuleta usawa kati ya masharti haya yanayopingana – huku ikijitahidi kuridhisha matarajio ya jamii ya kimataifa na sehemu za kidemokrasia za Syria, huku ikihitaji kutimiza matarajio ya wanaharakati wa misingi ya kidini. Pande zote mbili zinachunguza kwa karibu kauli na vitendo vya HTS.

Uwezo wao wa kuridhisha pande zote mbili utaamua mustakabali wao katika siasa nchini Syria.

Ahmed al-Sharaa (aliyekuwa akifahamika kama Abu Mohammed al-Jolani)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ahmed al-Sharaa (aliyekuwa akifahamika kama Abu Mohammed al-Jolani)

Katika taarifa zake ambazo amekuwa akizitoa baada ya kuchukua usukani nchini Syria, ni kama vile kusamehe wanajeshi wa zamani, kukataza kulipiza kisasi kwa waliokuwa maafisa wa Assad na kukumbatia kauli za kimaelewano wakati anapozungumza na maadui wa jadi, ikiwa ni pamoja na Israel, Marekani, Iran na Urusi.

Taarifa zake zimekuwa hazijikiti katika masuala ya vitisho na badala yake kuegemea upatanisho, maridhiano, udhabiti, na ujenzi wa taifa katika juhudi za wazi za kuondoa upinzani na kuondoa HTS na al-Sharaa kutoka kwenye orodha za kigaidi za kimataifa.

Changamoto zilizopo

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bado haijabinika wazi iwapo ni mbinu ya al-Sharaa ni mabadiliko halisi ya kiitikadi au ni mkakati wa kisiasa wa kujitengezea sifa ili kukubalika na raia kabla ya kuanza kutekeleza ajenda zilizo na misimamo mikali ya kidini.

Lakini tayari, hatua zake za kisasa zinazua wasiwasi mkubwa kwa wanaharakati wa kiimla katika Syria, ambao wanasisitiza kuwa serikali ya Kiislamu inapaswa kuzingatia utambulisho wa Kiislamu wa kanuni za Sunni.

Ingawa kundi la Sunni ndilo kubwa nchini Syria , kuna jamii za walio wachache kama vile Shia Alawites, ambao ni chimbuko la Bashar al- Assad rais aliyeondolewa- Kurdi, wakristo, Druze, Turkmen and Ismailis, pamoja na vikundi vingine vidogo zaidi.

Hata kama uongozi wa HTS unataka mabadiliko kwa dhati, kundi hili linakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa makundi ya kijihadi na Kiislamu yaliyoshikamana na Syria kwa muda mrefu – waliokuwa wakipinga utawala wa awali na hawataruhusu mkondo huo bali watataka nchi iongozwe kwa misingi ya kiislamu.

Iwapo HTS wataonekana kuchukua mkondo tofauti na makundi hayo basi watatarajia upinzani mkali katika utawala wao.

Japokuwa changamoto hii si geni kwa HTS.

Pia unaweza kusoma:

Kutoka IS kisha al- Qaeda na sasa HTS

Kwa muongo mmoja, kundi hili lilijulikana kama al-Nusra Front na lilikuwa na mizizi katika harakati za kijihadi za kimataifa.

HTS ilitoka kuwa tawi la siri la kundi kali la IS kuanzia mwaka wa 2011 na 2012, na kisha kuungana na al-Qaeda mwaka uliofuata, na kufikia mwaka 2016 kuwa tawi huru.

Ilichukua usukani katika mkoa wa Idlib , kaskazini magharibi mwa Syria mwaka 2017, wakitawala kiraia ulioitwa Serikali ya Ukombozi wa Syria (SSG), ambayo ilifanya kazi kwa ufanisi kwa kuonyesha uwezo wake wa kuongoza na kusimamia huduma za msingi kama elimu na afya.

Mkakati wa HTS unaashiria kuwa Syria sio tishio kwa ulimwengu.

Hayat Tahrir al-Sham (HTS) ilikuwa kundi huru mwaka 2016

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hayat Tahrir al-Sham (HTS) ilikuwa kundi huru mwaka 2016

Huku washirika wake wakuu wa jihadi , al-Qaeda na IS walikuwa wamemulikwa zaidi na muungano uliongozwa na Marekani- na hadi kiongozi wao kuuawa, cha kushangaza ni kuwa Idlib - al Sharaa wametawala kwa utulivu na uhuru.

Licha ya Marekani kuweka dhamana ya kitita cha dola milioni 10 cha kumuuawa kingozi huyo, amekuwa akijitokeza hadharani, kujumuika na watu kama mtu mwenye ustadi wa utawala.

Hata hivyo, wakosoaji wa al-Sharaa, ambao ni wanajihadi, wanamshutumu kwa kuwa mwanasiasa mwerevu ambaye yuko tayari kuachana na misingi muhimu ya kiitikadi ili kusonga mbele kisiasa na kupata faida kwa HTS, kwa gharama ya makundi mengine ya kijihadi nchini Syria.

Jinsi waasi walivyoteka nyoyo za watu na kupendwa

HTS ilijijengea mamlaka huko Idlib kwa kutumia mkakati wa aina mbili: kuwaridhisha wenyeji kwa kuwajengeza mazingira tulivu ,huku ikitumia nguvu kudhibiti washindani na hata washirika wa zamani.

Kundi hili lilijiondoa kwa msimamo wa kigaidi wa kuanzisha utawala wa kiislamu nchini Syria wa sheria kama sehemu ya mradi mkubwa wa kimataifa. Badala yake, walitumia mkakati wa "mapinduzi" na kitaifa, wakilenga lengo moja kuu la kuondoa Rais Bashar al-Assad na "kuikomboa" Syria.

Kutawala kiraia eneo la Idlib ilikuwa ni mkakati wao wa kuaminisha kuwa makundi ya kijihadi yanaweza kuendesha mkoa, na kujitenga na picha mbaya ya utawala wa IS katika maeneo ya Syria na Iraq.

SSG ilikuwa na muundo wa serikali ya mji mdogo, ikiwa na waziri mkuu, wizara, na idara za ndani zinazoshughulikia sekta muhimu kama elimu, afya na ujenzi, yote yakiongozwa na baraza la kidini la Sharia.

Pia, walianzisha shule za kijeshi na polisi na mara kwa mara walionyesha sherehe za kuhitimu , ambazo mara nyingi zilihudhuriwa na al-Sharaa.

Al-Sharaa pia ilihudhuria mara mbili hafla ya uzinduzi wa vitabu na kuzungumza na wakaazi.

Lakini utawala wa HTS katika mkoa huo wa Idib ulikuwa na misukosuko chungu nzima.

Kabla ya mwezi Novemba mahasimu wao wa kisiasa waliandamana dhidi ya uongozi.

Waandamanaji waliandamana baada ya tetesi kuwa wakosoaji wa serikali walipotea bila kupatikana na wengine kuzuiliwa jela.

Wapiganaji wa waasi Syria wakisherehekea huko Hamas baada ya wanajeshi wa Syria kuondoa wanajeshi wake eneo hilo

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wapiganaji wa waasi Syria wakisherehekea huko Hamas baada ya wanajeshi wa Syria kuondoa wanajeshi wake eneo hilo

Kundi hili pia limekosolewa vikali wakidaiwa kushirikiana na mataifa ya kigeni kudhoofisha jihadi nchini Syria.

Mwaka 2023 ilikumbwa na sakata ya majasusi kuingilia uongozi wao huku wanaharakati wa misimamo mikali wakialaumu kwa kutolipiza kisasi dhidi ya serikali ya awali wakiogopa kutokosea wasaidizi wao kutoka mataifa ya kigeni ambayo kufikia sasa haijabainika ni akina nani.

Hata hivyo wakosoaji wa HTS wa zamani na sasa walikuwa wenye misimamo mikali dhidi ya miradi ya al- Sharaa eneo la Idliba.

Na wengine pia wanakosoa wakidai kuwa kundi hilo lina chembe chembe za udikteta.

misimamo mikali vs misimamo ya demokrasia: vikwazo vya dini

Ingawa kuna baadhi ya raia kuripoti malalamiko ya kulazimishwa kufuata sheria za kidini eneo la Adlib malalamiko haya hayakufikia wengi.

Huenda ni kutokana na jamii inayoishi eneo hilo kuwa Sunni ilikuwa rahisi kuweka masharti ya kidini na kufuatwa pila pingamizi.

Al sharaa walijitetea kwa kusema watu wanapaswa kufuata mafundisho ya kiislamu kwa hiari na sio kwa nguvu.

''Hatutaki tujenge mazingira kuwa watu wanafanya ibada tukiwa na tukikosekana wanapuuza ibada zao.''

Licha matamshi hayo ambayo yamepambwa kuridhisha upande wa wanaotaka mabadiliko, wamekuwa wakitekeleza sheria kali za kidini ili kufurahisha wanaharakati wa kiislamu na huenda hili likatokea watakaposukumwa zaidi na kundi la kiislamu kufuata sheria za kidini.

Mahasimu wengine wa waasi wa HTS

Hadi hivi karibuni, makundi ya upinzani Syria yalikuwa yamegawanyika, yakigombania maeneo na mamlaka, jambo lililoshindwa kuleta ushindi dhidi ya Assad.

Umoja wa waasi uliosababisha kuanguka kwa Assad ni maendeleo mapya, lakini bado una hatari ya kudhoofika kutokana na changamoto za ndani.

HTS ina historia ya uhusiano mbaya na makundi mengine makubwa ya waasi nchini Syria

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, HTS ina historia ya uhusiano mbaya na makundi mengine makubwa ya waasi nchini Syria

HTS imekuwa na uhusiano mbaya na kundi kubwa la waasi linaloungwa mkono na Uturuki, Jeshi la Kitaifa la Syria (SNA).

SNA imekuwa ikilenga maeneo ya Kikurdi kaskazini mwa Syria, ili kuondoa tishio linaloonekana kutoka kwa Wakurdi.

Haijulikani kama makundi haya mawili yanaweza kufikia makubaliano kuhusu kugawana maeneo muhimu, kwani HTS inasisitiza umoja kamili chini ya uongozi wake.

IS bado inafanya kazi Syria kupitia operesheni zao, na imekataa mamlaka ya waasi ya HTS kama "waasi" waliowekwa madarakani na nguvu za kigeni.

IS inatarajiwa kusimamia magereza na kambi za Wakurdi, hasa huko Hasaka, ambapo inatarajiwa kuwaachia huru wafungwa wake na kuongeza nguvu zake.

Tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria kuanza mwaka 2011, Syria imekuwa kivutio kwa wapiganaji wa kigeni na makundi ya kijihadi.

HTS ilivunja baadhi ya makundi ya ndani na ya kigeni, na kujiunga nayo ili kudhibiti Idlib, ikijumuisha makundi kutoka Asia ya Kati, wahindi, na Wauyghur wa China.

Makundi haya madogo, ikiwa ni pamoja na Ansar al-Islam na Ansar al-Tawhid, yalishiriki katika mashambulizi ya hivi karibuni, yakionyesha umuhimu wao katika kujenga mustakabali wa Syria mpya.

Baada ya Assad, makundi kama al-Qaeda na wataalamu wa Kiislamu wanakumbusha HTS kutimiza wajibu wake wa kuanzisha mfumo wa Kiislamu Syria, ulio na utambulisho thabiti wa Sunni.

'Kuchukua mamlaka kwa nguvu'

Alipo ulizwa na mwandishi wa CNN tarehe 6 Desemba ikiwa HTS inakusudia kuanzisha mfumo wa Kiislamu, al-Sharaa alijibu kwa kuepuka moja kwa moja, akisema,

"Wale wanaogopa utawala wa Kiislamu ama wameona utekelezaji usio sahihi au hawaujui vyema."

Jibu hili linaashiria kuwa HTS ina mpango wa kuanzisha utawala wa Kiislamu, lakini kwa namna inayoweza kubadilika na yenye mtindo wa kipevu.

Tangu kuangushwa kwa serikali ya Assad, migogoro ya kiitikadi imeanza kuibuka baada ya furaha ya awali na juhudi za pamoja.

Tarehe 9 mwezi Disemba, HTS ilitoa amri ya msamaha kwa askari wa zamani, lakini wapinzani walikosoa hatua hii, wakidai ni "pole" na kinyume na sheria za Sharia, na kuhamasisha upinzani na mashambulizi dhidi ya wafuasi wa serikali iliyopita.

HTS ilijaribu kutuliza hali kwa kusema itawafuata wale waliotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita, huku ikisisitiza kuwa itawadhibiti wote watakaokiuka amri yake kwa kufanya vitendo vya kulipiza kisasi.

Mabishano mengine yalijitokeza tarehe 16 mwezi Disemba, al-Sharaa aliposema mipango ya kufuta makundi ya kijihadi na silaha, na kukusanya silaha mikononi mwa serikali na jeshi pekee.

Wapinzani walipinga, wakisema hatua hii ingekuwa ni kulifanya HTS kuwa na nguvu pekee na kuondoa uwezo wa makundi mengine kupinga utawala wake, na hivyo kusababisha utawala wa kidikteta.

Pia unaweza kusoma:

Kutokana na majibu yaliyolegea ya HTS kuhusu mashambulizi ya angani ya Israel huko Syria baada ya kuanguka kwa Assad, kutoridhika kuliibuka.

Baada ya kimya cha siku kadhaa, tarehe 14 mwezi Disemba, al-Sharaa alikosoa mashambulizi hayo lakini alisema kikundi chake hakikuwa na nia ya kuanzisha vita vipya, akisisitiza kuwa kipaumbele cha sasa ni kujenga tena Syria.

Aliongeza kuwa hataruhusu Syria kutumika kama kigezo cha mashambulizi dhidi ya Israel.

Baadhi waliona msimamo huu kama udhaifu na kutozingatia misingi ya Kiislamu.

Kelele za hasira ziliongezeka baada ya ujumbe kutoka al-Qaeda ukitoa wito kwa HTS kuweka mbele mapambano dhidi ya Israel na kutimiza "wajibu" wao wa kulinda Wapalestina Gaza.

Hali hii inaashiria kuwa wahafidhina, iwe ndani ya HTS au kutoka makundi mengine, wanaweza kuchukua silaha dhidi ya kundi hili ikiwa wataona linajitenga na maono yao ya Syria mpya ya Kiislamu.

Watu na makundi haya mengi yana maslahi makubwa nchini Syria na hayako tayari kuachana na malengo yao kirahisi.

Wanayaona maandalizi ya Syria kama mradi wa kuanzisha dola imara ya Kiislamu ya Sunni, inayoweza kuwa na ushawishi wa kikanda na kuwa kimbilio kwa Waislamu walioteseka na wahalifu wa jihadi.

Kwa shinikizo kutoka kwa waasi na wahafidhina, al-Sharaa na HTS wako njia panda, wakijitahidi kuepuka kukasirisha pande zote mbili, na kuonyesha kuwa ufanisi wao unategemea kubadilika na ustahimilivu.

Wiki moja iliyopita, msichana aliyeomba picha alielekezwa kufunika nywele zake.

Wiki hii, al-Sharaa alionekana katika picha na mabalozi wawili wa Uingereza, mmoja wao akiwa ni Ann Snow, mjumbe maalum wa Uingereza kwa Syria, ambaye alionekana nywele zake zikiwa wazi.

Mada zinazofanana:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid