Je, waasi nchini Syria ni akina nani?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Vikosi vya waasi vimeanzisha mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya serikali ya Syria katika miaka mingi iliyopita.

Kwa muda wa wiki moja wameudhibiti mji wa pili kwa ukubwa nchini humo Aleppo, mji wa Hama na walikuwa wakikusanyika nje ya mji mkuu wa Homs kusini zaidi.

Kusini mwa Syria karibu na mpaka wa Jordan, waasi wa eneo hilo wameripotiwa kuteka sehemu kubwa ya eneo la Deraa, mahali yalipotokea maasi ya mwaka 2011 dhidi ya Rais Bashar al-Assad.

Mashambulizi ya kushtukiza kaskazini yalikutana na upinzani mdogo kutoka kwa jeshi la Syria, ambalo liliwaondoa wanajeshi wake kutoka Aleppo, na pia kutoka Hama na maeneo mengine.

Shambulio hilo liliongozwa na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) ambalo lina historia ndefu inayohusika katika mzozo wa Syria.

HTS limetangazwa kama shirika la kigaidi na Umaja wa Mataifa , Marekani, Uturuki na nchi nyingine.

Unaweza pia kusoma:

Hayat Tahrir al-Sham ni akina nani?

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, HTS imeongoza mashtaka hadi Aleppo

HTS lilianzishwa chini ya jina tofauti, Jabhat al-Nusra , mwaka wa 2011 kama mshirika wa moja kwa moja wa Al Qaeda.

Kiongozi wa kundi linalojiita Islamic State (IS), Abu Bakr al-Baghdadi , pia alihusika katika uundaji wake.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

lilionekana kuwa mojawapo ya makundi yenye ufanisi zaidi.

Lakini itikadi yake ya kijihadi ilionekana kuwa nguvu yake ya uendeshaji wake badala ya bidii ya mapinduzi - na ilionekana wakati huo kama haikubaliani na muungano mkuu wa waasi chini ya bendera ya Free Syria.

Na mnamo 2016, kiongozi wa kikundi hicho, Abu Mohammed al-Jawlani, alivunja hadharani uhusiano na Al Qaeda, akaifuta Jabhat al-Nusra na kuanzisha shirika jipya , ambalo lilichukua jina la Hayat Tahrir al-Sham lilipounganishwa na vikundi vingine kadhaa vyenye itikadi sawa mwaka mmoja baadaye.

Kwa muda sasa, HTS imeanzisha kituo chake cha mamlaka katika jimbo la kaskazini-magharibi la Idlib, ingawa jitihada zake za kupata uhalali zimetiwa doa na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Pia limehusika katika mapigano makali na vikundi vingine.

Matarajio yake zaidi ya Idlib hayakuwa wazi.

Tangu lilipojitenga na Al Qaeda, lengo lake limekuwa tu kujaribu kuanzisha utawala wa Kiislamu wa kimsingi nchini Syria.

Lilikuwa limeonyesha dalili ndogo ya kujaribu kurejesha mzozo wa Syria kwa kiwango kikubwa na kuweka upya changamoto yake kwa utawala wa Assadkatika sehemu kubwa ya nchi, hadi sasa.

g
Maelezo ya picha, Nani anaidhibiti Syria?

Kwa nini kuna vita Syria?

Mnamo Machi 2011, maandamano ya kuunga mkono demokrasia yalizuka katika mji wa kusini wa Deraa, yakichochewa na maasi katika nchi jirani dhidi ya watawala wakandamizaji.

Wakati serikali ya Syria ilipotumia nguvu kubwa kuwaangamiza wapinzani, maandamano ya kumtaka rais huyo ajiuzulu yalizuka nchi nzima.

Machafuko yakaenea na ukandamizaji ukazidi. Wafuasi wa upinzani walichukua silaha, kwanza kujilinda na baadaye kuondoa vikosi vya usalama katika maeneo yao. Bw Assad aliapa kuponda kile alichokiita "ugaidi unaoungwa mkono na wageni".

Mamia ya makundi ya waasi yaliibuka, mataifa yenye nguvu ya kigeni yakaanza kuchukua upande na mashirika ya wanajihadi wenye itikadi kali kama vile kundi la Islamic State (IS) na al-Qaeda, yalihusika.

Ghasia hizo ziliongezeka kwa kasi na nchi ikaingia katika vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe katika mataifa yenye nguvu za kikanda na dunia.

Zaidi ya watu nusu milioni wameuawa na milioni 12 wamelazimika kukimbia makazi yao, takriban milioni tano kati yao ni wakimbizi au wanaotafuta hifadhi nje ya nchi.

Shambulio la waasi lilitokeaje?

Vita nchini Syria kwa miaka minne iliyopita vilionekana kana kwamba vimekwisha.

Utawala wa Rais Bashar al-Assad kimsingi ulikuwa haujapingwa katika miji mikubwa ya nchi, wakati baadhi ya maeneo mengine ya Syria yalisalia nje ya udhibiti wake wa moja kwa moja.

Hii ni pamoja na maeneo mengi ya Wakurdi mashariki, ambayo yamekuwa tofauti zaidi au kidogo na udhibiti wa serikali ya Syria tangu miaka ya mwanzo ya mzozo.

Kulikuwa na baadhi ya machafuko yaliyoendelea, ingawa yalikuwa kimya, kusini ambapo mapinduzi dhidi ya utawala wa Assad yalianza mwaka 2011.

Katika jangwa kubwa la Syria, watu wanaoshikilia kutoka kwa kundi linalojiita Islamic State bado ni tishio la usalama, haswa wakati wa msimu wa uwindaji wa truffle wakati watu wanaelekea katika eneo hilo kutafuta kitamu cha faida kubwa.

Na kaskazini-magharibi, jimbo la Idlib limekuwa likishikiliwa na makundi ya wapiganaji wanaofukuzwa huko katika kilele cha vita.

HTS, kikosi kikuu cha Idlib, ndicho ambacho kimeanzisha mashambulizi ya kushtukiza huko Aleppo.

Kwa miaka kadhaa, Idlib ilibaki uwanja wa vita huku vikosi vya serikali ya Syria vikijaribu kupata udhibiti tena.

Lakini makubaliano ya kusitisha mapigano mwaka 2020 yaliyosimamiwa na Urusi , ambayo kwa muda mrefu imekuwa mshirika mkuu wa Assad, na Uturuki, ambayo inawaunga mkono waasi, imeshikilia kwa kiasi kikubwa.

Takriban watu milioni nne wanaishi huko - wengi wao wakiwa wamekimbia miji na miji ambayo vikosi vya Assad vilishinda kutoka kwa waasi katika vita vya kikatili vya uasi.

Aleppo ilikuwa moja ya uwanja wa vita uliojaa umwagaji damu zaidi na iliwakilisha moja ya kushindwa kubwa zaidi kwa waasi.

Ili kupata ushindi, Rais Assad hakuweza kutegemea jeshi la nchi hiyo lisilo na vifaa vya kutosha na lisilo na ari nzuri pekee, ambalo hivi karibuni lilijiweka hatarini na kushindwa kushikilia nyadhifa mara kwa mara dhidi ya mashambulizi ya waasi.

Badala yake, alikuja kutegemea sana nguvu ya anga ya Urusi na usaidizi wa kijeshi wa Irani ardhini - haswa kupitia wanamgambo waliofadhiliwa na Tehran, ikiwa ni ni pamoja na Hezbollah.

Kuna shaka kidogo kwamba kushindwa kwa Hezbullah hivi karibuni kutokana na mashambulizi ya Israel huko Lebanon , pamoja na mashambulizi ya Israel dhidi ya makamanda wa kijeshi wa Iran nchini Syria, kumekuwa na sehemu kubwa katika uamuzi wa jmakundi ya jihadi na makundi ya waasi huko Idlib kushambuliia ghafla, bila kutarajiwa na kuendelea hadi Aleppo.

Katika miezi michache iliyopita, Israel imezidisha mashambulizi yake dhidi ya makundi yenye uhusiano na Iran pamoja na mifumo yao ya usambazaji bidhaa, na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye mitandao ambayo imewafanya wanamgambo hao wakiwemo Hezbollah kufanya kazi nchini Syria.

Bila wao, vikosi vya Rais Assad vimeachwa bila usaidizi.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi