Hakimiliki ya kitabu cha Hitler yamalizika

Mein Kampf

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Hakimiliki za kitabu cha Mein Kampf zimekuwa zikishikiliwa na jimbo la Bavaria

Kitabu kilichoandikwa na kiongozi wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler kitaanza kuuzwa tena baada ya hakimiliki za kitabu hicho kufikia kikomo.

Kitabu hicho kwa jina Mein Kampf kilipigwa marufuku baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na serikali ya Bavaria, ambayo ilimiliki haki za kitabu hicho.

Hii ina maana kwamba hakuna yeyote ambaye angeweza kuchapisha au kusambaza kitabu hicho kwa miaka 70.

Kwa mujibu wa Sheria Ujerumani, hakimiliki hudumu kwa miaka 70.

  • <link type="page"><caption> Kitabu cha Adolf Hitler kuchapishwa tena</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/12/151202_adolf_hitlers_book_republished" platform="highweb"/></link>

Sasa hakimiliki ya kitabu hicho imefikia kikomo na Taasisi ya Historia ya Kisasa (IfZ) mjini Munich imesema itaanza kuuza nakala za kitabu hicho wiki ijayo.

Nakala za kitabu hicho kinachoangazia sera aliyoifuata Hitler kilikuwa mwongozo wa utawala wa Nazi.

Nakala

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Nakala za kitabu hicho zitakazotolewa zitakuwa na ufafanuzi

Hatua ya kuchapisha upya kitabu hicho imepingwa na makundi ya Wayahudi, yanayodai kazi za Sanaa za Nazi hazifai kuendelezwa.

Lakini wanahistoria wanasema kitabu hicho Mein Kampf (Mapambano au Mapigano yangu) kitasaidia wasomi kufahamu yaliyotendeka wakati wa uongozi wa Nazi.

Mein Kampf kilichapishwa mara ya kwanza 1925, miaka minane kabla ya Hitler kuingia mamlakani.

Majeshi ya muungano yaliyoshinda vita dhidi ya Ujerumani 1945 yalikabidhi hakimiliki ya kitabu hicho kwa jimbo la Bavaria.