Tazama: Meli ya kivita ya Thailand ilivyozama
Jeshi la wanamaji linahangaika kutafuta manusura baada ya HTMAS Sukhothai iliyokuwa na wafanyakazi 106 kuzama ilipokumbwa na dhoruba.
HTMAS Sukhothai ilizama baada ya maji kusomba mitambo yake ya umeme siku ya Jumapili
Kufikia leo Jumatatu mamlaka zinasema zimefanikiwa kuwaokoa wafanyakazi 75 lakini 31 hawajapatikama
"Ni zaidi ya saa 12 lakini tutaendelea kutafuta manusura," msemaji wa jeshi la wanamaji aliambia BBC.
Vikosi vya uokoaji vilifanya kazi usiku kucha kutafuta manusura, huku operesheni ikiendelea Jumatatu kwa usaidizi wa jeshi la anga.









