Beyoncé atangaza albamu yake ya Renaissance baada ya miaka sita

Beyoncé ametangaza kile kinachoonekana kuwa albamu yake ya kwanza katika kipindi cha miaka sita, Renaissance, ambayo itatolewa Julai 29.
Itafuatia albamu ya Lemonade ya mwaka 2016, kutafakari kuhusu utambulisho wa watu weusi na uzinifu wa ndoa ambao uliongoza orodha mwisho wa mwaka.
Mashabikiwamekuwa wakisubiri taarifa hizo tangu Beyoncé alipofuta picha zake za wasifu kwenye mitandao yake kijamii wiki iliyopita.
Aliwatoa mashaka Alhamisi asubuhi, kwa kushirikisha neno "act i … RENAISSANCE" katika akaunti zake.
Mitandao yamuziki ya Spotify na Apple Music ziliposti kazi zake za sanaa skwa ajili ya rekodi, kuwapa mashabiki wake nafasi ya kuhifadhi mapema toleo hilo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Tidal, kampuni inayomilikiwa na mume wake Jay-Z, pia ilitoa taarifa lakini haitaiangazia kama albamu ya kipekee.
Lemonade, ilitambulishwa na Tidal pekee kwa miaka mitatu. Albamu ya pamoja ya Beyoncé na Jay-Z, Everything Is Love, ilikuwa ya kipekee kwa siku mbili tu katika 2018
Sasa uhusiano huo umekatishwa, utambuzi kwamba huduma ya utiririshaji - ambayo ina takriban hisa 2% ya soko - haiwezi kufikia ufuasi mkubwa ambao Beyoncé anahitaji kutawala chati.
Orodha kwenye Apple Music inaashiria kuwa albamu ya Renaissance itakuwa na nyimbo 16. Haijabainika ikiwa mada "Act i" inamaanisha huu utakuwa wa mwanzo wa mradi wa albamu nyingi, au kama nyimbo 16 zitatolewa katika sehemu nyingi.
Wakfu wa msaada wa Beyoncé BeyGOOD, uliwafichulia mashabikiwatarajie kitu kipya mapema wiki hii, iliposhiriki msururu wa majalada ya albamu kusherehekea Mwezi wa Historia ya Weusi nchini Marekani.
Kilichokuwa kimefichwa miongoni mwa rekodi hizo ni picha ya mkono wenye glavu ukielekeza kwenye albamu ya Brandy B7 - rekodi ya hivi punde zaidi ya Beyoncé ilitolewa na wafuasi wake.
Mwaka jana,msanii huyo mwenye umri wa miak 40-alithibitishia duka la Harper Bazaar kwamba ameanza kushughulikia muziki mpya. "Pamoja na hali ngumu tulizoshuhudia kutokana na kutengwa na ukosefu wa haki mwaka uliopita, nadhani sote tuko tayari kutoroka, kusafiri, kupenda na kucheka tena," alisema.
"Ninahisi ufufuo unakuja, na ninataka kuwa sehemu ya kukuza ufufuo huo kwa njia yoyote iwezekanavyo. Nimekuwa studio kwa mwaka mmoja na nusu."
Pia alizungumzia tabia yake ya kushirikiana na makumi ya watu kuandaa nyimbo; kuboresha na kutengeza muziki unamgusa yeye binafsi.
"Wakati mwingine inachukua mwaka mmoja kwangu kutafuta maelfu ya sauti ili kupata ubora wa hali ya juu. Kwaya moja inaweza kuwa na hadi sauti 200 zilizorundikwa pamoja," alisema.
"Mpaka sasa, hakuna kitu kunafikia upendo, shauku, na uponyaji ambao ninahisi katika studio ya kurekodi. Baada ya miaka 31, inahisi kusisimka kama nilivyokuwa wakati nilikuwa na umri wa miaka tisa. Naam, muziki unakuja!"

Chanzo cha picha, Getty Images
Nyota huyo alizindua taaluma yake ya muziki alipokuwa sehemu ya kikundi cha wasichana cha R&B kwa jina Destiny's Child mnamo 1997, kabla ya kuamua kuimba peke ya mwaka wa 2003. Akiwa na vibao kama vile Crazy In Love, Single Ladies na Hold Up, yeye ni mmoja wa wasanii waliofanikiwa na wenye ushawishi mkubwa wa kurekodi wa kizazi chake. .
Katika kipindi cha kazi yake ameshinda tuzo 28 za Grammy na teuzi 79, zaidi ya mwanamuziki mwingine yeyote wa kike.
Katika kipindi cha miaka sita tangu atoe albamu yake ya mwisho, ameunda soundtrack ya Lion King chini ya imamizi wa Disney na kutumbuiza katika tamasha la kihistoria la Coachella mwaka 2018, ambalo liliadhimisha utamaduni wa taasisi na vyuo vikuu vinavyohusishwa kihistoria na watu weusi nchini Marekani.
Tamasha hilo liliangaziwa katika toleo maalum la Netflix, Homecoming, ambayo pia ilishinda tuzo ya Grammy ya filamu bora ya muziki.
Toleo lake la hivi majuzi la muziki lilikuwa lile la kibao, Black Parade, ambalo lilitoka mnamo 2020 wakati wa maandamano ya Black Lives Matter yaliyoeneo kote duniani.
Wimbo huo ulijumuisha mashairi kuhusu historia ya watu weusi, ukatili wa polisi na maandamano ya George Floyd, huku nyota huyo akiimba: "Weka ngumi hewani, onyesha upendo mweusi / Ninahitaji amani na fidia kwa watu wangu."
Wimbo huo ulitolewa mnamo Juni kumi na moja, wakati wa likizo ya kuadhimisha mwisho rasmi wa utumwa nchini Marekani.













