Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Kaliningrad, eneo la Urusi ndani ya Ulaya ambalo sasa litazungukwa na nchi za NATO
Kufuatia uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine, nchi mbili za nchi za Skandinavia yaani Nordic zisizoegemea upande wowote, Finland na Sweden, zilibadili sera zao na kuomba kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO.
Kwa baadhi ya wachambuzi, uamuzi wa Finland na Uswidi ni "janga" kwa Moscow, ambalo mara zote imeona upanuzi wa muungano kama tishio la usalama.
Lakini Rais wa Urusi Vladimir Putin aliwashangaza wengi mwezi uliopita wa Mei aliposema kuwa suala hilo halina tatizo lolote ilimradi wanachama wapya wa NATO wajiepushe na kuhifadhi miundombinu ya kijeshi, hasa silaha za nyuklia, kwenye ardhi yao.
Kilicho wazi ni kwamba ramani ya kijiografia ya eneo hilo itaonekana tofauti kabisa wakati Finland na Uswidi zitajiunga na NATO.
"Bahari ya Baltic itakuwa ziwa la NATO," Andrey Kortunov, mkuu wa Baraza la Urusi la Masuala ya Kimataifa, Jopo la ushauri huko Moscow ambayo ina uhusiano na Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, alitangaza hivi karibuni.
Kwa hakika, pamoja na Uswidi na Finland kuwa wanachama wa NATO, Urusi itahifadhi baadhi ya kilomita 200 za ufuo wa Baltic.
Na 90% iliyobaki ya kilomita 8,000 za ukanda wa pwani zitashirikiwa na nchi za muungano: Estonia, Latvia, Lithuania, Poland, Ujerumani, Denmark, Uswidi na Finland.
Lakini huko, iliyoshikana kati ya Poland na Lithuania, ni Kaliningrad, eneo la utawala la Urusi ambalo halishiriki mipaka ya ardhi nayo.
Maeneo haya ya Kirusi, yenye wakazi chini ya milioni moja, yamekuwa hatua ya kimkakati ya mgawanyiko unaozidi kati ya Magharibi na Urusi.
Na baadhi ya wachambuzi wanadai kwamba eneo hili dogo ni muhimu kwa mashambulizi ya Moscow dhidi ya Ukraine na kwa ajili ya kulinda ulinzi wake dhidi ya uhasama wowote kutoka nchi za NATO.
Na kumekuwa na ripoti kwamba Urusi tayari imepeleka silaha za nyuklia katika eneo hilo
Kutoka Koenigsberg hadi Kaliningrad
Kaliningrad ni mojawapo ya majimbo 46 ambayo Urusi inayo kwa sasa, lakini ndiyo pekee ambayo haina mpaka wa ardhi na nchi hiyo.
Mbali na umuhimu wake wa kimkakati na kijeshi, Kaliningrad ina umuhimu mkubwa wa kihistoria kwa Ulaya na Urusi.
Mizizi ya eneo hilo inarudi nyuma sana katika historia na inahusishwa kwa karibu na hatima ya Prussia Mashariki na mji mkuu wake, Köenigsberg.
Königsberg ya kale ilianzishwa na Teutonic Knights mwaka wa 1255, mpiganiaji wa Kanisa Katoliki aliyezaliwa Ujerumani ambaye alitawala Prussia.
Prussia Mashariki ilipojitenga na Ujerumani baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, eneo hilo lilibaki kuwa sehemu ya Ujerumani hadi mapema mwaka 1945, mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, wakati lilishindwa na Jeshi Jekundu la Usovieti.
Kisha, katika Mkutano wa Yalta, mgawanyiko wake kati ya Poland na Umoja wa Kisovieti ulikubaliwa, ambao ulirasimishwa huko Potsdam mnamo mwaka 1945. Jina lake la Kirusi linatokana na Mikhail Kalinin, mmoja wa washiriki wakuu wa harakati ya ukomunisti wa Bolshevik na mkuu rasmi wa Umoja wa Usovieti kati ya 1922 na 1946.
Kati ya Urusi na nchi za Magharibi
Kaliningrad ina bandari pekee kwenye Bahari ya Baltic ambayo haina barafu mwaka mzima.
Ndiyo maana jiji la bandari ni muhimu kwa Urusi na Mataifa ya Baltic kuhakikisha usafiri na biashara katika eneo lote, ambapo halijoto huwa chini ya sifuri kwa muda mrefu wa majira ya baridi.
Lakini mbali na usafiri na biashara, Kaliningrad ni eneo muhimu kimkakati kwa Urusi kutokana na msimamo wake kwenye Bahari ya Baltic na ukaribu wake na NATO.
Ni nyumba ya Meli ya Baltic ya Urusi na iko katika nafasi nzuri kama eneo la magharibi zaidi la Moscow, karibu na kitovu cha Uropa.
Mnamo Mei, Meli ya Baltic ilitangaza kwamba ilifanya mfululizo wa mashambulio ya makombora kutoka kwa mfumo wake wa nyuklia wa Iskander.
Mfumo wa makombora wa Iskander ulianzishwa kwa mara ya kwanza katika eneo hilo mwaka wa 2016 na kisha kuboreshwa mwaka wa 2018, kama sehemu ya mkakati wa Urusi kukabiliana na kutumwa kwa NATO kwa ngao ya ulinzi wa makombora ya balestiki barani Ulaya.
Pia kumekuwa na mazoezi ya kijeshi ya mara kwa mara yanayohusisha Meli ya Baltic na mfululizo wa michezo ya kivita tangu uvamizi wa Ukraine.
"Kaliningrad imekuwa kitovu cha wasiwasi wa usalama wa Urusi tangu wimbi la kwanza la upanuzi wa NATO lilipotangazwa katika miaka ya 1990," Ruth Deyermond, profesa wa Usalama wa Baada ya Soviet katika Idara ya Mafunzo ya Sayansi, anaiambia BBC Mundo.
"Bila shaka, katika nyakati ambapo mvutano kati ya Urusi na NATO unaongezeka, hali kadhalika na wasiwasi kuhusu Kaliningrad," anaongeza.
Kaliningrad ilikuwa tayari imejaa kijeshi kwa miaka mingi, lakini hali hii ya kijeshi iliimarishwa baada ya kuingizwa kwa Urusi kutwaa eneo la Crimea mwaka wa 2014. Na mahusiano zaidi kati ya Urusi na Magharibi yakawa baridi, uwepo wa kijeshi wa pande zote mbili katika kanda unaimarishwa.
"Haishangazi kwamba eneo hili, ambalo labda ni sehemu ya Ulaya yenye mkusanyiko mkubwa wa vikosi vya Urusi na NATO kwa ukaribu sana, sasa ndio kitovu cha wasiwasi mkubwa wa usalama kwa pande zote mbili," Profesa. Deyermond alisema.
Urusi haikanushi, lakini haikubali, kwamba imepeleka silaha za nyuklia huko Kaliningrad na mara nyingi imetumia lugha isiyoeleweka kuhusu tuhuma hizo.
"Kutumwa kwa silaha moja au nyingine, kupelekwa kwa vitengo vya kijeshi, na kadhalika katika eneo la Urusi, ni suala la pekee la Shirikisho la Urusi," msemaji wa Kremlin Dimitry Peskov alisema mwaka wa 2018.
Lakini baadhi ya maafisa wa juu, kama vile rais wa Lithuania, wanasema Moscow tayari imepeleka silaha za nyuklia katika eneo la kimkakati la Baltic.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanaamini kwamba iwapo NATO ingeingilia kati mzozo unaoendelea wa Ukraine, au ikiwa Moscow italenga Jamhuri nyingine za zamani za Usovieti kama Lithuania, Kaliningrad inaweza kuwa njia ya kuanzisha mashambulizi ya Urusi katika nchi hizo.
Lakini Stefan Wolff, profesa wa usalama wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza, hafikirii kuwa hiyo ni hali inayowezekana hivi sasa.
"Sina hisia kwamba Urusi inazingatia kwa dhati ongezeko hilo au kwamba ina rasilimali za kufanya hivyo kwa wakati huu," mtaalam huyo aliambia BBC Mundo.
"Hata hivyo, ni uwezekano wa muda mrefu. Kwa hiyo, itakuwa muhimu kuimarisha uwezo wa ulinzi wa NATO sasa ili kuzuia hatua zozote za Urusi katika siku zijazo."
Wataalamu wanakubali kwamba mara tu Uswidi na Finland zikijiunga na muungano huo, huenda Urusi ikaimarisha jeshi lake huko Kaliningrad.
Lakini hii, anasema mtaalam wa Chuo cha Kings Ruth Deyermond, "labda inapaswa kueleweka zaidi kama kitu cha kujihami: Urusi itakuwa inalinda eneo lake kutoka kwa NATO, badala ya kuwa mtangulizi wa kushambulia Poland au mataifa ya Baltic."
"Haijulikani ni muda gani mchakato wa uidhinishaji wa kujumuishwa kwa Uswidi na Finland katika NATO unaweza kuchukua.
Jambo la kawaida ni angalau mwaka mmoja, lakini imesemekana kuwa katika hili, baadhi ya wanachama, kama vile Marekani, wanaweza kushinikiza kuharakisha mchakato huo.
Wakati huo huo, wataalam wanaamini kwamba eneo hili lenye wanajeshi wengi linaweza kuwa sehemu muhimu ya mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine.
"Sio muhimu bado, lakini inaweza kuwa muhimu zaidi ikiwa kutakuwa na kuongezeka kati ya Urusi na NATO au ikiwa Urusi itazindua shughuli za uondoaji utulivu katika mataifa ya Baltic au Poland," anasema Stefan Wolff.
Kwa Ruth Deyermond hatari kubwa zaidi si uvamizi wa kimakusudi au matumizi ya makusudi ya silaha za nyuklia.
"Hatari kubwa zaidi katika Baltic ni hesabu mbaya au kutoelewana kunakosababisha ongezeko ambalo hakuna mtu alitaka," mtaalam wa Chuo cha Kings College.
"Eneo ni ndogo, ardhi haitoi vikwazo muhimu vya asili, na kuna wanajeshi wengi wanaokaribiana sana. Hiyo inatoa picha nzuri ya hali kutoweza kudhibitika."
Lakini mradi wahusika wote wanafahamu uwezekano huu, na nadhani wanafahamu, hatari hiyo inaweza kudhibitiwa," anasema mtaalam huyo.
Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine