Vita vya Ukraine: Ukraine inaweza kupata mfumo wa roketi wa masafa marefu kutoka Marekani

Serikali ya Marekani inaonekana kukaribia kutuma mfumo wa roketi nyingi wa masafa marefu (MLRS) kwa Ukraine.

Urusi inaona uwasilishaji kama huo wa silaha nzito kama kuongezeka kwa uchochezi.

Rais Volodymyr Zelensky na maafisa wengine wa Ukraine wamehimiza kuwasilishwa kwa MLRS ili kukabiliana na mashambulizi makubwa ya Urusi katika eneo la mashariki la Donbas.

Urusi inaendelea kushambulia Severodonetsk na maeneo mengine ya Donbas kwa roketi, vifaru na mashambulizi ya anga.

Vikosi vya Kyiv tayari vinatumia ndege aina ya M777 zilizowasilishwa na Marekani, ambazo zina umbali wa kilomita 25 (maili 16). Lakini MLRS ingeruhusu Ukraine kufikia malengo yaliyo mbali zaidi ya hapo.

M270 MLRS inaweza kurusha aina mbalimbali za silaha, ikiwa na ya hali ya juu zaidi inayoweza kulenga shabaha ya umbali wa kilomita 300 (maili 186). Hatahivyo, inaweza pia kurusha makombora ya masafa mafupi na anuwai ya karibu 70km (maili 43).

Kuiwekea kikomo Ukraine kwa roketi ndogo kunaweza kuwa njia kwa Marekani kuepuka kuzidisha mzozo huo, huku bado ikiboresha kwa kiasi kikubwa safu ya silaha ya Ukraine.

Afisa mkuu wa Marekani aliyenukuliwa na gazeti la Washington Post alisema Ikulu ya Marekani iliridhika na kuipa Ukraine MLRS, lakini itazuia silaha ndefu zaidi zinazoendana na mfumo huo.

Kuna wasiwasi kwamba Ukraine inaweza kutumia mfumo huo kufikia malengo ndani ya Urusi, na hatua kama hiyo itahatarisha kuivuta Marekani na washirika wake wa Nato kwenye mzozo wa moja kwa moja na Moscow.

Uingereza pia ina MLRS. Waziri Mkuu Boris Johnson alisema Ukraine inapaswa kupata roketi "ili kujilinda dhidi ya ufyatuaji huo wa kikatili wa Urusi", lakini hakusema kwamba Uingereza itawapatia.

Marekani ilitumia MLRS kuharibu shabaha kuu za Iraq katika Vita vya Ghuba vya 1990-91 na 2003.

Urusi inaona 'vita vya wakala'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amezishutumu nchi za Magharibi kwa "kuwapatia raia wa Ukraine silaha".

Alisema nchi za Magharibi "zinaendesha vita vya wakala" dhidi ya Urusi ambayo, alionya, itamaanisha "kuongezeka kwa mzozo kusikoepukika".

Wiki iliyopita, mtangazaji katika runinga ya serikali ya Urusi alisema kuwa Marekani itakuwa ikivuka "mstari mwekundu" kwa kusambaza MLRS kwa Ukraine, na ingeonekana kama jaribio la "kuchochea jibu kali kutoka kwa Urusi".

Katika hatua ya ziada ya kutetea bandari kuu ya Bahari Nyeusi ya Ukraine - Odesa - Denmark imesambaza makombora ya kukinga meli ya Harpoon, yenye masafa ya takriban kilomita 130 (maili 70 za baharini).

Ukraine inaweza kuyatumia pamoja na makombora yake ya Neptune, ambayo yanasifiwa kwa kuzamisha meli kuu ya Urusi ya Moskva mwezi uliopita.

Makombora ya masafa marefu ya Urusi yameshambulia vituo vya reli, bohari za mafuta na miundombinu mingine magharibi mwa Ukraine - ambayo inaonekana kama juhudi za kuzuia uwasilishaji wa silaha za Magharibi.

Wakati huo huo, Urusi inaripotiwa kurusha mfumo wake wa hivi punde wa roketi nyingi dhidi ya maeneo muhimu ya Ukraine katika eneo la Kharkiv - silaha inayoelezewa kama giant flamethrower Utumiaji wake uliripotiwa na shirika la habari la Tass, likimnukuu afisa wa usalama wa Urusi.

TOS-2 Tosochka ni silaha ya hewa ya mafuta ya thermobaric: inaleta mlipuko mkubwa kwa kutoa wingu la gesi j na kumnyima mtu yeyote aliye katika eneo la oksijeni.

Urusi pia imesababisha uharibifu mkubwa kwa miji ya Ukraine kwa kutumia makombora ya masafa marefu, mengine yakirushwa kutoka kwenye meli za kivita.