Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Madai ya mashambulizi ya kemikali ya Urusi yathibitishwa
Urusi inaonekana kufuata mkakati wa zamani wa kubishana kuwa wapinzani wake hawakushambulia.
Hivi majuzi Urusi imevishutumu vikosi vya Ukraine kwa kushambulia vituo vya kuhifadhia mbolea nchini mwao.
Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya saa sita mchana mbele ya umati wa waandamanaji, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi.
Inadaiwa kuwa balozi huyo ndiye aliyetoa taarifa hizo.
Hata hivyo, hakuna ushahidi kwamba mojawapo ya madai haya ni ya kweli.
Urusi ina historia ya kuwashutumu wapinzani wake kwa uwongo kwa kufanya ''uchochezi'' ambao haujawahi kutokea kabisa, au ulifanywa na wao wenyewe au washirika wao..
Moscow ilisema nini?
Katika taarifa fupi iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi mnamo Mei 11, alisema, ''Vikosi vya Ukraine vimelipua meli ya mafuta iliyokuwa na mbolea. Huenda ikawa na nitrati ya ammonia yaani 'ammonia nitrate'.
Hii ilisababisha mawingu makubwa ya moshi kutokea hapo.
Kulingana na Moscow, lengo la mlipuko huo uliotokea katika eneo la Kharkiv lilikuwa ni kuishutumu Urusi kwa kutumia silaha za kemikali ili ''kuchomoa msaada wa ziada wa kijeshi kutoka Magharibi na utawala wa Kyiv''.
Hakuna ushahidi uliotolewa kuunga mkono madai kwamba vikosi vya Ukraine vilihusika na mlipuko huo.
Ni nini hasa kilitokea?
Kwa kutumia picha ya setilaiti ya eneo hilo, kwenye video inayoonyesha moshi wa rangi ya chungwa ukitoka angani, iligeuka kuwa shamba katika eneo la Dolgenkoye karibu na jiji la Kharkiv.
Vyombo vya habari vya Ukraine viliripoti kulingana na ripoti katika Telegram kwamba mawingu ya moshi yametokea baada ya ndege isiyo na rubani ya Urusi kugongana na kitu.
Oleksi Arrestovich, mshauri wa mkuu wa rais wa Ukraine baada ya mlipuko huo, alisema haamini kuwa ni shambulio la silaha za kemikali za Urusi.
BBC haijapata ushahidi wowote kuwa mamlaka ya Ukraine imeishutumu Urusi kwa kutumia silaha za kemikali baada ya tukio hilo.
Picha za video na satelaiti zinazoonyesha majengo ya shamba lililoathiriwa zinaendana na mlipuko ambapo vifaa vyenye nitrati ya ammoniamu vimechomwa moto - na kutoa wingu la rangi ya chungwa, anasema Wim Zwijnenburg, mtafiti wa silaha katika Pax, shirika la kibinadamu la Uholanzi.
Bw Zwijnenburg anasema hadi vituo 40 vya kilimo vinavyofanana vimeharibiwa nchini Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mwezi Februari.
Katika wiki za hivi karibuni, Dolgenkoye amekuwa akilengwa kwa makombora kutoka kwa vikosi vya Urusi, huku picha za satelaiti zikionyesha maeneo mbalimbali ya eneo hilo yakiwa na makovu ya makombora.
Madai ya Urusi ya uwongo
Operesheni Z, chaneli ya mitandao ya kijamii inayounga mkono Urusi iliyo na watumiaji karibu 800,000 hivi karibuni ilidai kuwa madaktari nchini Ukraine walikuwa wameagizwa kupeleka miili ya wanawake na watoto hospitalini, kutoka ambapo ingesafirishwa hadi ''moja ya vituo vya kijamii nchini humo, mji ambapo shambulio la anga linalodaiwa kufanywa na anga la Urusi litaigwa.''
Telegram post mnamo tarehe 12 Mei ilisema: ''Huduma maalum ya Ukraine inatayarisha uchochezi katika eneo la Dnieper (Dnipro) kushutumu jeshi la Urusi kwa kuua raia.''
Hakuna ushahidi wa simulizi hii, ambayo inafuata madai mengine sawa na vyombo vya habari vinavyounga mkono Urusi.
Mapema mwezi Aprili, wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema maafisa wa ujasusi wa Uingereza walikuwa wakiweka miili ya raia katika vyumba vya chini ya ardhi katika eneo la Sumy, ambao wanaweza kuonyeshwa kwa nchi za Magharibi kama waathiriwa wa ''mauaji ya Urusi''.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kuunga mkono madai hayo yaliyotolewa na vyombo vya habari vinavyounga mkono Urusi.
Urusi ina historia ya kuwashutumu maadui zake kwa kufanya kile inachokiita ''chokozi'', ambayo ina maana ya mashambulizi ambayo yanaweza kulaumiwa kwa Urusi.
Katika baadhi ya matukio, madai ni kufidia mashambulizi yaliyofanywa na Urusi au washirika wake
kwa wengine madai yanarejelea matukio yajayo ambayo yanaweza yasitokee kabisa.
Wakati wa mzozo wa Syria, Moscow mara kwa mara ilishutumu kundi la ulinzi la raia la White Helmet, Uingereza, Marekani, Ufaransa na Ubelgiji kwa kuandaa mashambulizi ya kemikali ambayo wanaweza kulaumu Urusi na Syria.
Hata hivyo, uchunguzi kuhusu mashambulizi ya kemikali wakati wa vita umehitimisha kuwa serikali ya Syria ilihusika na mashambulizi ya Douma na Ghouta.
Kabla ya uvamizi wa Ukraine, BBC iliripoti juu ya matukio kadhaa ya bendera ya uongo, ikiwa ni pamoja na madai kwamba gari lililochomwa na risasi lilikuwa ''ushahidi'' wa mashambulizi ya Ukraine dhidi ya raia.
Hata hivyo, ukaguzi wa karibu wa picha za waliojitenga wa Urusi wa tukio hilo ulibaini kuwa miili iliyokuwemo ndani ilikuwa na chale za upasuaji sambamba na kuonyesha mikato iliyowazi ya wazi hivi karibuni kwa uchunguzi wa baada ya maiti, na tayari walikuwa wamefariki wakati wa shambulio hilo linalodaiwa.