Jinsi macho yanavyoweza kuelezea hali yako ya afya

macho ya mwanamke

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha California, San Diego wametengeneza programu ya simu aina ya smartphone ambayo inaweza kutambua dalili za mapema za ugonjwa wa Alzheimer na magonjwa mengine ya mfumo wa neva.

Programu hutumia kamera ya karibu ya infrared ya simu ya mkononi kufuatilia mabadiliko katika ukubwa wa jicho la binadamu kwa ukaribu.

Teknolojia inapoendelea kukua, macho yanaweza kuwa muhimu zaidi kama njia ya kutambua aina zote za magonjwa na hali ya afya kwa ujumla. Kwasababu ya uwezi wake macho yanahitaji mbinu za uchunguzi zisizovamizi zaidi kuliko sehemu nyingine za mwili.

Lakini hata bila teknolojia, wataalamu wanaweza kutambua matatizo ya afya kwa kuangalia mtu machoni tu. Hizi ni baadhi ya dalili za tahadhari.

Ukubwa wa mboni

Mboni ya macho hujibu papo hapo mwanga, na kuwa ndogo katika mazingira angavu na kubwa katika hali ya kawaida.

Mboni

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mboni ya macho huangaza mara inapopata mwanga.

Majibu ya polepole au ya kuchelewa katika ukubwa wa mboni kunaweza kuashiria magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kujumuisha hali mbaya kama vile ugonjwa wa Alzeima, pamoja na madhara ya dawa na ushahidi wa matumizi ya madawa ya kulevya.

Kupanuka kwa mboni ya macho mara nyingi ni hali inayohusishwa na watu wanaotumia dawa za kulevya, kama vile cocaine na nyinginezo. Mboni ndogo sana huuonekana kwa watumiaji wa heroin.

Macho ya mekundu au njano

Kubadilika kwa rangi ya sclera (sehemu "nyeupe ya macho") kunaweza kuashiria kwamba una tatizo la kiafya.

Mabadiliko katika "sehemu nyeupe ya macho" kuwa rangi ya njano inaweza kuwa ishara ya mwasho au maambukizi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mabadiliko katika "sehemu nyeupe ya macho" kuwa rangi ya njano inaweza kuwa ishara ya mwasho au maambukizi.

Ikiwa mabadiliko ya rangi ya macho yataendelea, inaweza kuwa maambukizi makubwa zaidi, kuvimba, au athari kwa lensi za mawasiliano au maji yake.

Jicho jekundu katika hali mbaya zaidi linaweza kuonyesha glaucoma, ugonjwa ambao unaweza kusababisha upofu. Wakati sclera inageuka njano, hii ni kawaida ishara ya wazi ya homa ya manjano au ugonjwa wa ini.

Sababu za msingi za homa ya njano ni tofauti sana. Hii ni pamoja na kuvimba kwa ini (hepatitis), magonjwa ya maumbile au magonjwa yanayotokana na ukosefu wa kinga mwilini, hali inayotokana na matumizi ya dawa fulani, virusi, au uvimbe.

Baka jekundu kwenye jicho

Baka nyekundu kwenye jicho linaweza kusababishwa na utumiaji wa kupindukia wa pombe ama dawa za kulevya. Huenda pia ikasababishwa na mwasho au maambukizi, na mara nyingi baka hilo hutoweka ndani ya siku chache.

Baka hjekundu katika sehemu nyeupe ya macho linatisha na mara nyingi hutokana na kupasuka kwa mshipa mdogo wa damu kwenye jiccho.

Haijabainika ni nini husababisha hali hiyo na baka hilo hutoweka baada ya siku chache.

Hata hivyo wataalamu wanaashiria kuwa huenda unakabiliwa na shinikizo la damu, natatizo la kuganda kwa damu kunakotokana na kutokwa kwa damu nyingi.

Unapojiona na dalili hizo unashauriwa kumtembelea daktari.

Baka nyekundu kwenye jicho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baka nyekundu kwenye jicho inaweza kutokana na kukatika kwa mshipa mdogo wa damu na hutoweka baada ya siku chache.

Pete nyeupe au kijivu karibu na konea mara nyingi huhusishwa na cholesterol ya juu na hatari ya kuongezeka kwa ugonjwa wa moyo.

Inaweza pia kufichua ulevi na wakati mwingine inaonekana machoni pa watu wazee, ndiyo sababu jina la matibabu lililopewa ni arcus senilis.

Donge la mafuta

Wakati mwingine vitu vya kutisha zaidi vinavyoweza kuonekana machoni lakini habari njema ni kwamba rahisi kutibu.

Mujer observando un ojo gigante

Chanzo cha picha, Getty Images

Pinguecula ni uvimbe wa mafuta ya njano ambayo inaweza kuonekana kwenye sehemu nyeupe ya jicho. Ni amana ndogo ya mafuta na protini ambayo inaweza kurekebishwa kwa urahisi na matone ya jicho au kuondolewa kwa operesheni rahisi.

pterygium (inayojulikana the-ri-gion) ni ukuaji wa waridi kwenye sehemu nyeupe ya jicho. Sio hatari ya kuona hadi inapoanza kukua kwenye konea (sehemu ya rangi ya jicho). Kwa bahati nzuri, pterygium inakua polepole sana na, kama pinguecula, inaweza kuondolewa kwa urahisi. Ushauri, lazima uvimbe huo uondolewe mapema kabla haujafikia konea.

Ikiwa uvimbe huo utapuuzwa na kuendelea kukua, pterygium inaweza kuunda "filamu" ya mawingu kwenye konea ambayo itazuia kuona.

Mojawapo ya sababu kuu za pinguecula na pterygium inaaminika kusababishwa na ukukaa kwenye mwanga wa jua kwa muda mrefu.

Macho yanayoonekana kana kamba yamekodolewa huenda ni tatizo la tezi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Macho yanayoonekana kana kamba yamekodolewa huenda ni tatizo la tezi.

Macho ya kuvimba

Muonekano wa kukodoa macho unaweza kuwa sehemu ya hali ya kawaida ya maumbile ya uso.

Lakini wakati macho ambayo hapo awali hayakuwa hivyo yanapoanza kuchomoza mbele, sababu iliyo wazi zaidi inaweza kuwa shida ya tezi na inahitaji matibabu.

Jicho moja linalochomoza linaweza kusababishwa na jeraha, maambukizi au mara chache zaidi uvimbe nyuma ya jicho.

Kuchomoza kwa jicho moja kunaweza kutokana na kujeruhiwa, maambukizi, au hali ambayo sio ya kawaida, ya kuwa na uvimbe nyuma ya jicho.

Uvimbe juu ya kope

Uvimbe juu ya kope pia unaweza kuonesha magonjwa mengi. Hasa zile zinazohusiana na matatizo madogo ya tezi juu ya kope.

Uvimbe huo mara nyingi hutoweka wenyewe ikikandwa kwa uangalifu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uvimbe huo mara nyingi hutoweka wenyewe ikikandwa kwa uangalifu

Hali hiyo kitaalamu inafahamika kama stye au chalazion, ambayo inaonekana kama uvimbe mwekundu kwenye sehemu ya juu na mara chache sana, kope la chini na husababishwa na tezi ya mafuta iliyoziba.

Uvimbe huo ukiendela kwa muda, unapaswa kuondolewa kwa utaratibu rahisi.

Katika hali nyingi haina madhara kabisa na inaweza kuhusishwa na mafadhaiko, usawa wa virutubishi au unywaji mwingi wa kafeini.

Makala hii ni mwongozo tu. Ikiwa una shaka juu ya afya yako, wasiliana na mtaalamu.