Mwai Kibaki: Ratiba ya mazishi ya aliyekuwa rais wa kwanza wa upinzani Kenya imetangazwa

Mwai kibaki

Chanzo cha picha, TORU YAMANAKA/getty images

Maelezo ya picha, Rais Mwai Kibaki
Muda wa kusoma: Dakika 2

Aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki atazikwa kijijini kwake Othaya, Nyeri Jumamosi ya tarehe 30, Aprili.

Mwili wake utakuwa bungeni kati ya Jumatatu tarehe 25 Aprili na Jumatano, Aprili 27.

Ibada ya kitaifa ya kumuaga imepangwa kufanyika katika uwanja wa Nyayo, Nairobi tarehe 29, April.

Rais Kenyatta alitangaza kuwa Mwai Kibaki alifariki usiku wa siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 90.

Kibaki alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya kutoka mwaka 2002 hadi 2013.

Rais Uhuru Kenyatta amesema kiongozi huyo wa zamani wa taifa ataandaliwa mazishi ya kitaifa.

Kenyatta

Uhuru anamuomboleza mtangulizi wake kama kiongozi ambaye alileta ukuaji wa kiuchumi , demokrasia na kuimarisha hali ya uchumi ya Wakenya.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Uhuru anamkumbuka kwa jukumu lake la kupatikana kwa katiba mpya ya mwaka 2010 na kuongoza uidhinishaji wake.

Amesema kwamba bender azote katika majumba ya umma , wizara na balozi zote duniani zitasalia nusu mlingoti hadi pale atakapozikwa.

Rais Mwai kibaki wa Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images

Na kufuatia tangazo la kifo chake viongozi mbali mbali nchini Kenya wameanza kutuma risala za rambirambi kwa famili ya Mwai Kibaki.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema kwamba 'alipata fursa ya kufanya kazi naye kama mbunge akiwa katika upande wa upinzani , kama waziri wa nguvu kazi na barabara katika serikali yake na baadaye kama waziri mkuu katika serikali ya muungano.

TH

Raila Odinga: ''Asubuhi hii tumempoteza rais wa tatu wa Kenya, alikua mmoja wa wapigania uhuru wa nchi hii, ametumikia nchi hii kwa miaka mingi, kwa uwazi na utendaji kazi mzuri. Nilipata nafasi ya kufanya kazi na Mwai Kibaki, kwanza kama mbunge wa upinzani, pia kama mmoja wa mawaziri wake, na baadae kama waziri mkuu.''

Aliyekuwa wakati mmoja waziri wa fedha Musalia Mudavadi alichapisha ujumbe wake maombolezi katika twitter.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Balozi wa Marekani nchini Kenya Eric Kneedler alihuzunishwa na kifo cha ghafla cha rais Mwai Kibaki . Alituma risala za rambirambi kwa jamii, Wakenya na rafiki wa mzee Kibaki wakati huu mgumu.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3