Uhaba wa pesa Algeria: 'Kununua mafuta kunafananishwa na kununua dawa'

Chanzo cha picha, AFP
Bei za vyakula zinapanda kwa kasi nchini Algeria, ambako wanunuzi wanasema kuna uhaba wa mafuta ya kupikia na maziwa kiasi kwamba unahitaji kuwa karibu na wauza duka ili kupata bidhaa hizo.
Kwanza ilikuwa hatua za kushughulikia janga la corona na sasa vita nchini Ukraine vinafanya maisha kuwa magumu kwa watumiaji.
"Inahisi kama kununua dawa," anasema Samiha Sammer, 31, akiwa na na mchanganyiko wa hisia.
Alikuwa akipenda kutengenezea keki familia yake na marafiki zake na hata wakati mwingine kujipatia kipato cha ziada kutokana na kazi hiyo, lakini hawezi tena kupata viungo vyote anavyohitaji.
"Kununua mafuta ya kupikia kutoka doka la treja reja unahitaji kufahamiana na mwenye duka," Bi Sammer anasema.
Ubadilishanaji kawaida hufanyika kwa busara, na bidhaa hiyo adimu na ya thamani imefichwa nyuma ya duka.
Sawa na Waalgeria wengine aligundua mambo yameanza kubadilika mwisho wa mwaka jana, wakati makali ya athari za janga la corona kwa uchumi ilianza kushuhudiwa.
Huku, mfungo wa mwezi wa Ramadhani kwa waumini wa Kiislamu ukitarajiwa kuanza mwishoni mwa juma, Waalgeria wamekuwa wakiongeza juhudi za kupata mafuta ya kupikia kwani ni kiungo muhimu katika vyakula vingi maalum vinavyoliwa katika mwezi huo.
Bi Sammer wakati mwingine anajipata akisafiri mbali kutoka nyumbani kwake mjini Blida hadi mji mdogo wa Kolea, kununua bidhaa ambako bei za mboga ni nafuu kidogo.

Chanzo cha picha, Samiha Sammer
Siku hizi viazi ni ghali zaidi kwa 30% kuliko ilivyokuwa miezi michache iliyopita, na foleni ndefu za maziwa inamaanisha kuwa watu wanaanza kupanga foleni kabla ya jua kuchomoza ili kupata bidhaa hiyo.
"Sasa nimeacha kufanya hivyo kwani siwezi tena kusukumana na umati wa watu na wakati mwingine kupigana ili kupata maziwa," karani wa utawala anasema huku akihema. "Ni hali ya kufedhehesha."
Lakini kujiepusha na umati wa watu kunakuja na gharama za ziada.
Sasa analipa karibu dinar 420 sawa na ($2.90; £2.20) kwa kilo moja ya maziwa ya unga yaliyoagizwa binafsi badala ya dinari 25 kwa aina ya maziwayanayotolewa kupitia ruzuku ya serikali.
Algeriai inakuza maziwa kwa kiwango cha chini, kwa hivyo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitegemea uagizaji wa wa kutoka Ufaransa, nchi zingine za Muungano wa Ulaya na hivi karibuni Umoja wa Falme za Kiarabu-kawaida katika mfumo wa unga ambayo hutiwa maji katika viwanda vya ndani kabla ya kufikia watumiaji.
Kinachowakosesha usingizi Waalgeria ni mafuta ya kupikia.
Sawa na maziwa, bei hudhibitiwa na serikali, lakini hata kabla ya mgogoro wa sasa, mafuta yalikuwa tayari ghali - chupa ya lita tano itagekugharimu angalau dinari 600 ($ 4.20; £ 3.20).

Chanzo cha picha, Getty Images
Ikilinganishwa na wastani wa mishahara ya kila mwezi ya Algeria ya $240 kwa wafanyikazi wa sekta binafsi na $410 kwa wafanyikazi wa sekta ya umma, haishangazi kuwa shinikizo limekuwa likiongezeka kwa mamlaka kuchukua hatua.
Visa vya kuhodhi chakula na rushwa vimeongezeka kutokana na matatizo ya kiuchumi nchini humo, kulingana na ripoti ya uchunguzi wa kamati teule ya bunge.
Mwanachama wa kamati hiyo Hisham Safar aliambia BBC kwamba wafanyabiashara wa mafuta ya kupikia huingiza kwa njia isiyo halali kiasi cha bidhaa za ruzuku wanazouza ili kudai pesa zaidi kutoka kwa serikali.
Mwaka jana, takriban ukiukwaji 150,000 uliripotiwa kwa mamlaka, ambao wengi wao uliishia mahakamani, na maelfu ya vibali vya biashara vilitwaliwa.
Lakini pia kuna tatizo la utoroshwaji wa bidhaa za ruzuku katika mpaka wa kusini wa Algeria ili ziuzwe katika nchi jirani, jambo ambalo tume ya bunge ilieleza kuwa "limeenea".
Hakuna takwimu rasmi lakini vyanzo vimeambia BBC kwamba karibu malori 12 ya mafuta ya kupikiayalisafirishwa kimagendo kutoka Algeria hadi Mali na Niger kila siku.
Wahalifu huuza mafuta ya kupikia yanayofadhiliwa na serikali, yanayotengenezwa Algeria kwa fedha taslimu - wakichukua faida ya hadi $17,800 kwa shehena ya lori, vyanzo viliiambia BBC.
Mapema mwezi huu, Rais Abdelmadjid Tebboune alipiga marufuku usafirishaji wa bidhaa zozote za chakula ambazo zina viambato ambavyo viliagizwa awali - kama vile mafuta ya kupikia, sukari, pasta, semolina na bidhaa nyingine za ngano.
Ripoti inaashiria kuwa rais anataka vitendo kama hivyo viadhibiwe kama "uhujumu uchumi".
Lakini ili kupata sababu za kina za msukosuko wa Algeria lazima uangalie nyuma zaidi, wataalam wanasema.
'Mafia walipora nchi'
Kuegemea kwa uchumi katika uuzaji wa gesi na mafuta ghafi kama injini ya ukuaji na chanzo cha mapato ya serikali kumezua matatizo mengi, kulingana na mwanauchumi Abdal-Rahman Hadef.
Kando na hilo kuna usimamizi mbaya wa sekta hiyo huku mikataba mingi ikifanyika kwenye soko sambamba, ikigharimu hazina kiasi kikubwa cha fedha, Bw Hadef anaongeza.
Pia kuna wasiwasi kwamba matatizo ya kiuchumi yanaweza kusababisha machafuko zaidi ya kisiasa.
Kupanda kwa bei "huenda ikafikia mahali ambapo uhusiano ambao tayari ni dhaifu kati ya watawala na watawaliwa unaweza kukatika, na kusababisha kutoridhika sana miongoni mwa watu," anaonya mwanasosholojia Prof Rachid Hamadouche.

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa zamani, Abdelazziz Bouteflika, alilazimika kujiuzulu mnamo 2019 kutokana na maandamano ya watu wengi.
Mrithi wake, ambaye wakati mmoja alikuwa mshirika wa karibu, sasa anakemea mara kwa mara "mafia waliopora hazina ya nchi" chini ya Bouteflika.
Licha ya mabadiliko ya rais, vijana wengi bado hawajaridhika na waliendelea kushiriki katika maandamano ya kawaida ya barabarani hadi janga hilo lilipotokea mnamo Machi 2020.
Robo tatu ya watu wako chini ya umri wa miaka 37, na ukosefu wa ajira umefikia 11%, huku wengi wa wasio na kazi wakiwa wahitmu wa vyuo vikuu.
Hata hivyo serikali imesema kuanzia mwezi huu, watu wasio na ajira ambao wanaweza kuthibitisha kuwa wamekuwa wakitafuta kazi kwa bidii watapata posho ya kila mwezi ya takriban $ 90.
Jambo la kushangaza ni kwamba, kupanda kwa bei ya gesi duniani kote kutokana na vita vya Ukraine kunakomaanisha kuwa mamlaka zinaweza kumudu kulipa pesa hizi kwa muda mfupi.
Lakini wanauchumi wanasisitiza kuwa Algeria haiwezi kumudu kufuja fedha za hivi punde kutokana na mapato ya gesi kwa njia sawa na jinsi mapato ya mafuta yanavyoweza kuongezwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita yalivyopotea.
Lakini kwa sasa, wanunuzi kama Bi Sammer wamekwama kutafuta ofa bora zaidi na wanatumai kuwa muuza duka rafiki atawapa atawawezesha kupata mafuta mengi ya kupikia.













