Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Kwa nini India inanunua zaidi mafuta ya Urusi?
Urusi inatafuta masoko mapya ya mauzo yake ya mafuta huku vikwazo vya nchi za Magharibi vikizidi kuimarika - na India imekuwa ikichukua fursa ya bei iliyopunguzwa kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka nchini humo.
Marekani imesema ingawa uagizaji huu wa mafuta haukiuki vikwazo, "uungaji mkono kwa Urusi...ni kuunga mkono uvamizi ambao ni wazi una madhara makubwa".
India inapata wapi mafuta yake?
Baada ya Marekani na China, India ni nchi ya tatu kwa ukubwa duniani kwa matumizi ya mafuta, zaidi ya 80% ambayo huagizwa kutoka nje.
Mnamo 2021, India ilinunua takriban mapipa milioni 12 ya mafuta kutoka Urusi, 2% tu ya jumla ya uagizaji wake.
Kufikia sasa bidhaa kubwa zaidi mwaka jana zilitoka Mashariki ya Kati, na kiasi kikubwa pia kutoka Marekani na Nigeria.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Mnamo Januari na Februari, India haikuagiza mafuta yoyote kutoka Urusi.
Lakini kandarasi za Machi na Aprili tayari zimefikia mapipa milioni sita, kulingana na data iliyokusanywa na Kpler, kikundi cha utafiti wa bidhaa.
Serikali ya India inasema hata kama itanunua mafuta zaidi kutoka Urusi, "bado yatakuwa tone tu, katika ndoo kubwa" ya uagizaji wake wa mafuta duniani kote.
Kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine, sasa kuna wanunuzi wachache wa mafuta ghafi ya Ural ya Urusi, na bei yake imeshuka.
"Wakati hatujui bei kamili ambayo India inalipa, punguzo la Urals kwa Brent crude [kigezo cha kimataifa] katika wiki iliyopita imeongezeka hadi takriban $30 kwa pipa," anasema Matt Smith, mchambuzi wa Kpler.
Aina hizi mbili za mafuta ghafi kawaida huuzwa kwa bei sawa.
Lakini wakati mmoja mnamo Machi, wakati bei ya Urals iliendelea kushuka, tofauti kati yao ilifikia rekodi ya wakati wote, anaongeza.
Kwa hivyo "India na China zina uwezekano wa kununua angalau baadhi ya malighafi hii [ya Kirusi] kwa punguzo kubwa," anasema.
Je, vikwazo vya kifedha vina athari gani?
Kampuni kubwa za usafishaji nchini India zinakabiliwa na changamoto ya kujaribu kufadhili ununuzi huu uliopunguzwa bei, kwa sababu ya vikwazo kwa benki za Urusi.
Ni tatizo linalokabili biashara katika pande zote mbili.
Wachambuzi wa masuala ya fedha Bloomberg wanakadiria kuwa wasafirishaji wa India kwenda Urusi kwa sasa wanangoja malipo sawa na takriban dola milioni 500 (pauni milioni 381.5)
Mojawapo ya chaguzi ambazo India inaangalia ni mfumo wa ununuzi kulingana na sarafu za ndani, ambapo wasafirishaji wa India kwenda Urusi hulipwa kwa rubles badala ya dola au euro.
Ni wapi tena India inatafuta kununua mafuta?
Uagizaji wa mafuta ya India kutoka Marekani umepanda kwa kiasi kikubwa tangu Februari, kulingana na wachambuzi wa Refinitiv.
Hata hivyo, wachambuzi wa soko wanasema hii inaweza isiwe endelevu katika siku zijazo kwani Marekani inataka kutumia uzalishaji wake wa ndani wa mafuta kuchukua nafasi ya bidhaa kutoka Urusi baada ya uvamizi wake nchini Ukraine.
Pia kuna mapendekezo kwamba biashara na Iran inaweza kuanza tena chini ya utaratibu wa kubadilishana fedha ambao wasafishaji mafuta wa India wanaweza kutumia kununua mafuta yake. Mpangilio huu ulikoma miaka mitatu iliyopita, wakati Marekani ilipoiwekea tena vikwazo Iran.
Lakini hii haiwezekani kuanza tena bila makubaliano mapana zaidi yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kimataifa na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.