Mzozo wa Urusi na Ukraine: Sheria tata ya Putin ya kutorudisha zaidi ya ndege 500 za kibiashara kwa nchi za Magharibi

Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi inalipiza dhidi ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi.
Rais Vladimir Putin alitia saini sheria Jumanne kuzuia makampuni ya kigeni yaliyokodisha ndege zao kutoka Urusi kuzichukua tena.
Uamuzi huo umekuja baada ya makampuni kadhaa kuitaka Moscow kurudisha ndege walizokodi, ikiwa ni sehemu ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Na ni kwamba karibu 75% ya ndege zinazotumiwa na mashirika ya ndege ya Kirusi hukodishwa, kulingana na data rasmi, kwa jumla ya ndege 515 zenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 10,000.
Ili kuzuia hili, sheria mpya inaruhusu ndege za kigeni kusajiliwa nchini Urusi, ili "kuhakikisha uendeshaji usioingiliwa wa shughuli katika uwanja wa anga ya kiraia."
Hatua ya Kremlin ilikuja baada ya Bermuda na Ireland, ambako karibu ndege zote za kigeni zilizokodishwa zinazofanya kazi nchini Urusi zimesajiliwa, kusema kuwa zitasitisha vyeti vya kustahiki kwa ndege hizo.
Urusi sasa inataka kukwepa hatua hiyo kwa kuweka cheti cha usajili na usalama ndani ya mipaka ya nchi hiyo ili kuendelea kutumia ndege hizo za kigeni, ingawa inaweza kufanya hivyo tu kwa kuruka njia za ndani au kwa baadhi ya nchi washirika.
Anga iliyofungwa
Tangu uvamizi wa Ukraine mnamo Februari 24, makampuni ya Magharibi yamekuwa yakisitisha ukodishaji na kuomba kurejeshwa kwa ndege zao.
Njia nyingi za anga za kimataifa kutoka Urusi hazifanyikazi, baada ya idadi kubwa ya nchi, ikiwa ni pamoja na Marekani na wanachama wa Umoja wa Ulaya, kufunga anga zao kwa ndege za Kirusi.
Hatua hiyo iliyotiwa saini na Putin sasa imesababisha maswali ya kina kati ya wataalamu wa kimataifa wa masuala ya anga, lakini pia imezua shaka miongoni mwa mashirika ya ndege ya nchi hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tunatumai kuwa usajili wa ndege hizi nchini Urusi utaepukwa; tunataka kuzirejesha kwa makampuni ya kukodisha," chanzo katika mojawapo ya mashirika ya ndege kiliiambia Reuters.
"Ikiwa itasajiliwa nchini Urusi] shirika la ndege litakuwa mshirika. Sheria inatoa njia ya kujisajili nchini Urusi, lakini hailazimishi shirika hilo kufanya hivyo... Ni hatua ya kwanza ya kuteka nyara ndege," aliongeza.
Serikali ya Urusi imesisitiza kuwa inahitaji kutumia "hatua maalum" mbele ya vikwazo vya Magharibi ambavyo Putin amevitaja kuwa" sawa na kutangaza vita.
Katika jibu jingine kwa nchi za Magharibi, Kremlin ilitangaza Jumanne kwamba itaweka vikwazo dhidi ya maafisa kadhaa wa serikali ya Marekani, ikiwa ni pamoja na Rais Joe Biden na Waziri wa Mambo ya Nje Anthony Blinken.
Kama sehemu ya hatua hiyo, Moscow iliwapiga marufuku kuingia nchini.

Sheria yenye madhara makubwa
Uchambuzi na Theo Legget, mwanahabari wa BBC Biashara
Mamia ya ndege zinazomilikiwa na nchi za kigeni zimesalia nchini Urusi.
Ili kuzingatia athari hasi, makampuni ya kukodisha yanajaribu kuzichukua ndege zao.
Lakini hiyo inaonekana kuwa haiwezekani sana.
Ikiwa Urusi itashikilia ndege hizi, ambazo kwa pamoja zina thamani ya mabilioni ya dola, bado zitaweza kuruka, angalau nchini Urusi na katika jamhuri chache za zamani za Usovieti.
Lakini ni jambo moja kuiba ndege na ni jambo jingine kabisa kuendelea kuziendesha kwa muda mrefu zaidi.
Kampuni za Airbus na Boeing haziwezi kuwapa vipuri, kwa hivyo wakati kitu kinahitaji kubadilishwa, italazimika kuchukuliwa kutoka kwa ndege nyingine au kulichotengenezwa na kampuni nyingine.
Hiyo ina madhara makubwa ya kiusalama.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia itafanya iwe vigumu kupata usalama wa ndege hizo nje ya Urusi.
Huduma pia ni jambo la kutia wasiwasi, huku ndege nyingi zikihamishwa nje kwa matengenezo.
Na mzozo utakapoisha, Urusi italazimika kulipa bili kubwa.
Ikiwa ndege hazitatunzwa ipasavyo, thamani yake itashuka.
Kwa hiyo hata ikiwa mmiliki halisi atachukua ndege yake, watadai fidia.
Usafiri wa anga ni biashara ya kimataifa na unapaswa kuheshimu sheria.
Huenda Urusi ikaamua kudhihaki dunia nzima sasa.
Lakini siku moja atataka kujiunga tena, na hali inaweza kuwa ngumu sana.














