Mzozo wa Ukraine: Je ni kweli rais Vladmir Putin anataka kujenga himaya yake ''Russkiy Mir''?

Rais wa Urusi Vladmir Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Urusi Vladmir Putin

Vita ambavyo vinaendelea sasa nchini Ukraine vinatishia kuleta mabadiliko zaidi na hatari zaidi barani Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Katika siku za hivi karibuni, Rais wa Urusi Vladimir Putin ameongeza mashambulizi dhidi ya miji muhimu ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na Kherson, Kharkiv na mji mkuu, Kiev.

Na hajaonyesha ishara yoyote kwamba mashambulizi hayo yatakoma, licha ya vikwazo vikali vilivyowekwa dhidi ya nchi yake na mataifa ya magharibi.

Wachambuzi wengi wanajiuliza ni nini hasa kinachoendelea kwenye kichwa cha kiongozi huyo wa Urusi.

Moja ya majibu ya kawaida zaidi katika nchi za Magharibi, hasa nchini Marekani, ni kwamba Urusi ni kwamba Urusi siku zote inataka kujipanua na kwamba Putin ni mfano wa mtu mwenye kutamani hilo: kujenga himaya mpya ya Kirusi.

Na hii ndio ambapo dhana ya "Russkiy Mir" au "Ulimwengu wa Urusi" inaonekana.

Miji kadhaa ya Ukraine imeshambuliwa na Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Miji kadhaa ya Ukraine imeshambuliwa na Urusi

Kama Fiona Hill - mmoja wa wataalamu mahiri nchini Urusi - alisema katika mahojiano na Politico kwamba, Putin amekuwa akielezea wazo kwamba upo uwezekano waukraine na Warusi ni "watu wamoja," na kwamba lengo lake ni kuunganisha watu wanaozungumza Kirusi kutoka maeneo tofauti ambao wakati mmoja walikuwa sehemu ya himaya ya Kirusi 'tsarism'.

Lakini ni maana ya Ruskkiy Mir, ni ishara gani zinaonekana ambazo Putin anaelezwa kwamba anataka kuziunganisha, na jinsi gani uvamizi wa Ukraine unaweza kuwa muhimu katika kufikia lengo hili? Haya ni maelezo zaidi.

Ulimwengu wa Urusi au "Russky Mir" ni nini?

Ingawa hakuna ufafanuzi wa wazi wa kitaalamu kuhusu Ruskkiy Mir inamaanisha nini hasa, wachambuzi wamejaribu kuelezea.

Kwa wengine, Russky Mir ni ulimwengu unaojumuisha jamii nzima inayohusiana na utamaduni wa Kirusi, ambayo wana historia inayoingiliana, lugha na mila fulani. Kwa sababu hiyo hiyo, ni vigumu kuweka mpaka.

Kwa wengine, kuna misingi ya eneo ambayo inaweza kuwa msingi wa ulimwengu huu na ambayo inaweza kuundwa na Urusi yenyewe, pamoja na Belarus, Ukraine na Kazakhstan, kati ya mataifa mengine.

"Kuna vigezo viwili vya kufafanua Russkiy Mir. Ya kwanza ni utamaduni, ambao unahusisha utamaduni mzima wa Kirusi kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na wale walio nje ya eneo hilo," Juan Manuel de Faramiñán Gilbert, profesa katika Chuo Kikuu cha Jaen, aliiambia BBC.

"Dhana ya pili ni kijiografia na inategemea kile ambacho himaya ya zamani ya 'tsarist' iliyoundwa na Catherine. Inaweza kuenea hadi eneo la kusini karibu na Bahari Nyeusi au hata Georgia, "anaongeza.

Lakini kwa Sergey Goryashko, mwandishi wa habari wa IDHAA ya BBC ya Urusi, ufafanuzi wa ulimwengu wa Urusi katika kichwa cha Putin hauna mipaka.

"Miaka michache iliyopita, wanafunzi katika shule fulani walimuuliza Putin kuwamba mpaka wa Urusi unaishia wapi? Alijibu kwamba Urusi haina mpaka," anakumbuka kwa BBC Mundo.

"Na hiyo inaweza kuwa maana ya ulimwengu wa Urusi kwa Putin. Kwa sababu ikiwa tunaangalia vitendo vyao tangu 2014 (wakati wanaidhibiti Crimea), inathibitisha hasa kwamba ulimwengu wa Urusi hauna mipaka yoyote. Dunia ya Urusi ni dunia nzima," aliongeza.

Ni ishara gani Putin alizionyesha?

Vladimir Putin daima amekuwa akiisukuma Urusi kuibuka tena kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu duniani.

Na amewakosoa sana baadhi ya viongozi wa zamani wa Urusi ambao, kwa maoni yake, aliwashutumu kwa kuvunjika kwa Umoja wa Kisovyeti (ambao hatimaye ulijitokeza mwaka 1991).

"Putin amesema wazi kabisa kwamba (Vladimir Illich) Lenin aliharibu ulimwengu wa Urusi na kwamba hakuanzisha Urusi halisi.

Aliyekuwa kiongozi wa Usovieti Mikhail Gorbachev

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aliyekuwa kiongozi wa Usovieti Mikhail Gorbachev

"Kisha, alisema kwamba Mikhail Gorbachev na Boris Yeltsin ni waandishi wa kuvunjika moyo wa kweli wa Urusi," msomi anaongeza.

Kwa Putin, baada ya kuvunjwa kwa Umoja wa Sovieti, mipaka "iliwekwa kiholela kabisa na bila msingi wowote wa haki." Aliyasema hayo katika hafla ya harakati zake za kisiasa mwaka 2016.

Mnamo Julai 12, 2021, katika makala ndefu juu ya uhusiano na Ukraine iliyochapishwa kwenye tovuti ya Kremlin, Vladimir Putin alionyesha dalili zingine juu ya nia yake ya kuunganisha ulimwengu wa Urusi.

Rais Joe Biden amesema kwamba Rais Putin anataka kuanzisha ufalme wake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Joe Biden amesema kwamba Rais Putin anataka kuanzisha ufalme wake

Katika miaka ya hivi karibuni, rais ameimarisha matamshi na misimamo yake dhidi ya nchi za Magharibi, ambayo kwa baadhi ya wataalamu pia ni sehemu ya nia hii ya kuongeza nguvu za Urusi duniani.

"Anasema zaidi na zaidi katika hotuba zake, kwamba kila kitu kibaya ni kwa sababu ya Magharibi, kwa sababu ya vitendo vyake vya uhasama dhidi ya Urusi," anaelezea Sergey Goryashko.

"Mwaka 2014, kile kilichotokea Crimea, kila kitu kiligeuka kwa kutengeneza Ulimwengu wa Urusi na pia kwenye maneno ya uhasama ya Magharibi," anaongeza.

Mwaka 2007, Putin aliunda wakfu unaoitwa Russkiy Mir wenye lengo la kukuza lugha na utamaduni wa Urusi duniani, kama mradi wa kimataifa.

Kwa nini Ukraine ni muhimu?

Ukraine sio nchi baki duniani kwa Vladimir Putin.

Moja ya wakati mgumu zaidi wa kazi yake ya muda mrefu kama rais ilitokea mwaka 2004, wakati baada ya "mapinduzi yaliyoitwa ya chungwa" Viktor Yushchenko, anayeonekana huko Kremlin kama "kibaraka " wa Washington, alishinda uchaguzi wa Kiukreni.

Hii ilikuwa aibu kubwa kwa Putin kwa sababu ilionekana kama alikuwa amepoteza Ukraine. Wachambuzi wanasema kuwa rais hajasahau kushindwa kwenye hilo na hajasamehe.

"Mtazamo mkubwa wa utaifa wa Urusi ni kwamba Ukraine ni taifa dada la Slavic na, hata zaidi, kwamba ni moyo wa taifa la Rus. Ni itikadi yenye nguvu sana ambayo inaifanya Ukraine kuwa sehemu muhimu ya utambulisho wa Urusi," Gerald Toal, profesa wa mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Virginia Tech nchini Marekani, aliiambia BBC Mundo.

Katika muktadha huu, mji mkuu wa Ukraine, Kiev, unachukua umuhimu wa kipekee.

"Kiev imekuwa ikichukuliwa tangu mwanzo kile kilichoitwa mama wa miji ya Urusi. Kiev ni mji mkuu zaidi kwenye Dunia ya Urusi kuliko Moscow au St. Petersburg, "anasema Juan Manuel de Faramiñán Gilbert.

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi

Msomi anasisitiza kwamba "ikiwa Putin atachukua Ukraine, nina hakika kwamba atahamisha mji mkuu kwenda Kiev kwa sababu kwake dhana ya kiroho ya Kiev ina nguvu zaidi kuliko ile ya Moscow."

Kwa hivyo nini kitatokea?

Kwa mujibu wa Fiona Hill, hii haimaanishi kwamba Putin anataka kuyanyakua maeneo yote ya "Russkiy Mir", kama alivyofanya Crimea.

Lakini, kwa mujibu wa Mtaalam wa Politico, "inaweza kuanzisha utawala kwa kutenga nchi za kikanda, kuhakikisha kuwa viongozi wao wanaitegemea Moscow," iliyofungwa mitandao ya kiuchumi, kisiasa na usalama ya Urusi.

Kwa sehemu fulani, tayari imekuwa ikifanya hivyo.

Kazakhstan imepewa jina la "mshirika namba moja" wa Moscow na uhusiano huu wa karibu ulionyeshwa mnamo Januari mwaka huu wakati Putin aliamua kutuma vikosi vinavyounga mkono serikali ya mitaa kudhibiti maandamano ya vurugu ambayo yaliibuka baada ya bei ya mafuta kuongezeka sana katika nchi hiyo.

Belarus, wakati huo huo, imekuwa chini ya Moscow. Tangu uvamizi wa Urusi huko Ukraine imekuwa na jukumu muhimu, ikitumika kama msingi wa kupelekwa kwa jeshi la Urusi nchini Ukraine.

Lakini kwa Sergey Goryashko wa IDHAA ya BBC ya Urusi, hakuna anayejua nini kitatokea.

"Nitakuwa mkweli. Wiki mbili tu zilizopita, nilikuwa na uhakika wa 100% kwamba hakutakuwa na vita halisi nchini Ukraine. Na sasa nadhani Ukraine sio lengo kuu la Putin. Ni moja tu ya malengo yao," anahitimisha.