Nathuram Godse: Usiri unaomzingira muuaji wa Mahatma Gandhi

Chanzo cha picha, Mondadori via Getty Images
Katika jioni tarehe 30 Januari 1948, Nathuram Vinayak Godse alimpiga risasi na kumuua Mohandas Karamchand Gandhi alipokuwa karibu naye, wakati kiongozi huyo wa India anayeheshimika alipojitokeza katika mkutano wa maombi katika mji mkuu, Delhi.
Nathuram Godse mwenye umri wa miaka 38-alikuwa mjube wa Hindu Mahasabha, chamba cha mrengo wa kulia-kushoto.
Chama hicho kilikuwa kimemshutumu Gandhi kwa kuwasaliti Wahindu kwa kuwaunga mkono sana Waislamu na kutokuwa na msimamo mkali kuihusu Pakistan. Walikuwa wamemlaumu Gandhi kwa umwagaji damu ambao ulipelekea mgawanyiko,ambao ulisababisha kuundwa kwa India na Pakistanbaada ya uhuru kutoka kwa Uingereza katika mwaka 1947.
Kesi ya mahakamani ilimhukumu Godse kifo mwaka mmoja baada ya mauaji.
Alinyongwa Novemba 1949, baada ya mahakama ya juu zaidi kuidhinisha hukumu hiyo (Mhusika mwingine wa mauaji hayo,Narayan Apte, pia alipewa hukumu ya kifo, na wengine sita walihukumia kifungo cha maisha jela.)
Kabla ya kujiunga na chama cha Hindu Mahasabha, Godse alikuwa mjumbe wa Rashtriya Swayamsevak Sangh (Shirika la watu wanaojitolea la taifa) au RSS.
Waziri mkuu Narendra Modi mwenyewe ni mjumbe wa muda mrefu wa chama chama mama cha Hindu nationalism ambacho kimekuwepo kwa miaka 95. RSS huchangia ushawishi wa ndani katika serikali yake na nje.
Kwa miongo kadhaa, RSS kilichora picha ya Godse kama mtu wa kabila la wazawa aliyemuua "Baba wa Taifa", kama India wanavyopenda kumuita Mahatma Gandhi.
Hatahivyo,kikundi cha Wahindu wa mrengo wa kushito katika miaka ya hivi karibuni kimekuwa kikisifu ushujaa wa Godse na kusherehekea wazi wazi mauaji ya Gandhi. Waka jana mbunge wa BJP alimuelezea Godse kama ''mzalendo''.
Yote haya yamewakera Wahindi wengi, lakini RSS imeshikilia msimamo wake: Godse alikuwa meondoka katika shirika muda mrefu kabla ya kumuua Gandhi.
Kitabu kipya sasa kinadai kwamba hii sio kweli.
Godse, mvulana wa shule ya sekondari mwenye alifanya kazi ya kushona nguo na kuuza matunda kabla ya kujiunga na Mahasabha, ambako alihariri gazeti lake.
Wakati wa kesi, hakimu alichukua zaidi ya saa tano kusoma aya 150 za hukumu ya mahakama.

Chanzo cha picha, Haynes Archive/Popperfoto
Alisema alisema "hapakuwa na njama" ya kumuua Gandhi, ni hivyo kujaribu kuwalinda wahusika wenzake dhidi ya kufanya kosa lolote.
Alipinga shitaka kwamba alitekeleza mauaji chini ya mwongozo wa kiongozi wake, Vinayak Damodar Savarkar, ambaye alikuwa na mawazo ya Hindutva au Uhindu.
Godse pia aliiambia mahakama kuwa alikuwa ametoka katika RSS muda mrefu kabla ya kumuua Bw Gandhi.
Dhirendra Jha, mwandishi wa kitabu kuhusu mauaji ya Gandhi- Gandhi's Assassin, ameandika kwamba Godse - mwana wa kiume wa mfanyakazi wa post ana mama wa nyumbani- alikuwa "mfanyakazi maarufu" wa RSS. Hapakuwa na "ushahidi" wa kufukuzwa kwake kazi katika shirika.
Taarifa ya Godse iliyorekodiwa kabla ya kesi kuanza "haikuwahi kutaja idara ya RSS baada ya kuwa mjumbe wa Hindu Mahasabha". Hatahivyo, kauli yake ya mahakama ilisema kuwa "alijiunga na Hindu Mahasabha baada ya kuondoka RSS lakini alikaa kimya kuhusu ni lini hasa alifanya hivyo ".
"Hili limekuwa dai ambalo limesalia kujadiliwa zaidi kuhusu maisha ya Godse," Bw Jha anasema. Anaamini "waandishi wanaounga mkono-RSS " wametumia hili ku "Sukuma kimya wazo kwamba Godse alikuwa amevunja uhusiano na RSS na kujiunga na Hindu Mahasabha takriban muongo mmoja kabla ya kumuua Gandhi".
Mtafiti Mmarekani JA Curran Jr alidai kwamba Godse alijiunga na RSS katika mwaka 1930na kuondoka miaka minne baadaye, lakini hakutoa Ushahidi wowote wa matamshi yake.
Bw Jha ameandika kwamba taarifa iliyotolewa na polisi kabla ya kuanza kwa kesi yake, Godse alikiri kwamba alikuwa akifanyia kazi makampuni yote mawili mara moja.
Watu wa familia yake pia walijiunga na mjadala kipindi kilichopita. Kaka yake Gopal Godse, Nathuram, aliyefariki katika mwaka 2005, alikuwa amesema kaka yake "hakuwa ameondoka katika kampuni ya RSS".
Kando ya hayo, mpwa mkubwa wa Godse aliwaambia waandishi wa habari mwaka 2015 kwamba Godse alijiunga na RSS mwaka 1932, na kwahiyo "hakufutwa kazi wala kuondoka katika shirika ".

Chanzo cha picha, AFP
Aliandika kwamba chama cha Hindu Mahasabha na RSS alikuwa na "uhusiano mwema"na alikuwa na fikra zinazofanana na za RSS.
Makundi mawili, alisema, "mara kwa mara yalikuwa na mahusiano ya karibu na wakati mwingine yalikuwa hata yanabadilishana wanachama " hadi Bw Gandhi alipouawa. (RSS kilipigwa marufuku kwa zaidi yam waka mmoja baada ya mauaji ya Gandhi.)
Bi Golwalkar, mmoja wa viongozi wenye ushawishi zaidi wa RSS, alielezeza mauaji ya Bw Gandhi yalikuwa ni "msiba wenye ukubwa usio na kifani - kwasababu muovu mwenye akilinyingi ni mtu wa kawaida na Mhindu".
Hivi karibuni zaidi , viongozi wa RSS kama vile MG Vaidya wamemuita Godse ''muuaji'' ambaye ''aliwatusi'' Hindutva kwa kumuua mtu anayeheshimika zaidi India".
Waandishi kama vile Vikram Sampath wanamini kuwa RSS na Hindu Mahasabha vina uhusiano mkubwa. BwSampath, ambaye ameandika kwa kina Savarkar, ameandika kuwa uamuzi wa Hindu Mahasabha wa kuanzisha kikundi cha watu wanaojitolea kwa ajili ya "mapinduzi ya siri ya jamii" ku " linda maslahi ya Wahindu"wali kuwa na mahisiano ya "uhasama" na RSS.
Pia kulingana na Bw Sampath, RSS "waliacha kushirikiana na watu binafsi wasio na kazi tofauti na kiongozi wa Mahasabha, Savarkar ambaye aliamini katika " kuabudu mashujaa na waliopewa sifa zilizotiwa chumvi".
Bado mashaka kuwa Godse alikuwa ni sehemu ya mauaji na kwamba hakuwahi kuondoka katika RSS hayajafifia.
Unaweza pia kusoma:
Kabla Godse aende kwenye mnara wa kunyongwa tarehe 15 Novemba 1949, alisoma sentensi nne za sala ya RSS. "Hili tena lilifichua ukweli kwamba alikuwa mjumbe wa shirika hilo," anasema Bw Jha. "Kutohusisha mauaji ya Gandhi na RSS Gandhi ni kutunga historia."












