Hadithi ya Uasi uliowaleta pamoja Waislamu na Wahindu dhidi ya Wakristo na madhehebu mengine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Miaka 100 iliyopita , Bombay (ambayo kwa sasa inafahamika kama Mumbai) ilishuhudia mojawapo ya fujo za ajabu katika historia ya India ambapo Watu wa madhehebu ya Kihindu na Waislamu waliungana pamoja na kushirikiana kupigana dhidi makundi mengine ya kidini, kulingana na Mwanahistoria Dinyar Patel, ambaye aliandika kuhusu funzo ambalo India ilijifunza hadi leo kutoka na tukio hilo.
Ghasia za mwaka 1921, ambazo zinafahamika kama Ghasia za Mwanamfalme wa Wales, kwa sasa ni jambo lililosahaulika katika Mumbai
Lakini nyakati hizi za machafuko za kihistoria, hutoa masomo muhimu kuhusu ushabiki wa kidini na mfumo wa walio wengi .
Mashujaa wa matukio hay ani mashujaa wa uhuru wa India, Mfalme ajaye wa Uingereza, na Sultan wa Ottoman.
Matukio haya ya ghasia yalichpochewa na watu waliokuwa na itikadi tofauti mawazo na malengo ya swaraj (kujitenga), swadeshi (uchumi wa kujitegemea), kuzuwia vilevi, na umoja wa Kiislamu.
Mwezi Novemba 1921, Mwanamfalme wa Wales, baadaye Mwanamfalme Edward VIII, alifanya ziara ya kifalme katika wakati ulioonekana kama ni kujaribiwa kwa himaya ya India.
Wakati huo, India ilikuwa chini ya utawala wa uongozi wa ushirikiano wawa mwana wa kiume wa Mahatma Gandhi na ukoloni wa Kiingereza, ambao tangu tangu kuanza kwa Uasi wa 1958 ulikuwa tisha kubwa kwa utawala wa ukoloni wa Uingereza.
Chini ya kauli mbiu "Umoja kati ya Wahindu na Waislamu ", Gandhi alijiunga na vuguvugu lililoitwa Caliphate lililoongozwa na Waislamu nchini India ambao walikuwa wanahofia kwamba Uingereza itauangusha himaya ya Sultan wa Ottoman katika Vita kuu ya 1 ya dunia, kwani walimchukulia kama Khalifa wa Waislamu.
Huku hatua hii ilianza katika wakati wa kihistoria wa ukaka wa kijamii, Umoja wa Wahindu na Waislamu uliibua hofu wa Wakristo walio wachache, Wasikh, Waparsi na Wayahudi .

Kwa upande wake , Gandhi alisema hawana lolote la kuogopa. Alitangaza makubaliano baina ya Wahindu na Waislamu hayamaanishi kuwa madhehebu makubwa yanapaswa kutawala madhehebu madogo ."
Kwa upande wake Mwanamfalme wa Wales alitumaini kuwa ziara yake itaibua hisia za kuipenda Uingereza na kupunguza kasi ya viguvugu la Gandhi.
Katika kujibu hilo , Bunge la congress la taifa la India liliamua kumkaribisha mwanamfalme katika Bombay kwa mgomo, na kuchoma nguo zilizotengenezwa nje yan chi zenye alama za uchumi wa kinbeberu wa Uingereza.
Asubuhi ya tarehe 17 Nove,ba, 1921. Idadi kubwa ya wakazi wa Bombay walikiuka mgomo na kuhudhuria hafla ya kuwasili kwa Mwanamfalme wa Uingereza aliyefika kwa meli. Wengi wa wale waliomlaki walikuwa ni Waarabu, Wayahudi, Waingereza wenye asili ya kihindi na Waingereza wanaoishi India.

Chanzo cha picha, Getty Images
Licha ya amri ya Despite Gandhi ya kuheshimu agizo la mapokezi ya amani, Wajumbe wa congress walionyesha hasira wakati wa mapokezi.
Siku zilizofuatia kulishuhudiwa makabiliano makali ya hasira katika mitaa ya Bombay huku magenge ya watu weney fujo yakivamia aduka ya pombe ya watu wenye asili ya Persia(Iran) , na kuwapiga mawe na kutishia kuyachoma moto maduka hayo.
Gandhi alijaribu sana kujumuisha marufuku ya vilevi katika vuguvugu lisilo na ushirikiani na Uingereza, na akawataka Wapersia, ambao walikuwa na idadi kubwa ya maduka ya pombe kufunga kwa hiari maduka yao.












