Theluji nchini Pakistani: Mtu aliyekwama chini ya Theluji kwa saa kadhaa asimulia alichokiona

Pakistan"s Rescue 1122 personnel take part in the rescue efforts in the heavy snowfall-hit area in Murree, Pakistan, 09 January 2022

Chanzo cha picha, EPA

Mtalii ambaye alinaswa ndani ya gari lake kwa saa kadhaa kwenye theluji nzito nchini Pakistani alielezea hali hiyo kama "kuona kifo mbele yake" alipokuwa akisubiri msaada.

Samina alikuwa miongoni wa maelfu ya watu waliojitokeza kujionea theluji ilivyokuwa ikianguka kutoka milima ya Murree msimu wa baridi.

Lakini tukio hilo liligeuka mkasa baada ya theluji kuanguka kupita kiasi siku ya Ijumaa na kuangusha miti na kuziba barabara kiasi cha kukatiza shughuli katika eneo hilo lililopo kaskazini mwa mji mkuu.

Watu 22 walifariki katika mkasa huo , huku magari karibu 1000 yakikwama barabarani. Miongoni mwa waliofariki ni watu wawili kutoka familia moja.

Barafka Murree

Samina aliambia BBC kuwa aliondoka nyumbani saa kumi jioni saa za (Pakistan) kusafiri hadi mjini Murree, lakini aliishia kuwa miongoni mwa watu waliokwama ndani ya theluji.

Picha na kanda za video zilizoshirikishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha magari yaliyokwama na kufunikwa na theluji

Magari yalikuwa yamekwama kwenye barabara zenye msongamano karibu na mji wa milimani wa Murree

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Magari yalikwama kwenye barabara zenye msongamano karibu na mji wa milimani wa Murree

"Niliona kifo kikinikodolea macho," Samina alisema. "Nilidhani kulikuwa na magari ya theluji juu ya gari letu ... Yaani siwezi kusimulia hali yangu ilivyokuwa

"Tulimuomba Mungu atusaidie na tulikuwa na hofu ya kufa ndani ya theluji."

Kulingana na Tariq Ullah, afisa wa utawala katika jiji la Nathiagali lililo karibu, dhoruba ya theluji ilianguka kwa urefu wa futi tano (5ft) juu ya ardhi ndani ya saa chache.

"Ilikuwa dhoruba ambayo haikutarajiwa," aliambia shirika la habari AFP. "Kulikuwa na upepo mkali, ambao uling'oa miti. Watu waliokuwa karibu walijawa na uoga."

Samina hatimaye aliokolewa karibu saa nne asubyhi ya siku iliyofuata, baada ya kulala usiku mzima katika makazi yaliyojengwa katika mji huo wa kitalii, ambao uko mita 2,300 juu ya usawa wa bahari.

Watoto 10 walikua miongoni mwa watu waliofariki, kulingana na watoa huduma za dharura, pamoja na familia mbili za jamaa watano na wanane.

Polisi wanasema watu wanane walifariki kutokana na baridi kali huku wengine wakidhaniwa kufa kutokana na joto la gari walililokuwa wamewasha kujikinga na baridi.

Maswali mengi yameibuka kuhusu jinsi mkasa ho ilivyotokea bila ujuzi wa awali wa utabiri wa hali ya hewa.

PICHA

"Hatukupokea tahadhari yoyote ya umma, kutoka kwa wavuti wa serikali, taarifa ya habari wala idara ya utabiri wa hali ya hewa," mtalii Duaa Kashif Ali aliambia AFP

Yeye na jamaa zake wengine 13 na marafiki walikwama ndani ya magari yao kwa muda kabla yakuamua kutembea lilomita moja unusu kutafuta mahali pa kukaa.

Kulingana na mwandishi wa BBC Farhat Javed, eneo la Murree, linaweza kukimu hadi magari 5,000 kwa muda

Lakini siku ya Ijumaa, watu 100,000 waliruhusiwa kuzurueneo hilo, na kusababisha msongamano mkunwa wa magari.

Baadhi ya magari yaliachwa baarabarani, na watoaji huduma za afya - waliofahamishwa hali ilivyokuwa walikabiliwa na wakati mgumu kufika eneo la tukio asubuhi ya Ijumaa - waliambia BBC kuwa shughuli zao zilitatizika kutokana na msongamano katika eneo hilo

Mamlaka za Punjab zimesema kuwa zitachunguza madai kwamba haikutoa tahadhari ya mapema kuhusu hali ya hewa.

"Tume ya ngazi ya juu itapewa jukumu la uchunguzi, na ikiwa uzembe wowote utapatikana, hatua zitachukuliwa dhidi ya waliohusika," msemaji wa serikali Hassan Khawar alisema.

Lakini uchunguzi huo hautaanza kabla ya kusafisha mitaa ya Murree, jiji lililojengwa wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza wa karne ya 19.