Kwa nini sukari ya matunda ni nzuri kwa afya yako kuliko ile iliyosindikwa?

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Tunda ni chakula cha mmea ambacho hujumuishwa katika lishe zote zenye afya. Inajulikana, pamoja na mambo mengine, kwa utamu wake, hasa wakati limekomaa kwa usahihi.

Ladha hiyo tamu ya tunda ni kwa sababu ina kiasi kikubwa cha aina ya sukari inayoitwa fructose.

Pia ina glucose, lakini kwa kiasi kidogo. Lakini leo tutazingatia sukari ya fructose ambayo inaweza kuwa hatari zaidi kwa afya yetu.

Fructose pia, pamoja na glucose, sehemu ya sukari nyeupe na ile ya mahindi. Viungo vitamu vyote viwili hutumika kama viambato vya kawaida katika utayarishaji wa vyakula vilivyochakatwa, michuzi, peremende na vinywaji baridi vilivyotiwa utamu.

Na hapa ndipo tatizo linapoanzia. Tafiti nyingi zinahusisha ongezeko la matumizi ya bidhaa hizi na matukio ya juu ya magonjwa kama vile kisukari na mengineyo

Kiwango na ubora - maneno mawili makuu

Kiwango : Ulaji kwa wingi vyakula ambavyo vimeongezwa sukari humaanisha matumizi ya juu ya kalori. Ikiwa kalori haitachomwa, hujilimbikiza kama mafuta katika mwili na kusababisha magonjwa.

TH

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Kwa bahati mbaya, matumizi ya vyakula vyenye kalori nyingi, visivyo na matunda na mboga mboga na vilivyo na mafuta na aina hii ya sukari, imesababisha kuwepo janga la magonjwa duniani.

Kwa upande mwingine, ikiwa tnaenda kwa mtaalamu wa lishe utapata ushauri sawa kila wakati: ikiwa unataka kuwa na afya njema, kula karibu sehemu tano za matunda na mboga, umegawanywa katika milo tofauti ya chakula ya siku.

Ulaji wa wastani wa kila siku wa chakula cha asili, ambacho hakijachakatwa, kama vile matunda, ni afya. Na hatuzungumzi juu ya kula kilo mbili za pears na tikiti kwa siku!

Ubora: fructose hubadilika kuwa mafuta kwa urahisi sana kwenye ini. Kwa kiasi sawa kilichoingizwa, kwa mfano, fructose na glucose….fructose hutoa kiasi kikubwa cha mafuta katika ini.

Kwa maana hii, fructose ya ziada ina uwezo mkubwa wa kuwezesha kuonekana kwa magonjwa kuliko sukari nyingine.

Upakiaji ni kila kitu

Sote tunajua kwamba, baada ya yote, sisi ni nyani waliobadilika. Kwa mamilioni ya miaka, babu zetu waliishi na kutumia lishe tofauti, iliyojaa mboga mboga na matunda ambayo walikusanya siku nzima.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Tunapokula fructose, tunaimeza mzima yaani (matunda yenyewe), pamoja na vipengele vingine vyote: fiber, madini na vitamin.

Ndiyo maana ni lazima kutafuna vizuri kila kipande tunachochukua. Lengo ni kuchanganya vipengele vyake mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nyuzinyuzi nyingi, na mate yetu na juisi za kusaga chakula. Hii husababisha fructose iliyomo kwenye tunda kuingia mwilini mwetu polepole.

Kwa hivyo, seli za matumbo hutumia sehemu kubwa ya fructose wanayonyonya, hivyo kwamba kidogo sana hufikia ini kupitia damu na kubadilishwa kuwa mafuta.

Hivi ndivyo sukari ya viwandani inavyofanya kazi mwilini

Tunapokula kiasi kikubwa cha fructose, kilichopo kwenye peremende, ice cream au, kikiwa kioevu katika kinywaji cha sukari, hali ni tofauti sana.

th

Chanzo cha picha, AVERAGE PA

Tunajaza njia yetu ya utumbo na fructose , iliyochangamywa katika maji, ambayo huingizwa kwa haraka na seli za matumbo. Kisha hufikia ini, ambapo hubadilishwa kuwa mafuta.

Ini lina jukumu la kusambaza mafuta haya ya ziada katika mwili wetu. Ikiwa tunatumia vyakula hivi kwa wingi na mara kwa mara, kwa muda mrefu tutakuwa na matatizo ya afya.

Mafuta ya ziada yaliyowekwa katika mwili wetu yanaweza kusababisha magonjwa kama kisukari

Baada ya muda, matatizo ya afya yataongeza hatari ya mshutuko wa moyo au hata saratani. Kwa mfano, uchunguzi umechapishwa hivi karibuni ambapo umeonyesha kuwa matukio mengi ya saratani yanahusishwa na matumizi makubwa ya sukari.

Sukari ya matunda ni nzuri au mbaya?

Kwa hivyo sukari ya matunda ni nzuri au mbaya? Ikiwa umesoma hapo juu, unaweza ukaona jibu.

th

Chanzo cha picha, EPA

Ulaji wa matunda kama hayo katika lishe yetu ni ya afya. Hiyo ina maana kwamba tunauma, kutafuna, kuchanganya na vyakula vingine, ili kurahisisha usagaji wake. Kwa njia hii, vipengele vya matunda, ikiwa ni pamoja na fructose, huingizwa polepole katika mwili wetu.

Tunapokunywa juisi ya matunda, hata ikiwa ni ya asili, mambo hubadilika. Tunakula matunda mengi zaidi kuliko ikiwa tulilazimika kumenya, kuuma na kutafuna. Kwa kuongeza, kwa kuwa hatuchukui fructose katika hali yake ya asili, inafyonzwa ghafla, haraka, kufikia ini na mara moja huko tunajua tayari kinachotokea.

Kwa hivyo, matunda huliwa kama hivyo na juisi ni raha ambayo tunaweza kujiingiza mara kwa mara.

Na ukiamua kuwa na juisi, tafadhali usiondoe nyama! nyama husaidia sukari kutoka kwa tunda kuingizwa polepole ndani ya mwili wetu, kwa njia inayofanana zaidi na kile kinachotokea tunapokula tunda moja kwa moja.