Kuharibika kwa mimba: Hadithi ya Mlimbwende wa zamani wa dunia aliyehangaika kupata ujauzito

Rosanna Davison and husband

Chanzo cha picha, Phillip Massey/ Getty Images

Maelezo ya picha, Rosanna Davison na mume wake Wesley Quirke walipatwa na tatizo la kuharibika kwa mimba mara 14 kati ya mwaka 2014 na 2016

Kuwa na watoto ilikuwa ndio ndoto ya kila mara ya mlimbwende wa zamani wa dunia Rosanna Davison na mume wake Wesley Quirke.

Lakini huku marafiki zao wote "walionekana kuwa na mimba zenye afya ya kawaida ",wanandoa hawa walipatwa na tatizo la kuharibika kwa mimba mara 14 mfulurizo katika kipindi cha miaka miwili. ''Lilikuwa ni jambo la kusikitisha sana kwetu," anakumbuka Rosanna.

"Kupitia wakati, na hisia kwamba mtoto anayekuwa tumboni hadi kupotea kwa maisha ghafla sana. Lilikuwa ni jambo la kuvunja moyo."

Onyo: Baadhi ya wasomaji wanaeza kuhisi baadhi ya maelezo kwenye makala hii ni ya kuogofya.

Mshindi wa shindano la dunia la Ulimbwende mwaka 2003 anakiri ilijihisi kana kwamba sehemu ya mwili wake "ilikuwa inavunjika".

"Nilizaliwa na uwezo wa kujifungua lakini haukuwa unafanya kazi unavyopaswa."

Binti huyo wa muimbaji wa wimbo wa Lady In Red, Chris de Burgh alisea alibaini mbinu za kuishi na tatizo hilo" kwa kuzungumza na marafiki na familia, lakini aliongeza kuwa "kama wenza lazima utafute njia za kuishi na tatizo pia ".

"Kulikuw ana wakati katikati yam waka 2017 wakati tulipokuwa tumekwama ," Rosanna alielezea, katika mahojiano na kipindi cha Good Morning cha BBC Radio Ulster.

"Nilimwambia mumu wangu.'Sidhani mimi ni mwanamke wa kukupatia familia'.

"Nilifahamu ni kwa kiasi gani alitamani kuwa baba, ilikuwa ni ndoto yake pia.

"Aliniambia, 'Rosie tutakuwa na maisha mazuri, hata kama hatutakuwa na familia tutaangalia la kufanya'.

"Amekwa na mimi lakini ni jambo linaloweza kuwatenganisha wanandoa ."

Rosanna Davison pictured with her father, singer Chris de Burgh

Chanzo cha picha, Andreas Rentz/ Getty Images

Maelezo ya picha, Rosanna Davison kwenye picha akiwa na baba yake,muimbaji Chris de Burgh

Baada ya kufanyiwa matibabu mbali mbali na kuzungumza na kile kilichoonekana kama orodha ya madaktari bingwa isiyoisha "ili kujua ni nini ambacho kilikuwa sio ", wanandoa hawa walizungumza na Rafiki ambaye "aliamua kubebewa ujauzito na (surrogacy) na kuwa na uzoefu mzuri sana".

Rosanna alisema hii ilimtia moyo na na mume wake kuchunguza mchakato kwa ajili yao

"Tulipata ushauri wote wa kimatibabu na kisheria ambao tungeweza kuupata ," alisema.

Alikumbuka kwamba ilichukua "karibu mwaka mzima kupata vipimo vyote vya damu na kusainiwa kwa mikataba, huku utoaji wa uzazi ukianza mapema 2019.

"Nililiona kuwa jambo gumu kufikia uamuzi wa kubebewa ujauzito kwani vilikuwa ni kama vita vya hisia akilini mwangu kusema kweli , 'Ninaweza vipi kumtazama mwanamke mwingine akinibebea mimba , mtoto wangu?'

"Tuliamua kuwa lilikuwa ndio chaguo letu pekee."

Wenzi hao waliamua kuchagua kubebewa mimba kwa misingi ya biashara " kwasababu tulitaka kuhakikisha hakuna anayetumiwa " ingawa wali " hisi ilikuwa bora kwetu sisi kutojenga uhusiano " na mwanamke anayetubebea ujauzito hadi utakapofanyika uchunguzi wa scan ya mwisho kabla yam toto wao Sophia alipozaliwa.

'Lilikuwa ni jambo lisilo la kawaida'

Kufuatia kufanikiwa kwa mchakato huo katika mwaka 2019, Rosanna alisea mpango umekuwa ni " kubebewa mimba tena katika mwaka 2020" hatahivyo mpango huo haukutekelezwa kwani alibaini kuwa alikuwa na ujauzito wa mapacha.

Mwezi Aprili, 2020, wiki chache baada ya Jamuhuri ya Ireland ilipoingia katika kipindi cha amri ya kukaa nyumbani ''lockdown'' kutokana na janga la Covid-alijihisi "mchovu,mwenye izunguzungu na mwenye hysia kiasi" na kwahiyo akafanya kipimo cha ujauzito.

"Mara moja kilikuwa na mistari miwili ya rangi nyekundu iliyokolea ," alisema.

"Lilikuwa ni jambo lisilo la kawaida nab ado ninafikiria tukio hilo sana."

Kwa kushirikisha watu hadithi yake na mume wake, Rosanna anasema anamatumaini ya kuvunja unyanyapaa unaozingira kukosa uwezo wa kupata ujauzito na uharibikaji wa mimba.

"Wakati tulipokuwa tunapitia miaka yote hiyo ya kuhangaika, nilikuwa natamani sana kupata hadithi ya matumaini," alisema.

"Bado ninajihisi manusura wa majuto. Siamini tumetoka katika upande mwingine na familia yetu.

"Ninahisi mwenye na uhusiano sana na wanawake na wenzi , na wanaume , ambao hawajabahatika kama kama sisi ."alisema Bi Rossana.