Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Gavana wa zamani wa DRC atiwa nguvuni kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali ya umma
Gavana wa zamani wa Jimbo la Kongo Central katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Atou Matubuana amekamatwa Jumamosi mjini Kinshasa.
Mahakama ya mwanzo ilikuwa tayari imetoa kibali cha kumkamata (arrest warrant) ,
Gavana huyu ambaye alikuwa anaongoza jimbo la Kongo Central ambalo limekuwa miongoni mwa majimbo yaliochangia pakubwa katika mfuko wa serikali, alitumiwa na mkaguzi mkuu wa maswala ya fedha kwa ubadhirifu wa mamilioni ya pesa. Kwa takriban miezi minne iliyopita, Bw Matubuana alifahamishwa kuhusu tuhuma dhidi yake lakini alishindwa kujisalimisha kwenye mahakama.
Maafisa wa polisi wa mahakama ambao hawakuwa wamevalia sare za kazi, walionekana kwenye video wakimkokota kwa nguvu Bwa Mutubuana kwenye mitaa, huku umati wa watu ukiwafuata nyuma.
Video ya tukio hilo imesambazwa na watu mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii:
Taasisi ya ukaguzi wa fedha za umma nchini Congo/Kinshasa (IGF) ilibaini ubadhilifu wa mali ya umma dhidi ya gavana huyo, baada ya kufanya ukaguzi katika jimbo la Kongo Central na ilikuwa tayari imechukua hatua za kisheria dhidi yake.
Ripoti ya afisa wa polisi wa mahakama katika alimhusisha Gavana Atou Matubuana Nkuluki na uadhilifu wa pesa za DRC 6,116,626,205(sawa na dola 3,058,313 , ambazo baadhi yake zilitolewa benki bila nyaraka kutoka kwa mfuko wa kusaidia shuguli za maendeleo ya kiuchumi, kijamii , sayansi na utamaduni , mfuko wa kukabiliana na majanga asilia na ajali, na pesa za usafi.
Mkuu wake wa wafanyakazi , Nzeza zi Ngeti, hakuwahi kuhamishwa tangu ufichuzi wa IGF ulipofayika.
Watu wengine waliotajwa kuhusiana na sakata hiyo ni pamoja na Mhasibu mkuu wa umma wa jimbo, naibu gavana, na Katibu binafsi wa gavana ambaye hajulikani alipo.