Vilivyotafutwa mitandaoni 2021: Squid Game, Madiliko ya tabianchi na afya ya akili yaongoza

Seong Gi-hun, mmoja wa wahusika wakuu wa Squid Game, akishikilia dalgona

Chanzo cha picha, Netflix

Maelezo ya picha, Squid Game iko kwenye orodha ya show za TV iliyotafutwa sana

Google imezindua orodha yake ya kila mwaka ya mitindo na mada kuu, ambayo inatoa muhtasari wa panda shuka za maisha katika mwaka 2021 na safari ya busara ya kumbukumbu ya matukio hayo.

Kampuni hiyo kubwa ya kiteknolojia hutumika kama injini ya utafutaji maarufu zaidi duniani na kila mwisho wa mwaka hufichua ripoti kuhusu maswali na mada zinazotafutwa zaidi.

Mwaka mgumu

A finger scrolling on a phone

Chanzo cha picha, Getty Images

Janga la Corona lilipotokea kote duniani, tuliingia mwaka 2021 kwa neno maarufu la utafutaji lililoashiria hali ya nyakati: 'doomscrolling'.

Neno hili linafafanua kitendo cha kuangalia skrini ya simu yako kwa kutarajia habari mbaya zaidi.

Google inasema neno 'doomscrolling' lilitafutwa 'sana' duniani, na lilivuma zaidi mwezi Januari.

Kwa watu wengi duniani, ulikuwa wakati wa wasiwasi na hofu. Mipaka ilifungwa, safari za ndege kukatizwa, na amri ya kutotoka nje kuwekwa.

Watu waliingia mitandaoni kupata habari za hivi punde kuhusu Covid-19 na wengi wao walitafuta neno linaloelezea maana halisi ya kile wanachofanya - doomscrolling.

Afya ya akili

Mwanamke akiangalia nje kupitia dirishani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Amri ya kutotoka nje iliathiri afya ya akili ya watu kote duniani

Mnamo 2021, utafutaji wa kimataifa wa 'afya ya akili' ulifikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea, kufuatia mwaka mmoja wa kutengwa na baadhi ya watu wakihangaika na upweke na kuomboleza kuwapoteza wapendwa wao.

Ulimwengu ulitafuta 'jinsi ya kudumisha afya ya akili' na 'jinsi ya kuponya' zaidi kuliko hapo awali.

Katika ishara nyingine kwamba tulizingatia zaidi afya yetu ya akili, maneno 'chanya ya mwili' na 'uthibitisho', kutoa kauli chanya ili kushinda mawazo hasi, yalitafutwa mwaka huu zaidi kuliko hapo awali.

Mabadiliko ya tabianchi

Mwanamke akitembea ndani ya maji akiwa amebeba begi lenye vitu vyake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Karibu wakazi milioni mja wa jimbo la Louisiana nchini Marekani waliachwa bila umeme baada yaKimbunga Ida kutua

Lakini haikuwa tu afya zetu,ustawi wa sayari pia ulikuwa akilini mwetu.

Kuanzi Kimbunga Ida hadi ukame na mioto mikubwa ya mwituni - uliwengu ulimwengu ulishuhudia athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa katika mwaka wa 2021.

Kulingana na data ya Google, tulitafuta njia salama ya kushi kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Utafutaji wa 'jinsi ya kuhifadhi' na 'uendelevu' ulifikia kiwango cha juu zaidi duniani kote.

Kuanzia mji mikubwa hadi visiwa,ulimwengu ulitafuta 'athari za mabadiliko ya hali ya hewa' zaidi kuliko hapo awali.

Labda haishangazi, Fiji, mojawapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, ilitafuta zaidi.

Pesa ni muhimu

Kuwa bosi wako mwenyewe imekuwa mtindo wa Google

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuwa bosi wako mwenyewe imekuwa mtindo wa Google

Watu wamekuwa wakihofia usalama wa kazi zao na uchumi, haswa kutokana na kutokuwa na uhakika wa kifedha unaosababishwa na janga hilo.

Nia ya kuwa bosi wako iliongezeka.

Mwaka 2021, ulimwengu ulitafuta fursa mpya za ujasiriamali, ukitafuta 'jinsi ya kuanzisha biashara' kuliko 'jinsi ya kupata kazi'.

Nchini Marekani pekee, zaidi ya watu milioni nne waliacha kazi mwezi Oktoba, kulingana na takwimu za Idara ya Kazi.

Kwa watu wengine, janga hilo lilikuwa kipindi cha kutathmini tena vipaumbele vyao, kuwasukuma kutafuta kazi ambazo zinatimiza mahitaji yao zaidi au kutafuta tu malipo bora mahali pengine.

Google,NFT ni nini?

Mada nyingine iliyohusiana na jinsi ya kutafuta pesa ilikuwa NFTs.

NFTs au ishara zisizo na kuvu ni picha za kidijitali au kazi ya sanaa ambayo inaweza "kuwekwa alama" ili kuunda cheti cha umiliki, ambacho kinaweza kununuliwa na kuuzwa.

NFTs zimekuwepo kwa muda, lakini wakati NFT ya mwanzilishi wa Twitter Jack Dorsey ya tweet ya kwanza kabisa ilipouzwa kwa dola milioni 2.9, udadisi wetu ulishika kasi.

Tulitaka kujua zaidi kuhusu mali ya kidijitali, tukiweka neno NFT juu ya orodha ya mambo ambayo ulimwengu ulitafuta 'kuunda'.

Watu mashuhuri wa kifalme

Kundi la wafanyakazi wa Squid Game

Chanzo cha picha, Netflix

Maelezo ya picha, Filamu ya Squid Game kwenye Netflix ulitazamwa zaidi katika nchi 90

Mwezi Machi Mwanamfalme Harry na mke wake Meghan Markle walifanya mahojiano yao ya kwanza ya runinga na mtangazaji wa Runinga ya AMarekani Oprah Winfrey tangu waache majukumu yao kama washiriki waandamizi wa familia ya kifalme.

Mahojiano ya Meghan na Harry yakawa "mahojiano yaliyotafutwa zaidi katika historia ya Google Trends ulimwenguni".

Wanandoa hao walifichua uhusiano wao wa kifamilia na familia ya kifalme ya Uingereza na mazungumzo yanayodaiwa yalifanyika kuhusu rangi ya ngozi ya mtoto wao Archie, na kugonga vichwa vya habari kote duniani.

Lakini hiyo haikuwa wakati pekee wa matukio katika Televisheni mwka 2021.

Korean drama

Kwa kuwa watu muda mwingi walikuw amajumbani, walipata nafasi ya kutazama filamu ndefu kwa kutumia simu zao.

Squid Game, ya Korea Kusini kwenye mtandao wa Netflix, ni kipindi cha televisheni kilichotafutwa sana kote duniani.

Hadithi ya kikundi cha watu ambao lazima waokoke katika mfululizo wa michezo hatari ili kujishindia zawadi ya pesa itakayobadilisha maisha iliufurahisha ulimwengu, na kukifanya kiwe kipindi kilichotazamwa zaidi katika Netflix.