Unyanyasaji wa nyumbani: Mwanamke aliyetumiwa vibaya na kudhibiwa na mpenzi ambaye nusura ayaharibu maisha yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Udhibiti wa mwenzi iwe mpenzi wa muda au mwenzi wa ndoa ni mojawapo ya ukatili unaofanyika katika familia na katika mahusiano baina ya wenzi.
Wakati mwingine aina hii ya mahusiano inaweza kumuachia mmoja wao majeraha ya kimwili. Lakini uharibifu mkubwa ambao muathiriwa hubaki nao zaidi ni kisaikolojia ambao unaweza kuwa mbaya zaidi y ahata kupigwa au kutukanwa na mtu anayempenda.
Hii ni simulizi ya mwanamke mmoja kwa jina Sarah (sio jina lake halisi) aliyekuwa na mahusiano ya kimapenzi na ZacK ( sio jina lake halisi)
'Jinsi safari ya mahaba ya majonzi ilivyoanza'
Wakati alipokuwa na umri wa miaka 15 au 16 hivi, alikuwa Rafiki yake Zac, walipokuwa shuleni.
Baada ya kuzungumza kwa wiki kadhaa, Zack alimkaribisha Sarah kwenye tamasha. Sarah alikuwa mwenye aibu wakati ule kwasababu hakuwahi kutoka kwa matembezi peke yake. Kwahiyo aliwaalika marafiki zake waende naye.
"Nilitaka tuende wawili peke yetu." Anakumbuka maneno ya Zack'. Alimpa onyo kwamba kama hawataenda wawili peke yao hakutakuwa na fursa tena ya kuwa pamoja tena.
'Kwanini kwanza unaongea naye?.'
Sarah alianza kumpenda Zack. Na mara kwa mara alimualika watembee pamoja peke yao. Anafahamu kuwa Zack anampenda pia. Kwahiyo ingawa aliogopa kutembea kwenda nyumbani peke yake, lakini Sarah alikubali kuwa pamoja kwa mud ana Zack.
Miezi michache baadaye wawili hao walikuwa tayari wamekuwa wapenzi.
Kabla ya kwenda kwenye sherehe katika nyumba ya Rafiki yake Sarah mara nyingi hupenda kujaribu gauni ambalo atavaa kwa ajili ya sherehe. "Gauni hili linaonye sana mwili wako," alimwamba Zack, na kwa kuamini maoni ya mpenzi wake, Sarah hanabadili nguo alizopanga kuzivaa.
Wakati Sarah alipokuwa akizungumza na rafiki yake mwingine wa kiume shuleni, Zack alikuwa anamwambia asiongee naye kwani inamfanya ajihisi mwenye wivu.
"Kwanini kwanza unaongea naye," Zack alifoka.
Sarah alifahamu kuwa hakukuwa na mazungumzo ya siri. Lakini alifikiri Zack alikuwa sahihi. Alifikiria basi kama inamfanya Zack ajihisi hivyo basi ni sawa tu.
Wakati Zack alipoanza kutumia madawa ya kulevya mara kwa mara, Sarah alimwambia kuwa ana hofu juu yake.
"Acha kunieleza ni nini la kufanya!'', Zack alimwambia.
Kadri Sarah alivyoendelea kuwa Zack kwa muda mrefu zaidi, alianza kutoweka zaidi na zaidi na kujitenga na marafiki zake. Zack alisema ni kawaida kwa wapenzi ambao ndio wamekutana. "Hatahivyo, hata siwapendi marafiki zako ."alimwambia.
Baadaye alikuja kugundu akwamba Zack aliwatumia ujumbe marafiki za , Sarah kisiri alisema, "Sarah anawachukia na kuwasengenya wasipokuwepo."

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kuingia Chuo kikuu Sarah alipata kazi katika Chuo kikuu alichokichagua. Zack aliamua kufanya tena mtihani ili kuendelea kuwa naye.
"Usiende, kwanini unaondoka hapa?" Zack alimuuliza.
Hakutaka Sarah aende chou kikuu zaidi na zaidi. Kwa kusema kwamba haina maana kwake kuendelea na masomo.
"Ni kupoteza pesa. Kwanza mimi ndiye nitakayefanya kazi nitunze familia yangu…" Zack alidai.

Sarah, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 23, alisema miaka yake ya kwanza na Zack mahusiano yao''hayakuwa mabaya sana'' "Ninamaanisha kuwa hayakuwa mabaya sana kama yalivyokuwa mwishoni,'' anaeleza.
Kudhibitiwa kimapenzi kuna maana gani?
Kutumiwa vibaya na mwenzi au mpenzi mara mara nyingi hakubainiki kwa vitendo, bali kwa mchanganiko wa maneneo, tabia, vitisho na manyanyaso, kutengwa na kuwa muathiriwa wa udhibiti huwafanya waathiriwa kupoteza uhuru wao wa kibinafsi na uwezo wa kujiamini.
Mara nyingi waathiriwa huelezea unyanyasaji wao wa kisaikolojia na kihisia.
Ni njia ambapo mwenza au mpenzi wako anaharibu uhuru na kujiamini kwako na kitu unachobaki kuwa nacho cha ''kawaida'' unachokifahamu ni mwenza anayekuumiza.
Asili ya udhibiti huu ni kwamba mara nyingi waathiriwa huwa hawaonekani. Au ni vigumu kumtambua dalili za mwenza anayenyanyaswa miongoni mwa wenza wawili.
"Alisema anaweza kuvunja shingo langu, iwapo anataka kufanya hivyo ."
Mara nyingi Zack alilalamika kwamba hana pesa ya kununua chakula, kwahiyo ilimlazimu Sarah kumpa pesa nyingi. Lakini hakutaka kumuadhibu.
Zack kila mara alimwambia, "Unafanya haya kunifanya nijihisi mimi vibaya ."

Chanzo cha picha, Getty Images
'…uko wapi?, uko nanani?, Unafanya nini.?'
Wakati wa masomo ya chuo kikuu Zack hakuwa na Sarah, lakini alikuwa akimlazimisha asikae wala kutembelewa na marafiki zake nyakati za usiku, mara nyingi akisema kuwa "atapewa dawa za kulevya na kubakwa na watu asio wajua " na hilo lililuwa linamfanya Zack awe mwenye wasi wasi na kumkosesha usingizi.
Lakini kama Sarah akisisitiza kwamba anataka kuwa na marafiki na kuamua kufanya hivyo , alikuwa akipokea jumbe nyingi sana kutoka kwa mpenzi wake wa kiume ambaye alikuwa akimuuliza…uko wapi?, uko nanani?, Unafanya nini.?
Hatahivyo kabla ya kubaini mambo hayakuwa sawa katika mahusiano haya, alianza kuhofia usalama wake.
Anakumbuka zaidi kisa ambapo Zack alikuja kumuona katika chuo kikuu.
Alimlipia garama ya usafiri. Na wakati walipokuwa wamelala kitandani pamoja, ghafla alisema , "Ninaweza kuvunja shinyo yako sasa hivi nikitaka kufanya hivyo."
Sarah alisema tabia ya ukatili ya Zack ilifika hadi kitandani. "Alipenda kuzungumzia jinsi anavyotazama filamu za ponografia za ukatili ."
"Wewe huwezi kufanya haya chumbani. Ndio maana ninatafuta kwingine," Zack alisema.
Zaidi ya mara moja Sarah alisema anahofia maisha yake kwasababu Zack anapokasirika hurusha viti huku na kule na kupasua viti huku akimtishia, utafikiri ni jambo la kawaida
"Nilikuwani ninafikiria kila mara na kujiuliza 'Je ninapenda kuishi hivi maisha yangu yote yaliyobakia?'"
Kwa bahati mbaya, mara nyingi unyanyasaji wa aina hii huwa haumaliziki kwa kuacha urafiki.
Haikuwa rahisi kujinasua kutoka maisha ya mahusiano

Kulingana na Dokta. Jane Mocton Smith, ambaye ni mtaalamu wa uhalifu nchini Uingereza, tabia kama hizi ni uhalifu.
Wakati Sarah alipoamua kuachana na Zack aliamua kuachana naye njiani kwasababu nilitaka kufanya hivyo mbele ya jamii ili asithubutu tena kumuumiza. Lakini baada ya miezi kadhaa Zack badi anamnyanyasa.
"Nisipojibu simu yake ananitishia kuwa kuwa atajiua ," Sarah anakumbuka.
Wakati Sarah alipojaribu kuizuwia simu yake Zack alivamia nyumba yake. Na kuna siku alivamia nyumba ya mama yake.
"Nilikgundua kuwa sitaweza kuondokana naye hadi nitakapohamia kwingine ambako hatajua niliko tena ,"anasema Sarah.
Imepita sasa miaka miwili, tangu Sarah ayaepuke maisha hayo ya kutisha. Ameweza kuingia tena katika jamii kama kijana yoyote wa kike na sasa ana mahusiano ya furaha na anasema ameanza kujihisi ni yeye tena.
Dalili zinazoashiria kuwa unadhibitiwa na kutumiwa vibaya na mpenzi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la misaada la wanawake Women's Aid, linalowasaidia wanawake wanaokabiliwa na unyanyasaji wa nyumbani linaainisha dalili hizo kama ifuatavyo:
- Kukutenga na familia pamoja na marafiki zako
- Kutopata mahitaji ya kimsingi kama vile chakula
- Kuchunguzwa kwa muda wako
- Kufuatiliwa kwa mawasiliano kwa kutumia vifaa vya mawasiliano ya mtandao au vya upelelezi
- Kudhibiti mambo maisha yako yya kila siku, kama vile unakoenda, nani unayekutana naye, nguo unazovaa na ni lili unalala
- Kukuzuwia kupata usaidizi wa huduma kama vile huduma za matibabu
- Kujihisi mwenye makosa mara kwa mara, na kujihisi hauna maana.
- Hukufanya ujihisi mwenye aibu, usiyejiamini na kukudhalilisha.
- Huchukua udhibiti wa fedha na mali zako.
- Kukutisha na kukufanya ujihisi muoga
Unaweza pia kusikiliza:














