Uber yapiga hatua ya kwanza kujiunga na soko la bangi

Chanzo cha picha, Getty Images
Uber inaingia kwa mara ya kwanza katika soko la bangi, na watumiaji wa Uber Eats huko Ontario, Canada wataweza kuagiza bidhaa za bangi hivi karibuni kwenye programu hiyo tumishi.
Kampuni hiyo ilikataa kuthibitisha iwapo itasambaza bidhaa hizo zaidi nchini Canada na Marekani.
Thamani ya soko la bangi nchini Canada kwa mwaka ni karibu dola bilioni nne.
Watumiaji wa Uber Eats watalazimika kuthibitisha umri wao kwenye programu na kisha wataweza kuchukua maagizo yao ndani ya saa moja, kampuni hiyo ilisema.
Chini ya sheria za Kanada, ingawa matumizi ya bangi yamekuwa halali tangu 2018, bado ni haramu kuiwasilisha.
Kwa muda sasa Uber imekuwa na malengo yake katika soko linaloshamiri la bangi.
Mwezi Aprili, Afisa mkuu mtendaji wa Dara Khosrowshahi alisema kampuni hiyo itazingatia kuwasilisha bangi mara tu itakaporuhusiwa chini ya sheria za Marekani.
Wazlishaji haramu
Licha ya uuzaji wa bangi kwa matumizi ya burudani kuwahalalishwa nchini Canada miaka mitatu iliyopita, wazalishaji haramu bado wanadhibiti sehemu kubwa ya mauzo. Hili na jambpo ambalo serikali imekuwa ikijaribu kupata ufumbuzi.
Uber imesema ushirikiano wake na Tokyo Smoke utasaidia nchi kununua bangi salama na halali ili kudhibiti wauzaji haramu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Soko la bangi la Canada linakadiriwa kuwa litaendelea kukua katika miaka ijayo na kampuni ya utafiti wa tasnia ya BDS Analytics inatarajia mauzo kukua hadi dola bilioni saba ($6.7bn) ifikapo mwaka 2026.
"Tutaendelea kuzingatia kanuni na fursa kwa karibu soko kwa soko. Na jinsi sheria za ndani na shirikisho zinavyobadilika, tutachunguza fursa na wafanyabiashara wanaofanya kazi katika maeneo mengine," msemaji wa Uber alisema.
Mahitaji ya bidhaa za bangi yalikua kwa kiasi kikubwa mwaka jana kwani watu walikuwa wamekwama majumbani amri ya kutotoka nje ilipowekwa.















