Kanisa la bangi: Unajua imani ya wafuasi wa 'Kanisa la Kimataifa la bangi?

Kanisa la kimataifa la bangi ni kanisa kama yalivyo makanisa mengine, kinachoongezeka hapa ni bangi tu na kuondolewa kwa imani ngumu ngumu," mwakilishi wa Kanisa hili.
Lee Molloy amezungumza na BBC kutoka nyumbani kwake kwenye milima ya Colorado, Marekani ambapo wameruhusu bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa tangu mwaka 2000 bangi na matumizi kwa ajili ya starehe tangu 2012.
Huyu ndio aliyeasisi Kanisa hilo, akiwa na Steve Burke, na marafiki zake wengine kadhaa, wakilitumia Kanisa la zamani huko Denver, na kulibadili kuwa Kanisa la bangi.
Lilikuwa jengo la zamani lenye miaka zaidi ya 110, na wamiliki wake walitaka kulifanya kuwa eneo la makazi, lakini waasisi hawa wakawashawishi wamiliki na kulitumia kwa ajili ya shughuli za umma.
Katika miaka kadhaa iliyopita, imekuwa sehemu inayowavutia wageni wengi kufanya utalii. Serikali ya Marekani inalitambua kanisa hilo kama taasisi isiyojiendesha kifaida kama ilivyo kisheria kwa dini zingine nchini humo.
Aprili 20 kila mwaka ni siku muhimu katika kalenda ya Kanisa hilo, ikiwa maalumu kwa ajili ya kusheherekea matumizi ya mmea huo na aina nyingine ya mimea kama hiyo yenye kuwekwa kwenye kundi la dawa ya kulevya.
Pia namba 420 na Aprili 20 ni alama ya utamaduni wa bangi nchini Marekani, na inaaminika kwamba wanafunzi kadhaa wa Marekani wenye umri unaokadiriwa kufikia miaka 17 hukubaliana kukutana kila siku saa 10 na dakika 20 jioni kwenda kutafuta bangi.

Wakati wa janga la corona, Kanisa hili la bangi liliweka masharti ya kujilinda na virusi kama walivyofanya makanisa mengine.
Lee Molloy anasema kabla ya janga: "Tunakusanyika, kunakuwa na muziki na mishumaa, tunawasha bangi, tunashirikiana pamoja, na tunasoma masomo ya matakatifu kutoka vyanzo tofauti tofauti."
Kuwa sehemu ya Kanisa hilo, hauhitaji kubadili dini yako ama imani yakona wafuasi wa kanisa hilo wanajiita wokovu ama walokole, wameokoka.
Lee Molloy anafananisha kitendo hicho kama kupanda mlima ama hali ya kuwa juu kwenye uwanda wa juu.
Anasema: "Naishi milimani, ninapozidi kupanda mlima nahisi muinuko uliounganishwa na mazingira nilipo, lakini kuna muinuko wa kiroho, vile ulivyo kiroho. Ni kama unavyosikia unavyovuta sigara.

Kanisa la Kimataifa la Bangi sio la kwanza Marekani kutumia bangi kwenye imani ya kidini. Mwaka 2016 ilishuhudiwa kuanzishwa kwa makanisa mawili kama hayo, lakini hawafuati mafundisho anayosema Molloy kuhusu hisia za muinuko. Kulikuwa na kanisa lilililoitwa "First Cannabis Church of Reason and Reason" huko Michigan na baadaee likaanzishwa lingine "First Cannabis Church" huko Indiana.
Mafundisho yaliyokuwa yanatolewa wakati huo ilikuwa ni 'mmea wa uponyaji (kwa maana ya bangi au marijuana) unatuleta pamoja na kutuunganisha na wengine, na ni chanzo cha afya zetu, mapenzi na dawa kwa magonjwa na msongo wa mawazo."
Sababu ya ubaguzi

Sonia kutoka Lebanon (sio jina lake halisi) amekuwa akitumia bangi kwa miaka mingi, lakini havitiwi na wazo la yeye kujiunga ama kuwa sehemu ya Kanisa hilo la Kimataifa la bangi.
Ameiambia BBC: "Sijali kuhusu kujaribu kuwa sehemu ya Kanisa, lakini sioni kama ni mmea mtakatifu. Kwake bangi imekwa kama nyenzo ya kumsaidia kukabiliana na masahibu yanayomsumbua.
"tunapovuta bangi mkiwa kundi, usiogope kuzungumza kitu cha kijinga, kiwango chako cha kufikiri wakato huo kinakuwa kidogo na tunacheka tunafikiri tuna akili sana. Kwa Sonia haoni kama bangi ina kitu kingine zaidi.
Moja ya malengo ya Kanisa la bangi ni kuondoa unyanyapaa wa kimaadili unaohusishwa na matumizi ya bangi. Tumemuuliza Lee Moloy huwa anawajibu nini wale ambao wanaona matumizi ya bangi kama kitu kibaya "Mawazo haya mengi yanatoka kwa wato wasioelewa, lakini ni ngumu kuwamabia watu hivyo haitaonekana vyema, kwa hiyo nawakaribisha wafanye utafiti na kusoma. Wakubali mawazo haya kwamba kitu cha asili kinatupa zawadi," anasema.














