Je, India inajiandaa vipi kwa ndege zisizo na rubani katika vita vya siku zijazo?

Serikali ya India huenda ikanjunua ndege mpya zisizo nz rubani kutoka Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Serikali ya India huenda ikanjunua ndege mpya zisizo nz rubani kutoka Marekani
Muda wa kusoma: Dakika 4

India inajaribu kuongeza uwezo wake wa kijeshi kwa kupata teknolojia ya hali ya juu ya ndege zisizo na rubani kupitia uvumbuzi wa ndani na ununuzi wa kigeni huku kukiwa na mvutano unaoendelea na nchi jirani za China na Pakistan.

Katika onyesho la hivi majuzi la teknolojia katika nyanja hii, Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Ulinzi ya India (DRDO) ilionyesha 'Drone Swarm' Novemba 17. Kulikuwa na ndege 25 zisizo na rubani katika kundi hili ambazo zilikuwa zikiruka pamoja.

Kundi hili la ndege zisizo na rubani lilionyesha hali kadhaa. Kwa mfano, kuzunguka eneo linalolengwa, kufanya shambulio lililopangwa, na kadhalika.

Kulingana na gazeti la Hindustan Times, onyesho la kwanza la aina hiyo ya ndege zisizo na rubani lilifanywa na jeshi la India mwezi Januari mwaka huu. Kisha ndege 75 za kiasili zilirushwa kwa wakati mmoja. Ndege hizi zisizo na rubani pia zilifanya oparesheni mbalimbali, zikiwemo za kukera.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa Twitter baada ya zoezi hilo la November 17, DRDO ilisema kuwa "Maabara ya Sayansi ya DRDO Young inayoshughulikia teknolojia ya Asymmetric (DYSLCT) inafanyia kazi teknolojia ya swarmili kuimarisha uwezo wa kivita]."

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

India inajaribu kupata ndege zisizo na rubani ili kuongeza uwezo wake wa kivita. Jeshi la India limekuwa likitumia ndege zisizo na rubani za kijasusi kwa miaka mingi. Nyingi za ndege zisizo na rubani katika jeshi la India ni za Israel.

Onyesho la ndege isiyo na rubani ya Buraq ya Pakistan wakati wa gwaride la kijeshi la 2015

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Onyesho la ndege isiyo na rubani ya Buraq ya Pakistan wakati wa gwaride la kijeshi la 2015

Hata hivyo, ushirikiano ambayo India imefanya na nchi kama vile Israel na Marekani katika miaka ya hivi karibuni unaonyesha kwamba India inashinikiza uwezo wa kuharibu ngome za adui kupitia ndege zisizo na rubani.

Kwa kuzingatia hali ya usalama ambayo imeundwa katika eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni, pia imekuwa hitaji la India.

Ikisisitiza hitaji la ndege zisizo na rubani, DRDO katika nakala ilisema kwamba shambulio la anga la Jeshi la Wanahewa la India nchini Pakistan mnamo Februari 2019 lingekuwa na ufanisi zaidi ikiwa ndege zisizo na rubani pia zingetumiw.

Masomo kutoka kwa Vita vya Azerbaijan-Armenia

Kwa muda mrefu, India imekuwa ikijaribu kutumia ndege zisizo na rubani katika mashambulizi yake kando na ujasusi. Wakati huo huo, mafunzo yaliyopatikana kutokana na vita vya mwaka jana kati ya Azerbaijan-Armenia pia yamesisitiza hitaji la India.

Wataalamu wa masuala ya kijeshi na ulinzi duniani kote wanakubali kwamba ndege zisizo na rubani zilichangia pakubwa katika ushindi wa Azerbaijan katika vita hivyo.

Vyombo vya habari vya India viliripoti kuhusu vita hivi na uongozi wa kijeshi wa nchi hiyo ulikuwa ukifuatilia matumizi ya ndege zisizo na rubani katika vita hivyo. Hasa Azerbaijan ilivyotumia ndege hizo kwa kiwango kikubwa.

Kiwango kikubwa cha ndege zisizo na rubani za Azerbaijan ziko Israel na Uturuki. India tayari inatumia ndege zisizo na rubani za Israel katika shughuli zake za kijasusi.

Mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya ulinzi Shekhar Gupta ameonya katika makala kwamba jirani hasimu wa India Pakistani huenda akanunua ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki kwa vile uongozi wa kisiasa wa nchi hizo mbili uko karibu.

तुर्की का ड्रोन

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa habari, mwezi Agosti mwaka huu, kampuni ya India ya DCM Shriram Industries imenunua asilimia 30 ya hisa za kampuni ya kutengeneza ndege zisizo na rubani za Uturuki Zyron Dynamics.

Ushirikiano kati ya kampuni hizi mbili za kibinafsi unaaminika kukuzwa na Serikali ya India na wakati mkataba huo unasainiwa huko Istanbul, Balozi wa India Sanjay Panda alikuwepo.

Pia imeangaziwa katika ripoti za vyombo vya habari kwamba DCM Shriram Industries na kampuni nyingine ya Zen Technology zinaweza kuchukua fursa ya sera mpya ya mdege zisizo na rubani ya Serikali ya India.

Lengo la sera mpya ya ndege zisizo na rubani ni kuifanya India kuwa kitovu cha utengenezaji wa ndege zisizo na rubani ifikapo 2030. Chini ya sera hii, makampuni ya kibinafsi yatapewa mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo na utafiti wa teknolojia ya ndege zisizo na rubani.

Kujikita katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya India imeongeza juhudi za kuandaa jeshi la mashambulizi ya fujo kwenye safu ya ya ndege zisizo na rubani za Marekani za Predator na Reaper.

Katika hali hii, India inaweza kupata matoleo 20 ya Sky Guardian na 10 Sea Guardian ya ndege isiyo na rubani ya MQ-9 Reaper kutoka Marekani. Inaaminika kuwa Marekani itatoa ndege hii isiyo na rubani kwa India kwa gharama inayokadiriwa ya dola bilioni tatu.

Kulingana na ripoti ya Dainik Jagran, India pia inaweza kuagiza ndege hii isiyo na rubani ifikapo Desemba mwaka huu.

Ndege ya kivita ya Uturuki isiyo na rubani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege ya kivita ya Uturuki isiyo na rubani

Wakati huo huo,kulingana na ripoti ya gazeti la India Today, India pia inaanza mchakato wa kupeleka silaha kwenye ndege isiyo na rubani aina ya Heron. iliyotengenezwa na Israel.

Israel itapeleka mabomu yanayoongozwa na leza na makombora ya kutoka angani hadi ardhini kwenye ndege hizi zisizo na rubani katika mradi wa pamoja na India kwa kima cha takriban dola milioni 400.

Zingatia uvumbuzi na uzalishaji ndani ya nchi

Mnamo Novemba 17, kundi la ndege zisizo na rubani la DRDO lilionyeshwa Jhansi kama sehemu ya mpango wa Azadi Ka Amrit Mahotsav ukiadhimishwa katika kukamilika kwa miaka 75 ya uhuru wa India.

Serikali ya India inasherehekea mafanikio ya nchi na kuhimiza kujitegemea.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Lengo la Serikali ya India kwa sasa ni kukuza uwezo wa mapambano ya kizazi kijacho Hili linaweza kufikiwa kupitia uvumbuzi na uzalishaji unakuzwa ndani.

Waziri Mkuu Narendra Modi alitweet, "Sheria mpya za ndege zisizo na rubani zitasaidia wanaoanza na vijana wanaofanya kazi katika uwanja huu na kuifanya India kuwa kitovu cha ndege zisizo na rubani kwa kuimarisha nguvu za India katika uvumbuzi, teknolojia na uhandisi."

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Kuna majukwaa kadhaa ya ndege zisizo na rubani zilizotengezwa nchini India ambayo yako katika hatua tofauti ya maendeleo na uendeshaji

Kulingana na ripoti ya India Today, ndege bora zaidi kati ya hizi zijazo ni mshambuliaji ambaye pia anaitwa 'lethal''.

Kulingana na ripoti hiyo, majaribio ya ndege hii isiyo na rubani, ambayo itakuwa msingi wa kikosi cha baadaye cha ndege zisizo na rubani, yameanza.