Orlan-10: Ifahamu ndege ya Urusi isiyo na rubani iliyodunguliwa na jeshi la Ukraine

Орлан-10

Chanzo cha picha, Мінобоорни Росії

Ndege hii ni ya hivi punde zaidi ya Urusi ambayo haijawai kutumiwa na Jeshi la Ukraine.

Lakini inatumiwa sana na jeshi la Urusi.

Novemba 16 makao makuu ya oparesheni za pamoja za jeshi yaliripoti kuwa mifumo ya elektroniki ilidungua ndege isiyo na rubani ya Orlan -10 ambayo ilivuka mstari wa mbele wa vita na kuingia eneo la Donetsk.

Орлан-10

Chanzo cha picha, Операція об'єднаних сил

"Jeshi limeitambua ndege iliyodunguliwa ya adui isiyokuwa na rubani. Ilitambuliwa kuwa aina ya Orlan-10 ya Urusi ambayo imeundwa kufanya upelelezi na kuelekeza makombora", makao hayo makuu ya jeshi yalisema.

Taarifa zaidi zilifichuliwa na kamanda wa jeshi la Ukraine Valery Zaluzhny.

Kulinga naye, ndege hii ni ya mwaka 2019; "Licha ya kuanguka kutoka umbali wa mita 2500, vifaa muhimu vya chombo hicho vilibaki salama," jenerali Zaluzhny alisema.

"Hii ndiyo ndege ya pili ya aina hiyo isiyo na rubani kudunguliwa na vikosi vya pamoja miezi michache iliyopita," aliongeza kamanda huyo.

"Kulingana naye, huu ni ushahidi wa uwepo wa wanajeshi wa Urusi, silaha na vifaa ndani ya ardhi ya Ukraine."Jeshi la Ukrain lilionyesha ndege isiyokuwa na rubani ya Orlan-10 huko Donbass, ndege hii hutumiwa kuelekeza mizinga na kwa ujasusi.

Орлан-10

Chanzo cha picha, Головнокомандувач ЗС України

Maelezo ya picha, "Орлан-10" приземлився фактично неушкодженим. Розібрали його вже на землі

Orlan-10

Orlan-10 ni ndege isiyo na rubani iliyoundwa miaka ya 2000 katika kituo maalum cha St. Petersburg Special Technological.

Inatajwa kuwa moja ya vifaa vya kisasa zaidi vya aina hii vinavyomilikiwa na jeshi la Urusi.

Ndege hiyo ina kamera za video zenye uwezo wa kuona kila upande na inaweza kupaa umbali wa kilomita tano, hali inayoifanya kutoonekana kwenye mifumo ya ulinzi.

Катапульта

Chanzo cha picha, Мінобоорни Росії

Orlan-10 - ya masafa ya kati, hutumika hadi umbali wa kilomita 120 kutoka kituo cha kuielekeza lakini bila kuelekezwa inaweza kuruka hadi umbali wa kilomita 600.

Inaweza kukaa hewani kwa muda wa saa 18 na kusafiri kwa kasi ya kati ya kilomita 90 hadi 150 kwa saa.

Inatumiwa kutuma data kwa wanajeshi ambao hutumia data hiyo kuelekeza mizinga.

Ndege nne za aina hiyo zinaweza kuelekezwa kutoka kifaa kimoja.

"Orlan-10" huko Donbass

Орлан-10

Chanzo cha picha, Міноборони Росії

Ndege aina ya Eagles-10 hazijawai kutumiwa na jeshi la Ukraine. Jeshi la urusi limetumia ndege hizi wakati wa mazoezi, kwenye oparesheni nchini Syria na hivi majuzi wakati wa oparesheni za kulinda amani huko Nagorno- Karabakh.

Jeshi la Ukraine limekuwa likilaumu makundu yanayoiunga mkono Urusi huko Donbas kwa kutumia ndege zisizo na rubani aina ya "Eagles-10" kwenye mstari wa mbele.

Oktoba mwaka 2018, ndege ya helikopta ya Ukraine aina ya Mi-24 ilidungua moja ya vifaa hivi karibu na Lysychansk, karibu na eneo lilipo jeshi la Ukraine la Luhansk.

Mamlaka za Urusi zinakanusha msaada wowote wa kijeshi na kiufundi kwa makundi yanayoipendelea Urusi.

Kundi la DNR halijatamka lolote juu ya ripoti ya ndege hiyo ya Orlan-10 isiyo na rubani iliyodunguliwa.

Орлан-10

Chanzo cha picha, Операція об'єднаних сил