Damon Galgut ashinda tuzo kwa riwaya ya 'tour de force' The Promise

Mwandhishi wa vitabu wa Afrika Kusini Damon Galgu ameshinda tuzo ya kifahari ya uandishi wa vitabu Booker Prize kwa tamthilia aliyoiandika baada ya kujaribu mara ya tatu kuwania tuzo hiyo.

Galgut, ambaye awali aliteuliwa katika mwaka miaka ya 2003 na 2010, alipokea zawadi ya pauni 50,000 katika sherehe iliyofanyika Jumatano.

The Promise ni riwaya yake ya tisa na ilifuatilia kwa miaka minne jinsi familia moja ya Afrika Kusini ilivyopungua kwa miongo minne kuanzia enzi ya ubaguzi wa rangi hadi leo.

Mwenyekiti wa majaji walioamua ushindi wake, Maya Jasanoff, aliielezea riwaya hiyo kama safari ya nguvu "a tour de force".

"Inajumuisha hadithi isiyo ya kawaida ,mandhari ya kuvutia na historia ya miaka 40 iliyopita ya Afrika Kusini kwa njia iliyobuniwa na kuundwa kuandikwa kwa ujuzi wa hali ya juu ," alisema.

"Iliweza kuvuta pamoja thamani ya msimulizi hadithi, ina mawazo mazuri, ni kitabu ambacho kina mengi ya kujifunza ,kikiwa na mvuto usio wa kawaida kwa muundo na mtindo wake wa kifasihi."

Jina la kitabu, The Promise, linamaanisha ahadi kwamba kijakazi wa familia ya mzungu atapewa nyumba atakayoishi na ardhi yake.

'Kitabu bora'

Uchambuzi wa Rebecca Jones, Mwandishi wa BBC wa Sanaa

The Promise cha Damon Galgut ni mshindi bora Kwa mtazamo wangu ni kitabu kilichojitokeza kwa ubora zaidi na ni vigumu kutokubaliana na hilo wakosoaji: "Bila shaka hiki ni mojawapo ya tamthilia bora ya mwaka ."

Kwanini? Kwa upande mmoja ni sakata inayoshika kasi, kufuatia kupungua na kuanguka kwa familia ya wazungu ya Afrika Kusini kwa kipindi cha miongo minne. Kimejaa matukio ya -ngono, mihadarati, ufyatuaji wa risasi- na kuna uigizaji, na kifo. Lakini kuna uchekeshaji mwingi usiotarajiwa ndani yake ambao unafurahisha. Kilinifanya nicheke.

Pia kiufundi wa uandishi ni kizuri sana. Kuna muelezaji asiyeonekana, ambaye anajifanya kama kamera ya filamu. Kwahiyo unapelekwa kiulaini kutoka eneo moja kwenda lingine, kutoka kituo kimoja cha muhusika kwenda kingine, wakati mwingine ndani ya ukurasa mmoja, au maelezo mafupi.

Wakati mmoja tulipaa ndani ya ndoto za mtu fulani. Wakati mwingine tukaingia ndani ya hisia za fisi n ahata familia ya mbwa.

Damon Galgut karibu afe kutokana na saratani alipokuwa mtoto mdogo. Katika mwaka 2010 aliniambia kuwa kilikuwa ni kipindi kigumu cha maisha yake.

Vitabu vilimfariji wakati wa ugonjwa wake. Wakati alipopona shinda moja aliyobaki nayo ni haja kubwa ya kuandika. Sasa ameshinda moja ya tuzo kubwa zaidi katika uchapishaji.

Kwa upande mwingine , ingawa kinatupa taswira ya familia hii moja, The Promise pia kinaelezea hadithi ya Afrika Kusini na kipindi chake kigumu cha mpito kuanzia kipindi cha ubaguzi wa rangi. Kwahiyo kimejaa taarifa nyingi zilizokusanywa katika kurasa chache, chini ya 300.

The Promise kilianza 1986 na kutembelea tena familia katika kipindi cha mazishi manne, kila mazishi katika muongo tofauti na katika wakati tofauti wa safari ya taifa.

"Kilichonivutia mimi kusema kwelli ni jinsi alivyoweza kuonesha katika kila kipengele jinsi muhusika mmoja anavyobadilika kadri muda unavyokwenda ," mwandishi alikiambia kipindi cha BBC Radio 4's Open Book mapema mwaka huu.

Galgut, mweney umri wa miaka 57, alikulia katika mji wa Pretoria na aliiambia BBC kwamba jina la kitabu pia linamaanisha kutotimizwa kwa ahadi katika Afrika Kusini baada ya ubaguzi wa rangi, sera ya ubaguzi wa rangi na utengeno ilitekelezwa na serikali ya wazungu walio wachache.

PICHA: Galgut alikuwa mmoja wa waandishi sita waliochaguliwa kwa ajili ya tuzo

"Ninadhani wengi wetu tulikuwa na matarajio ya hali ya juu ya siku zijazo," Galgut alisema. "Na nadhani wengi wetu tunahisi matumaini hayo yamepotea. Ile hati ya kipande cha ardhi ni moja ya ahadi ambazo hazikutimizwa, kusema kweli ."

Ahadi ilipongezwa na wengi wakati ilipochapishwa katika Uingereza mwezi Juni, huku gazeti la The Guardian likiita ya "kushangaza", gazeti la The Sunday Times liliielezea kama "iliyo gizani lalini iliyoelezewa kwa ubora zaidi" nalo The Financial Times likiitangaza kama "ngumu, ya matamanio, kazi nzuri ".

Waandishi wengine ambao vitabu vyao viliteuliwa kwa tuzo walikuwa ni:

  • Anuk Arudpragasam - A Passage North
  • Patricia Lockwood - No One Is Talking About This
  • Nadifa Mohamed - The Fortune Men
  • Richard Powers - Bewilderment
  • Maggie Shipstead - Great Circle

Tuzo ya m =waka jana ya Booker alishinda Douglas Stuart kwa kitabu chake cha Shuggie Bain. Mwandishi huyo Mskochi alisema ushindi "kwangu ulibadilisha kila kitu", tamthilia yake iliongoza katika orodha ya vitabu vilivyouzwa zaidi na sasa inaandaliwa kwa ajili ya kipindi cha televisheni.