Kwanini Iran ilipeleka silaha kali za kijeshi katika mpaka wake na Azerbaijan?

Chanzo cha picha, Anadolu Agency
Moto unafukuta kwenye uhusiano baina ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan, licha ya kwamba nchi hiyo ya Azerbaijan ni changa, mzozo wa kisiasa na sera za kigeni baina yao unafuatiliwa kwa karibu.
Uwepo wa majeshi ya Iran kwenye mpaka na Azeberbaijan sio suala ambalo Elham Aliyev ama waangalizi wengine wanafuatilia maendeleo ya siasa za kimataifa huko mashariki ya kati.
Hakuna tatizo la amani kwenye mpaka wa Iran na majirani zake, tangu vita vya Azerbaijan-Armenia katika miongo mitatu iliyopita.
Hata hivyo tangu mwaka 1947, wakati majeshi ya Soviet yalipoivamia Iran na kuvuka mpaka wa Tehran, hakujawahi kuwa na tishio lolote kubwa la kiusalama dhidi ya Iran kwenye eneo hilo la mpaka. Na limekuwa eneo salama tangu miaka ya 1990s
Hata hivyo taarifa za uwepo wa majeshi na silaha za kijeshi za Iran katika mpaka huo, kumeibua maswali. Kwanini sasa? Aliuliza Rais wa Azerbaijan kupinga hatua hiyo ya Iran. Nini kimebadilika kufanya Iran kuleta hofu kwenye mpaka?

Chanzo cha picha, Getty Images
Tembo chumbani
Nchi iliyoko kilomita 1,400 kutoka mpaka wa Iran na Azerbaijan, lakini inaonekana kuwa kivuli tangu mwaka wa kwanza Azerbaijan ipate uhuru na imekuwa muhimu kwenye uhusiano wa Tehran na Baku..
Ingawa uhusiano kati ya Baku na Tel Aviv sio jambo geni kutokana na ukaribu angalau katika miaka mitano iliyopita, ikionyesha pia chanzo cha matatizo ya Iran yapo kwenye uhusiano huu wa kimkakati wa nchi hizi mbili, ambao unazidi kukua siku hadi siku.
Israel ilikuwa nchi ya mwanzo kabisa kutambua uhuru. Azerbaijan na miezi michache baadae serekali mpya ya Azerbaijan nayo ikajiunga na nchi kadhaa zilizokuwa zinaitambua Israel.
Hatua hiyo ikaimarisha vyema uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Sasa uhusiano wa Azerbaijan-Israel si wa kutikiswa kirahisi. Kwa Israel, Azerbaijan ni nchi ya kiislam, tofauti na nchi zingine ni rafiki wa kihistoria inayomsaidia kukabiliana na wasioitaka Israel ambao wanatajwa kuwa ni Iran.
Kwa Azerbaijan, Israel ni njia muhimu ya kukimbilia iliyowasaidia kuwa huru dhidi ya Urusi na kutumia kujijenga kwa ulinzi wake binafsi.
Kiuhalisia, Iran haijawahi kuupenda uhusiano huu, lakini haijaweza kuuzuia kiurahisi. Hata hivyo Waazabaijan pia walijaribu kujiepusha na vitendo vya uchochezi, hasa kuhusu suala la utumiaji wa vikosi vya kijeshi vya Azerbaijan katika eneo la mpaka wa nchi hiyo.
Katika miongo miwili iliyopita, uhusiano huu ulichukua sura mpaka baada ya kufunguliwa kwa bomba la kusafirishia mafuta la BTC mwaka 2006, linalosafirisha mafuta ya Azerbaijan kuelekea bahari ya Mediterania na kuongeza mafuta yanayosafirishwa nje zaidi hasa Israel. Asilimia 40% ya mafuta ya Israel yanatoka Azerbaijan, kiuchumi uhusiano huo ni muhimu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka 2012, waziri wa kigeni wa Israel wakati huo Avigdor Lieberman alisema, "Azerbaijan ni nchi muhimu kwa Israel kuliko Ufaransa," pengine alikuwa anajua siri zaidi za ndani kwenye uhusiano uliopo wa nchi yake ya Israel na Azerbaijan.
Israel yenyewe imekuwa muuzaji mkubwa wa silaha kwa Aberzaijan. Kwa mujibu ewa takwimu kutoka
69% ya silaha zote za Azerbaijan zilizonunuliwa kati ya mwaka 2016 na 2020 zimetengenezwa Israel.
Moto unafukuta

Chanzo cha picha, Getty Images
Taarifa kwamba kuna silaha za kivita za IRGC kwenye mpaka wa Azerbaijan na Iran kwenye mto Aras , zinaonyesha kwamba watu walioko Tehran ambao wanaamua sera za kigeni za Iran kwamba hawawezi kufanya maamuzi ya mabadiliko hayo.
Kilichotokea kinaweza kusababisha mabadiliko makubwa, lakini kwa miongo kadhaa sasa kuna moto unafukuta kuhusu na uhusiano wa Tehran-Baku, na kinachotokea sasa kinazidi kuchochea moto huo.
Iran inawatuhumu iliyowaita maadui zake wa nje kwa kujaribu kuleta chokochoko kwenye uhusiano wao kati ya Baku na Tehran. Kama Azerbaijan haitabadili utaratibu wake wa kukubaliana na vikosi na silaha za kijeshi za Iran kwenye mpaka wake huenda moto unaofukuta ukawaka siku si nyingi












